Vijana: JPM tumbua jipu kodi za nyumba

singidadodoma

JF-Expert Member
Nov 11, 2013
4,394
1,536
BILA shaka upo salama na unaendelea na kuifurahia ‘wikiendi’.
Sitachoka kukukumbusha kuhusu kesho, timiza wajibu wako kwa sababu leo unayafanya unayoyafanya kwa sababu una nguvu za ujana. Kesho ina mambo mengi likiwemo suala la makazi ambalo ninaamini kutokana na sababu kadhaa ni vijana wachache wamemudu kuwa na nyumba zao.
Wengi wao wamepanga, baadhi yao hasa mijini, kila iitwapo leo ‘wanaumia’ kwa kufiria kodi ambazo, katika hali halisi ni kubwa kulinganisha na vipato vyao. Hawana namna, wamekuja mjini ‘kutafuta maisha’, hawana nyumba zao na wanahitaji kuwa na pa kuishi, lazima wapange.
Hakuna bei elekezi ya chumba au nyumba kama ilivyo kwa lita moja ya dizeli au petrol. Hakuna sheria inayowalazimisha wenye nyumba kupanga kiasi cha kodi kulingana na vigezo fulani. Suala la kodi za nyumba linafanywa kiholela, hakuna anayejali nani analipa nini, anamlipa nani, vipi, wapi kwa vigezo vipi.
Udhaifu wa mamlaka za Serikali kutosimamia suala hilo imekuwa mzigo mzito kwa wapangaji, na unaisababishia serikali hasara kwa sababu wenye nyumba wanatoza kodi lakini wao hawalipi kodi ya mapato.
Huko nyuma kulikuwa na Sheria ya Udhibiti wa Pango ya Mwaka 1984, Bunge liliifuta mwaka 2005, mpangaji kaachwa ajitetee yeye kwa kunung’unika au kumnyenyekea mwenye nyumba. Usishangae kumuona mpangaji anakuwa mnyonge kwa mwenye nyumba, mazingira yanamlazimisha, ndiyo hali halisi.
Kwa sababu hakuna sheria, kwenye suala la kiwango cha kodi ya nyumba anachoweza kufanya mpangaji ni kuumia kimya kimya, hana haki ya kuhoji ukubwa wa kiwango cha kodi anachoelezwa au kukipinga, kujua vigezo vilivyotumika kukipata kiwango husika.
Mpangaji, anatambua wajibu wa kulipa kodi kulingana na mkataba, lakini hana haki ya kukataa uamuzi wa mwenye nyumba wa kulipa kodi ya mwaka au miezi sita na hakuna anayemtetea. Kwa hali ilivyo, mwenye nyumba kaachwa afanye anavyojisikia, aamue anachotaka, kwa wakati anaotaka yeye, hii si sawa, hili ni jipu na limeshaiva, litumbuliwe haraka.
Serikali lazima itazame upya suala la kodi za nyumba kwa ujumla wake ikiwa ni pamoja na mfumo, viwango, na utaratibu wa kulipa ili wapangaji wawe na haki badala ya kujiona wanyonge kwa wenye nyumba. Kumlazimisha mpangaji alipe kodi ya mwaka au miezi sita wakati yeye analipwa mshahara kwa mwezi ni unyanyasaji.
Uhuru wa mwenye nyumba kupandisha kodi kadri anavyojisikia si sahihi, ni udhaifu katika usimamizi wa mambo ya msingi yenye maslahi kwa mwananchi na taifa. Kupangisha nyumba ni biashara, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wana sababu zipi za msingi kuhalalisha kuwaacha wenye nyumba wasilipe kodi ya mapato?
Serikali inaifahamu mikataba ya wenye nyumba na wapangaji? Kwa nini wapangaji hawapewi risiti za kodi wanazolipa? Wenye nyumba wasipewe uhuru kuliko wanavyostahili, lazima kuwe na sheria inayohusu kodi za nyumba ili mwenye nyumba na mpangaji wapate haki kwa mujibu wa sheria.
Nchi nyingi zina sheria ya kudhibiti pango, na kuna sehemu ambako ni marufuku kutoza kodi ya zaidi ya miezi miwili. Watanzania wamenung’unika sana sasa inatosha.
bmsongo@ gmail.com

