lusekelo Andrew
Member
- Dec 10, 2012
- 62
- 19
Nilipotoa maoni yangu kwenye Tume ya kukusanya maoni ya katiba mpya, niligusia umuhumu wa uwepo wa sera za Kitaifa kwajili ya rasilimali za taifa na uwepo wa uwazi katika mikataba inayoingiwa na serikali (kwa niaba yetu, wananchi) hasa juu ya rasilimali zetu. pia kwa kirefu sana, zilipotokea vurugu juu ya swala la gesi, mtwara, niliandika walaka wa "UMUHIMU WA KUWEPO SERA ZA KITAIFA JUU YA MAMBO NYETI YA KITAIFA" hapa kwenye www.lusecky.blogspot.com . sasa, Ijumaa, Wabunge wamepewa Rasimu (Draft) ya SERA YA GESI. Nikafarijika, angalau mwanzo mzuri. Nikajipanga kuitafuta na kuipitia rasimu hii, na kuandaa waraka kuhusu mtazamo na maoni yangu juu ya swala hili, na kuuwasirisha bungeni (kwa baadhi ya wabunge) mapema June.
Jana nimeipata rasimu ya sera ya gesi, Imetolewa kwa lugha ya kiingereza! hivi watanzania wangapi wanaweza wakasoma na kuelewa lugha hii, ili watoe maoni juu ya rasilimali yao? Jamani, tunakua watumwa na lugha za watu, hata kwenye mambo ya kitaifa ya msingi kama haya! Wakati juzi, kwenye website yao, wazara ya madini walitoa taarifa kwa umma Faida za gesi asilia mikoa ya Lindi na Mtwara kwa Kiswahili, kwanini rasimu, ambayo watanzania wana haki ya kutoa maoni yao, iletwe kwa kiingereza? Kwa manufaa ya nani? Hii ndio lugha inayoeleweka na watanzania (wenye rasilimali husika) wote? Mizaha hii kwenye rasilimali na mambo nyeti ya kitaifa, itakoma lini?. Ni Lazima serikali ijue, kua rasilimali za Taifa ni mali ya watanzania wote, hakuna mwenye haki miliki, serikali imepewa dhamana TU! Ya kusimamiia rasilimali za taifa, lakini hii haiondoi wala kupunguza nafasi ya mwananchi kutoa maoni juu ya usimamizi na uendeshaji wa rasilimali kwa manufaa ya taifa-kizazi hiki na vijavyo pia.
Nimeendelea kuwahimiza vijana, kufuatilia, kusoma na kutoa maoni yao juu ya swala hili la sera ya Gesi Asilia pamoja na zingine zote zitakazofuata kuhusu rasilimali za Taifa letu. Bado nasisitiza tena, hasa vijana, tusome rasimu hii na tutoe maoni yetu mapema, juu ya sula la gesi, hizi ni rasilimali za wananchi, hivyo, kila mwananchi anahaki ya kusimamia rasilimali hii, na nyingine pia. Vijana tusikae kimya, au kupuzia mambo ya msingi ya taifa letu, tu kwa mihemko na kisiasa, Taifa ni letu.
Kuisoma/copy rasimu hii, ingia hapa. Economist Lua