singidadodoma
JF-Expert Member
- Nov 11, 2013
- 4,394
- 1,536
VIGOGO zaidi hasa wa Serikali ya Awamu ya Nne walioshiriki katika ufisadi wa aina tofauti na kwa nyakati tofauti, wataendelea kufikishwa mahakamani kujibu mashtaka yanayowakibili, huku Raia Mwema ikithibitishiwa kwamba, vigogo hao ni pamoja na baadhi ya wakuu wa mashirika kadhaa ya umma.
Kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari, katika kuelezea hali halisi ya kitakachofuata ikiwa ni takriban wiki mbili tangu baadhi ya wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kufikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam kujibu tuhuma za rushwa, kimedai kwamba Watanzania wasubiri mshtuko zaidi ya kilichotokea. Ikidaiwa kwamba, si ajabu baadhi ya watumishi waliowahi kufanya kazi Ikulu nao wakajikuta wakifikishwa mahakamani.
Raia Mwema limeelezwa kwamba ndani ya mwezi huu wa Aprili, taifa litashuhudia vigogo mbalimbali maarufu wakifikishwa mahakamani kujibu tuhuma za ufisadi wanaohusishwa nao moja kwa moja wao binafsi au taasisi walizopata kuziongoza.
Wengi miongoni mwao watashtakiwa kwa kosa la “matumizi mabaya ya madaraka.” Vyanzo nyeti vya gazeti hili vimebainisha maeneo makubwa matatu ambayo ‘yatazoa’ vigogo wengi kwenda kortini na miongoni mwa maeneo hayo, sheria mbalimbali zitatumika katika kuwafungulia wahusika mashitaka, lakini kubwa zaidi ni ukiukwaji wa maadili ya viongozi wa umma.
Katika ukiukwaji huo wa maadili ya viongozi wa umma, inaelezwa kwamba ndimo kunakopatikana makosa kadhaa yakiwamo ya matumizi mabaya ya madaraka, kosa ambalo ni maarufu kwa sasa na ambalo tayari limetumika kuwafikisha mahakamani na hata kuwahukumu viongozi kadhaa, wakiwamo mawaziri wa Serikali ya Awamu ya Tatu, Daniel Yona na mwenzake, Basil Mramba.
Mbali na matumizi hayo mabaya ya madaraka, eneo jingine litakalozoa vigogo kadhaa kwenda mahakamani ni matumizi mabaya ya taarifa za serikali; vitendo vya rushwa na mgongano wa maslahi.
Katika rushwa, vitendo vitakavyojumuishwa ni pamoja na kuomba, kupokea, kushawishi na kujipatia maslahi ya kifedha yasiyostahili; kujipatia maslahi ya kiuchumi yasiyostahili; kuingia mkataba na serikali bila kutamka maslahi kwenye mkataba huo.
Miongoni mwa mambo ya dhahiri ambayo ni sawa na kukiuka maadili ya uongozi wa umma, kwa mujibu wa Sekretariati ya Maadili ya Viongozi wa Umma ni pamoja na; “…Kiongozi kutumia cheo, wadhifa na madaraka yake kuweka shinikizo katika kuteua, kuthibitisha, kupandisha cheo mtumishi, kuajiri, kuchukua hatua za kinidhamu, kutumia rasilimali za umma kwa manufaa binafsi na kufanya uamuzi kinyume cha sera, sheria, kanuni na miongozo mbalimbali.
Taarifa zaidi zinabainisha kwamba, katika utawala uliopita, kumekuwa na ukiukwaji mkubwa wa sera, sheria, kanuni na miongozo mbalimbali miongoni mwa viongozi wakuu na kati ya matukio yanayothibitisha hali hiyo ni pamoja na kuibuka kwa tuhuma kuhusu utoaji wa vibali vya uagizaji sukari mwaka jana.
Matumizi mabaya ya taarifa
Kiongozi wa umma hapaswi kisheria kutoa taarifa za serikali za siri au za kawaida ambazo anazitunza au amezipokea kwa kuaminiwa kutokana na madaraka aliyonayo na kujinufaisha binafsi au vinginevyo na taarifa alizozipata wakati wa kutekeleza majukumu ya serikali.
Viongozi wengi wanatajwa kunaswa katika mtego huu na baadhi yao tayari mafaili yao yamejipanga ndani ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).
