ndege JOHN
JF-Expert Member
- Aug 5, 2015
- 25,065
- 61,402
Yaani inafikia kipindi hata 10000 ya kununua nguo inakushinda unaona Bora upotezee hamna haja ya nguo mpya.kingine tunakimbia mpaka wAnawake zetu kwa sababu hatuna Cha kuwapa hela ya kula yenyewe inatushinda utapata wapi ya kumpa Mwanamke.unachukua mzigo wa laki mbili let's say kutoka ubungo unaenda kuuza gongo la mboto faida utashangaa unapata 5000 bado hujala hapo.mwisho wa siku unakula na msingi wa biashara wenyewe.vijana wengi Sana hapa mjini hawana hata sehemu ya kukaa kwa sasa.mjini hapa angalau ili uishi vizuri uwe na uhakika wa 20000 kwa siku Sasa kama hata 5000 hupati mpaka ukomae saaana.kwa Hali Kama hio mnadhani mawazo yataishaje ukipiga picha unaona washkaji wana drive mandinga barabarani hawana habari magari kibao,watu nyomi Kama kawaida huu mji buana kabla hujaja unaona life zuri ndo lipo Huku ukishaingia kwenye jiji ndo Sasa unapagawa kukuta mambo sivyo sio poa kabisa.