Vijana tusipande penzi pasipo mapenzi...!!

Vijana tusipande penzi pasipo mapenzi...!!

Joined
Oct 15, 2013
Posts
9
Reaction score
2
Imekua ni kawaida sana katika jamii yetu kuskia vioja vitokanavyo na mapenzi: mara utaskia "anywa sumu, ajinyonga" na mengineyo yanayochukiza ambayo hayaleti haiba nzuri kwa jamii haswa kwa vijana ambao ndio hasa msingi wa Tanzania yetu ya kesho... Nikiingia kwenye mzizi wa mada yangu hii, moja kwa moja naipeleka kwa vijana wa kiume. Ki ukweli matatizo mengi katika mahusiano hasa ya kimapenzi yamechangiwa kwa kiasi kikubwa na tabia ya wanaume wengi ambao walijikuta wakiendeshwa na hisia na mihemko yao ya kimwili ambayo ni ya mda mfupi, iliyopelekea kutumia mali walizokua nazo ambazo zinatamanika machoni pa wanawake wengi kwa lengo la kuwa nao kama wapenzi wao, huku wakijua fika kwamba hakukua na msingi wa mapenzi ya kweli ambayo hutoka rohoni. Hatima yake vijana wengi wakajikuta wakipanda penzi kwa wanawake wasiokua na mapenzi kwao, bali walikubalika kwa misingi ya pesa na vitu vionekanavyo kwa macho. Hatima yake ni kuporomoka kwa maadili ya jamii, uaminifu katika jamii umepotea, ndoa nyingi zinavunjika, vijana wengi wamepoteza hamasa ya kujenga familia sio kama zamani na kikubwa zaidi kama alivyosema mwanauchumi maarufu Joseph Stiglitz kwamba "countries behave like individuals"..... inamaanisha kuwa uchumi wa kijamii unaporomoka.......... Hivyo vijana wenzangu haswa wa kiume ambao historia, dini, mila na desturi zinatupendelea dhidi ya wenzetu kambi ya upinzani (KE), inatupasa turudie misingi mizuri ya kuanzisha mahusiano " TUSIJE PANDA PENZI PASIPO MAPENZI" ,,,,,:crying::crying:
 
Hahaha nimeipenda mada yako ila tatizo linakuja nitajuaje kama nimepanda kwenye mapenzi ya kweli kwani wanaume wenyeww maopportunistiiiiiii hapandi penzi pasipo mpenzi mwenye ajira au kujiajiri
 
Nyerere inawezekana ukawa sahihi kwa upande mmoja... ila kumbuka nadharia mara nyingi ndio huwa haswaa inajenga umbo la nje...... hata gari lilianza kuundwa kutoka kwenye nadharia. Kuwa na nadharia ni mwanzo mzuri, vivyo hivo katika mapenzi. kuwa na nadharia nyingi kichwani kunaweza saidia kwa kiasi..
 
Sista! ki ukweli waweza jua binadamu tunauwezo mkubwa sana wa kupambanua na hata kwa kiasi Fulani mambo ya baadaye, sema tatizo linatokana na tamaa na mihemko ya mda mfupi. But, for sure! tunaweza jua kabisa kama penzi hili ni la kweli au lah!.... mfano mdogo tu sista, ni mara ngapi umefanya jambo ambalo uliliona kama ni baya na ukaamua kufanya tu, bila kujali athari zake na ukasema "potelea mbali"........... akili zetu zina ewezo mkubwa sana wa kufikiri... (wanasayansi wanasema, ni watu wachache tu wameweza kutumia angalau asilimia 10 ya uwezo wa ubongo wao kufikiria)....
 
Nyerere inawezekana ukawa sahihi kwa upande mmoja... ila kumbuka nadharia mara nyingi ndio huwa haswaa inajenga umbo la nje...... hata gari lilianza kuundwa kutoka kwenye nadharia. Kuwa na nadharia ni mwanzo mzuri, vivyo hivo katika mapenzi. kuwa na nadharia nyingi kichwani kunaweza saidia kwa kiasi..

Asante mkuu, lakini jaribu kufikiri kwa mapana fiziolojia ya mwili wa binadamu. Mwanaume ni tofauti sana na mwanamke inapokuja kwenye hisia za mapenzi. Nguvu ya mapenzi ni kubwa sana mnapokuwa mbalimbali, kila mmoja akimuwakia tamaa mwenzake. Lakini pale unapoishi chumba kimoja, inahitaji kusomana sana ili muweze kulinda hisia zenu. Siku ya kwanza, unatoka asubuhi unarudi jioni unakutana na sura ile ile chumbani, wiki ya kwanza, mwezi wa kwanza, mwaka wa kwanza etc. Si suala dogo hili, na hapa ndipo huwachanganya watu na kuanza kutafuta mawindo pembeni.

Ukiwa nje ya ndoa ni rahisi sana kunyoosha kidole kwa wengine. Ukishaingia sayansi ya ndoa ni tofauti kabisa. Tofauti ya ndoa zenye furaha (japo kwa nje) na zisizo na furaha ni kiwango cha kuvumiliana na kuchukuliana. Na hapo ndipo penye hekima.
 
unaneno la msingi ila kumbuka kwamba kuweza kutenganisha penzi la kweli na la uongo ni ngumu sana..kunatofauti ndogo mno hasa katika dunia hii ambayo mbwa mwitu wamevaa ngozi za kondoo. Acha yale unayoyaona na kujua kabisa tena kwa uwazi kwamba yapoje.
 
ni kweli kabisa ila mi nachojua kitu kinachoitwa mapenzi ni kama 'ambiguity' au ni kama hakuna kitu mapenzi,yaani ni kwamba sisi binadamu huwa tunatamaniana tu sasa huko kutamaniana ndio wengine tunaona au ndio tunaita mapenzi,but when you speak about mapenzi to me frankly speaking its something so complicated i can't even define it.
I submit,
 
Back
Top Bottom