Vijana tujiunge vyama vya upinzani

Vijana tujiunge vyama vya upinzani

.... Vijana Hawapendi Kupiga Kura, Mfano Angalia Uandikishaji Wa Wapiga Kura Wamejaa Wanawake Tu
 
Swala ni kugombea. Kuambiwa Vijana tunatumika tukatae kabisa. Mfano mimi natngaza nia ya Kugombea Udiwani kata fulani huku Mbinga_Ruvuma
 
Nhnnnn..... nafikiri twende zaidi ya kugombea na kupiga kura. Si kitogonji, kijiji au jimbo, kwa sasa wasimamizi wa ccm wanabadirisha matokeo kweupe. Ushindi wa chadema unaenda ccm na kushindwa kwa ccm kunaenda chadema. Isingiro mjini wamefanya hivyo, Kijiji cha Kitoma jimbo hilo hilo la Kyerwa kata Rukuraijo wamefanya hivyo. Niliona ITV jana, Jimbo la Kawe wamefanya hivyo.

Bahati mbaya tunarazimishwa kwenda mahakamani ktk matukio kama hayo.....tupoteze muda, fedha na wakati mwingine mahakimu wasio na maadili kuhukumu kesi hizo watakavyo wao. Tufikirie zaidi ya kugombea na kupiga kura....
 
mimi nimehamasika pia,sikuwahi kupiga kura before ila mwakani nitaitumia vema haki yangu ya kikatiba,ni wajibu wetu kulikomboa taifa kutoka kwa mafedhuli ccm.
 
Vyama vya upinzani nchini wawewaangalifu sanaa na Daftari la kudumu/ uboreshaji wa daftari la wapiga kura hafu cha msingi kwamba vijana wengi ambao ndo wapiga kura wakubwa wa upizani huwa hawapigi kura kisa hakujiandikisha kwenye kituo husika hususani ni vijana wa vyuo vikuu nchini wakati wa uchaguzi wapo field/likizo nyumbani na wanajiandikisha vyuoni. Ikiwezekana wapewe fursa moja tu kwa nafasi ya rais pekee ikitokea hivyo au uchaguzi ubadilishwe mpk Dec au mwishoni mwa Nov!.
 
Ni vyema vijana tubakie bila vyama ili tuwe na akili na fikra huru,ukishajiingiza kwenye vyama tu utapateza uwezo wako wa reasoning maana kila jambo utalitazama kwa kutumia miwani ya kiitikadi (ideological blinkers) badala ya kulitazama jambo kulingana na facts zilizopo mezani..
 
Vijana wenzangu,

Popote ulipo, ndani ya Tanzania ama nje ya Tanzania. Tafuta Chama cho chote cha Upinzani kujiunga nacho na ugombee uongozi. Kuendelea kuishabikia CCM ni kuendeleza umaskini na rasilimali za Taifa kuibiwa na kikundi kidogo. Jana uliona mwenyewe jinsi Mhe. Rais amabye ni mwenyekiti wa Taifa wa CCM alivyowatetea kwa nguvu zote mafisadi wa mali za Umma.
Tuige mifano ya akina Zitto, Machali, Kafulilla, Mnyika,Silinde…..Kuimarisha hivyo vyama ili ikifika mwakani wakati wa uchaguzi kila chama kwa sehemu yake ama mwavuli wa upinzani visimamishe wagombea kila sehemu na tuweze kuiondoa ccm madarakani. Tutaendelea kulialia hadi lini? Nguvu, Nia na Uwezo tunao. Tuamke wakati ndiyo huu. Wananchi wanatusubiri, Wazee wamechoka.

Sio vijana tu na wazee pia. Niliongea na shangazi yangu kijijini nikamuuliza kuhusu hotuba ya JK jana . Jibu alilotoa nimecheka. Wanasema Kikwete hana BEJI.
 
Back
Top Bottom