Vijana lini tutabadilika

Vijana lini tutabadilika

UMUGHAKA

JF-Expert Member
Joined
Sep 1, 2021
Posts
3,104
Reaction score
14,258
Habari ndugu wanajukwaa wote, poleni na mihangaiko ya kimaisha ya kila siku, poleni pia kwa kupanda kwa gharama za maisha, tuendelee kupambana kwa kumshirikisha Mungu, kama hujapata leo usikate tamaa uenda kesho ikawa yako!.


HOJA

Nimekuwa nikihuzunishwa sana na vijana(wengi) wa hili taifa la Tanganyika lenye historia lukuki za kujivunia. Imefika sehemu kiukweli nimeshindwa kuvumilia namna vijana walio wengi wa hili taifa kwa namna walivyo wapumbavu, wajinga na mazwazwa.

Hivi ni lini mtaacha hizi tabia za kijinga za kujipendekeza? mnajipendekeza kwa lipi hasa? aliyewadanganya ili maisha yasonge ni lazima ujipendekeze ni nani?

Hivi hizi nguvu za kuandamana kumpongeza Rais mkisema anaupiga mwingi baada ya kutumia Bilioni 7 kwenye filamu yenye low quality mnazitoa wapi?

Vijana wa hii nchi ni nani aliyewaroga? Tatizo ni nini? Kwani vichwani mmbeba hizi hizi akili ambazo Mungu alituwekea baada ya kutuumba au nyie mlipelekwa gereji mkapigwa spana ubongo ukatolewa wakaweka oil chafu?

Nilitegemea muandamane kutetea na kuishinikiza serikali kuwapatia vijana wenzenu ruzuku kutokana na kuunguliwa na mabanda yao pale Karume na kwingineko katika nchi, nilitegemea mtaandamana na kuishinika serikali kuangalia namna bora ya kupunguza tozo kwenye mafuta ili maisha ya mtanzania yapate nafuu!, nilitegemea muandamane na kuishinikiza serikali kuwashughulikia waliotajwa kwenye ripoti ya CAG kwa kashfa ya ubadhirifu wa mali ya uma!

Nilitegemea kuona mnaishinikiza serikali kuwekeza kwenye kilimo hasa kuweka mtaji mkubwa kwenye benki ya kilimo ili vijana wakope wakalime wapige pesa kuliko kukaa na kuuza barakoa kwenye mageti ya kila Halmashauri nchini Tanzania.

Kwahiyo mnaona ni bora muendelee kuuza barakoa kuliko kuwekewa mazingira mazuri ya mikopo ili iwatajirishe na kuwanufaisha kwa maisha ya baadae.

Mnaona ni bora kuimba "Mama anaupiga mwingi" lakini hamtaki kutoka kwenye foleni za magari na kulazimisha kusafisha vioo vya magari na kupewa 200.

Kila taasisi kwenye hii nchi inanuka rushwa kwa mujibu wa ripoti ya CAG, nyie mnaona mnapoteza muda na haina maslahi kuishinikiza serikali iwajibike ila kwenu lililobora ni kuimba "Mama anaupiga mwingi"

Nawauliza tena- VIJANA WA KITANZANIA NI NANI ALIWAROGA?

Kwa sehemu kubwa nilitegemea vijana ndio mngekuwa mstari wa mbele kuwapigania watanzania lakini imekuwa kinyume chake!!

NI RAHISI KUMBADILI INZI AKILI AKATOA ASALI KULIKO KUIBADILI AKILI YA KIJANA MPUMBAVU WA KITANZANIA.
 
walioleta uchawa nchi hii ndo walioharibu kila kitu .... inasikitisha yaan huoni professionalism , creativity zero kbs etc. Imagine media za bongo zina mavipindi mengi ya hovyo wamejikita kwenye umbea cz ndio content wabongo wengi wanapenda ,badala yakutumia muda mwingi kuhamasisha umma juu ya faida za EAC , SADC na tufanyaje kupata izo fursa, Wakenya apo na wazambia Wana take advantage ya izi blocs kukuza uchumi wao, ila vijana wa bongo wamelala tu.
Nway ,acha tuwe wapole .
 
Wale siyo vijana. Ni unemployed youth walikusanywa kwa malipo ya sh. 2000 na Tshirt. Ni kazi waliajiriwa kuifanya na wameifanya.
 
Nisipo jipendekeza nitakula wapi boss
Au nyinyi mshapata ulaji ?



Hapa kuna mdau yupo wizara fulani najipendekeza sana kwake kumsifia kumpa misifa na misalamu kama yote hivi sina ajira nimesoma anajua basi utaskia dogo mwezi wa saba wa bajeti sikuachi uwe kitaa wala wasiyamwage tu



We achana na sisi tukikaa maskani mnatuita waizi
 
Nisipo jipendekeza nitakula wapi boss
Au nyinyi mshapata ulaji ?



Hapa kuna mdau yupo wizara fulani najipendekeza sana kwake kumsifia kumpa misifa na misalamu kama yote hivi sina ajira nimesoma anajua basi utaskia dogo mwezi wa saba wa bajeti sikuachi uwe kitaa wala wasiyamwage tu



We achana na sisi tukikaa maskani mnatuita waizi
Pole sana. Pambana sana. Utatoboa tu.
 
Back
Top Bottom