Inadaiwa kwamba baadhi ya bodi za mashirika ya umma zimekuwa katika uhusiano wa moja kwa moja na baadhi ya wafanyabiashara ili kunufaisha wafanyabiashara hao sambamba na viongozi wanaovujisha taarifa husika kwao na hili linaangukia moja kwa moja katika matumizi mabaya ya taarifa, kinyume cha maadili ya viongozi wa umma.
Taarifa hizi za hivi karibuni kuhusu vigogo wengi zaidi kuburuzwa mahakamani zinaibuka katika wakati ambao tayari viongozi kadhaa, wabunge na hata wasio wabunge, kwa nyakati tofauti wakifikishwa mahakamani kujibu tuhuma mbalimbali zinazowakabili zikiwamo za rushwa.
Awali, haikuwa jambo la kawaida kwa wabunge walioko madarakani tena wa chama tawala – Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuburuzwa mahakamani kwa tuhuma za rushwa lakini kwa sasa, hilo limewezekana na wabunge; Victor Mwambalaswa, Selemani Sadiq, Richard Ndassa na Kangi Lugola wamefikishwa mahakamani kwa tuhuma za rushwa, wakidai kuomba rushwa ya hadi shilingi milioni 30.
Lakini mbali na wabunge hao, Watanzania wameshuhudia tukio jingine la kihistoria baada ya aliyekuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Harry Kitilya na wenzake, akiwamo mkwe wa Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, Sioi Solomon Sumari, wakifikishwa katika Mahakama ya Kisutu, jijini Dar es Salaam.
Kitilya, Sioi na mwenzao, Shose Sinare wamepandishwa kizimbani katika Mahakama hiyo ya Hakimu Mkazi Kisutu wiki iliyopita, wakikabiliwa na mashtaka nane likiwamo la kutakatisha fedha haramu.
Inadiwa kuwa kati ya Agosti 2012 na March 2013 katika Jiji la Dar es Salaam washitakiwa hao wote kwa pamoja walikula njama ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu kutoka katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Wandaiwa kuwa Novemba 5, 2012 katika Benki ya Stanbic makao makuu, Kinondoni jijini Dar es Salaam watuhumiwa hao walitengeneza mkataba wa kughushi kuonyesha kuwa kampuni ya EGMA itaratibu upatikanaji wa mkopo wa dola za Marekani milioni 550 kutoka Standard Bank ya London kwa kushirikiana na Stanbic ya Tanzania na kisha wao wangejilipa asilimia 2.4 ya fedha hizo.
Magufuli azimua mafaili ya Hosea
Taarifa zaidi zinabainisha kwamba, hadi sasa kinachofanyika ndani ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ni kuyafanyia kazi ‘mafaili’ ya viongozi kadhaa ambayo licha ya kazi yake kukamilishwa, hakuna vigogo waliokuwa wamefikishwa mahakamani.
“Jambo jipya kwa upande wa Takukuru hadi sasa ni kuwafikishwa wale wabunge wanne mahakamani, lakini haya mengine yote ni kazi ambayo ilikwishakuwa imefanywa. Ni uzembe tu wa kuidhinisha watu wafikishwe mahakamani ndiyo ulikuwa kikwazo. Lakini sasa, Magufuli ametoa maelekezo na kwa kweli, mmewahi kumsikia akisema katika rushwa…hataangalia mtu usoni,” kilieleza chanzo chetu cha habari.
Kati ya uamuzi ambao Rais John Magufuli ameutekeleza tangu aingie madarakani ni pamoja na kutengua uteuzi wa aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (Takukuru), Dk. Edward Hosea, ambaye naye, hata hivyo, inaelezwa kwamba alikuwa, kwa kiasi fulani, akikwamishwa na mamlaka ya juu zaidi katika kuwafikishwa watuhumiwa kadhaa wa ufisadi mahakamani, ingawa naye pia anatajwa kuwahi kuingia katika kashfa ya kutoa taarifa ya kuisaifisha iliyokuwa kampuni tata ya kufua umeme ya Richmond, mwaka 2007.
Magufuli alitengua uteuzi huo wa Dk Hosea kutokana na kutoridhishwa na namna taasisi hiyo ilivyokuwa ikitekeleza wajibu wake katika kukabiliana na rushwa, hususan kwenye upotevu wa mapato ya serikali katika Bandari ya Dar es Salaam.
Kutokana na uamuzi wake huo, Rais Magufuli alimteua aliyekuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Valentino Mlowola kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru.
Chanzo: Rai Mwema