Vijana na siasa Chadema

Vijana na siasa Chadema

ndiwela

Member
Joined
Jul 19, 2012
Posts
25
Reaction score
4
Mi naona kama huna dhamira ya dhati kisiasa (usifanye siasa sehemu ya kuganga njaa) ni bora ukakaa pembeni uwaachie wenzako wenye dhamira ya dhati. Matokeo ya watu wanaoingia kwenye siasa kwa sababu ya njaa zao (ubinfsi) ndio tunayoyaona yakitokea Bavicha (gazeti la leo January 7 J3 2013 la Tanzania daima sauti ya watu na mwananchi). Kama ni kweli wameyafanya haya wale wote wanaotuhumiwa akiwemo dada yangu Juliana Shonza, Mtela Mwampamba na Mchange Kupokea fedha ili kuwachafua viongozi wa chama chao ni mchezo usiofaa hata kidogo kwenye siasa, niseme tu mi napinga kwa nguvu zangu zote tabia ya aina hii.Kwani kufanya mambo kama hayo kuna kuondolewa heshima na imani kwa jamii ambapo kuirudisha tena inakuwa ni ndoto.

Binafsi sikutegemea hao ndugu zangu kutuhumiwa kwa kashfa kama hizo ni fedheha na aibu kubwa katika jamii ukizingatia kuwa jamii iliwategemea sana kuwa mngekuwa wakombozi wao,tena vijana ambao ndio tuko mstari wa mbele kwenye harakati za kupinga vitendo vya rushwa, udhalimu, unyanyasaji, na mambo yafananayo na hayo ambapo tuliona kwamba wazee wetu wameshindwa kutekeleza na tukitegemea kuwakabidhi vijana Rungu, leo hii mmeanza kuonesha tabia chafu namna hii! Kwa hiyo mnataka kudhihirisha na kuwapa sifa wazee wanaosema vijana ni wahuni na si vema wakapewa nchi licha ya kuwa wana nguvu nyingi. Tukiendelea kuchukua hongo kutoka kwa akina shibuda na wengine kama mnavyofanya vijana wenzangu zile harakati za kupambana na mafisadi papa sijui wengine wanaita Nyangumi zitafanikiwa kweli? Mi naona hapa tukiendekeza tabia hizi harakati zetu za kujikomboa kwa wanyonyaji hazitafanikiwa.

Hivi kwanini hatujifunzi kutoka kwa wanasiasa kama akina Mh. Edward Lowasa aliyekuwa waziri mkuu, angalia jinsi anavyotaabika kurudisha heshima na imani aliyokuwa amejijengea kwa jamii, na ukae ukijua Lowasa ni mtu ambaye amejitosheleza kiuchumi (yuko vizuri financially) kiasi kwamba angeweza kusema ngoja akapumzike na wamasai wenzake huko Monduli kusingekuwa na tatizo lolote lakusumbua linalohusiana na fedha. Lakini anajua thamani ya heshima na ndio maana anahaha huku na kule kwa gharama yoyote ile kuirejesha hiyo heshima yake.
 
Back
Top Bottom