Habari leo
 
Nimewahi kusikia kuna chama kinahusika na maswala ya wapangaji sijui kama kipo hai?hiki kingekuwa na jukumu la kuwaunganisha makundi yote ya wapangaji na kukuza sauti yao kwani kwa kweli kuna haja ya serikali kuangalia kwa jicho la huruma sekta hii ya upangaji wa nyumba.
 
Una hoja japo hoja yako ina ukakasi.

Hebu fikiria mtu kajenga Nyumba kwa 60-80 Millions, afu anapangisha chumba kimoja kwa 50 elf na Nyumba inavyumba 4 hivyo kwa mwezi ana laki 2.Je,itamchukua mda gani kurudisha capital yake ili aanze kupata faida?

Nadhani Mara nyingi Nyumba za kupangisha ni msaada kwa wapangaji na si biashara,ni njia ya kutunza mali "in terms of fixed assets".

Sasa kiasi cha 50 elfu kwa mwezi kipunguzwe kama unavyotaka na kifikie labda 20-25 elfu kwa mwezi,unadhani mwenye Nyumba atakuwa amekujengea Nyumba kwa manufaa yako au biashara.?

Unasema wapangaji walipe kwa mwezi, yaani ndo kuzidi kumdidimiza mwenye nyumba kwa kutonufaikia hata kwa hicho kidogo.

Nadhani suruhisho hapa,ni kama ifuatavyo..

1.Serikali inatakiwa iwekeze kwenye kujenga Nyumba kupitia National housing kisha kuwapangisha Wananchi kwa gharama nafuu.Isiwe kama biashara,iwe Huduma kama ilivyo Umeme na Maji.

2.Serikali ijitahidi kuimarisha uchumi wa nchi ili kupunguza makali ya maisha magumu kwa wananchi wake hivyo kuweza kumudu angalau basics needs kama vile Malazi n.k

3.Utashi wa kuanzisha viwanda kwa dhamira ya kweli ni kichocheo cha suruhu namba 2 hapo juu.
 
jmn mbona tunapwaya kwn hayo mnayasema nyie ila mtekelezaji akiyatekelza mnasema dikteta ebu tuwe wa kweli hiv ni kweli mtu nyumba kajenga kwa gharama zake hlf mtu aje apange bei kwan unajua mjengo ukisimama unagharm sh ngap ebu achen mengine yapite we km umeshindwa mjin rud kijijini bhana
 
Kiuhalisia upangishaji nyumba sio biashara bali ni huduma, tukitaka mdhibiti basi kodi hazitabebeka, mfano kwa yale maeneo ambayo yanefanyiwa tathmini nyumba za biashara wenye nyumba wanalipa property tax ya 6% ya thamani ya nyumba hivyo tukifuata priciple za biashara huyu mwenye nyumba ili apate faida inabidi apige hesabu za gharama zake zote na faida juu ili aweze kupata kiwango cha kodi stahili jambo litakalopandisha sana kodi
 
Chamuhimi serikali kupitia NHC ijenge nyumba kwawingi pia ipunguze mikodi ili ujenzi uzidi kuwa rahisi
Nyumba za NHC zikiwa nyingi mahitaji yatapungua na automatically kodi zitashuka.
 
Dunia nzima investment nzuri ni ya majengo, kwa hali ya kawaida thamani yake huongezeka kila mwaka. Watu wamejibana na kujinyima ili kujenga. Leo hii unataka kodi elekezi? Sio haki! Tusijitoe ufahamu kwa shida zetu. Kama kuna waliopata hayo majengo kwa ufisadi basi serikali itaifishe.
 
Back
Top Bottom