Vijana Chadema kuchaguana Mei

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
Baraza la Vijana wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema (Bavicha) ngazi ya taifa, linatarajia kufanya uchaguzi mwezi ujao.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mbunge wa Ubungo kwa tiketi ya chama hicho, John Mnyika, nafasi zitakazogombewa ni pamoja na Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu, Naibu Katibu Mkuu, Mratibu wa Uhamasishaji, Mweka Hazina, Wawakilishi wa Bavicha kwenye Mkutano Mkuu wa chama na wawakilishi wa Bavicha kwenye Baraza Kuu la chama.
Alitaja umri unaoruhusiwa kugombea kwa mujibu wa Katiba umri wa ujana ni kati ya Miaka 18 na 35.
Alisema mgombea anatakiwa kugombea kwenye umri unaomruhusu kumaliza kipindi chake cha uongozi akiwa bado na umri wa Ujana; hivyo wagombea wenye umri wa zaidi ya miaka 30 hawataruhusiwa kugombea ili kufanya viongozi wa vijana wasiwe zaidi ya miaka 35 katika kipindi chao chote cha utumishi katika Bavicha.
" Wagombea watachukua na Kurudisha Fomu kuanzia tarehe 4 Aprili hadi tarehe 26 Aprili. Fomu zitatolewa kuanzia ngazi ya Mkoa, Makao Makuu ya chama," alisema Mnyika.
Alisema kwa nafasi za Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu, Naibu Katibu Mkuu, Mratibu wa Uhamasishaji na Mwekahazina watalipia shilingi elfu thelathini.
Alisema waliogombea uchaguzi wa awali uliofutwa watajaza na kulipia upya hata kama waliogombea nafasi hizo hizo wanazogombea sasa kwa mujibu wa kanuni za chama.
Alisema mikutano ya Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Wawakilishi wa Bavicha kwenye Baraza Kuu na Mkutano Mkuu watachaguliwa na Mkutano Mkuu wa Bavicha kwa mujibu wa katiba, kanuni na taratibu.
Alisema Katibu Mkuu, Naibu Katibu Mkuu, Mratibu wa Uhamasishaji na Mwekahazina watapendekezwa na Kamati ya Utendaji ya Bavicha na uteuzi wao utathibitishwa na Kamati Kuu ya chama.
kuhusu kampeni, Mnyika alisema kampeni za uchaguzi zitafanywa kwa kuzingatia kanuni za chama, maadili ya uongozi/viongozi pamoja na muongozo juu ya uendeshaji wa uchaguzi ndani ya chama uliopitishwa na Baraza Kuu la Chama unafafanua mambo yanayopaswa kufanywa na yasiyopaswa kufanywa wakati wa kampeni na uchaguzi ndani ya chama kwa lengo la kujenga mshikamano na umoja ndani ya chama na kufanya uchaguzi uwe huru na wa haki.
CHANZO: NIPASHE
 
Back
Top Bottom