Vigogo CCM wahojiwa TAKUKURU

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,903
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) imeanzisha uchunguzi wa kashfa ya uuzaji wa gari la Jumuiya ya Wazazi ya CCM Mkoa Kilimanjaro baada ya mauzo kudaiwa kugubikwa na utata.

Kamanda wa Takukuru Mkoa Kilimanjaro, Alex Kuhanda alisema jana kuwa wanaendelea na uchunguzi wa suala hilo.

“Ni kweli kabisa hilo suala tunalo na uchunguzi unaendelea lakini ukiniuliza nini hasa tunachunguza, hilo utanisamehe kwa vile sheria hainiruhusu kutoa taarifa za uchunguzi unaoendelea,” alisema Kuhanda.

Habari zilizolifikia gazeti hili zilisema tayari vigogo watatu wa jumuiya hiyo wameitwa na kuhojiwa.

Vyanzo vya habari vilidai kuwa gari hilo aina ya Toyota Hiace lilinunuliwa kwa thamani ya Sh19 milioni na baadaye kuuzwa kwa Sh10 milioni, lakini fedha zilizoingia kwenye akaunti ya jumuiya hiyo ni Sh7 milioni tu.

Katibu mpya wa jumuiya hiyo, Khatibu Mnuwa alikiri kulikuta jambo hilo mezani na kuomba apewe muda ili aweze kukutana na mwenyekiti wake kujua kilichotokea.

Mnuwa alidai kuwa hajafurahishwa na hatua ya Takukuru kuwaita na kuwahoji wafanyakazi walio chini yake bila kumshirikisha ilhali wanawajibika kwake.

Alisema mwenyekiti wake yuko visiwani Zanzibar katika uchaguzi wa marudio unaotarajiwa kufanyika Machi 20.

Akijibu madai ya katibu huyo ya wafanyakazi wake kuitwa Takukuru bila kushirikishwa, Kuhanda alisema taasisi yake ni ya uchunguzi wa jinai hivyo inayo mamlaka ya kumuita yeyote na wakati wowote kwa ajili ya kuhojiwa.

Chanzo cha habari kilidai kuwa mmoja wa viongozi wa jumuiya hiyo, juzi aliitwa Takukuru na kuhojiwa kwa saa tatu kuhusiana na uuzaji huo unaodaiwa haukupata idhini ya Baraza la Wadhamini wa CCM kwa mujibu wa Katiba.

Kifungu cha 130(5) cha Katiba ya CCM ya mwaka 1977 kinasema mali yoyote inayoondosheka na isiyoondosheka itakuwa mikononi mwa Baraza la Wadhamini lenye mamlaka ya kusaini mikataba ya mali za CCM.


Chanzo: Mwananchi
 
Aisee hao vigogo ni wangapi wanao husika na na uuzaji wa hiace ya milion 19 sijui ,nilijua vigogo wa ccm wanao husika na madawa ya kulevya ama ujangili wa tembo
 
kwa kuwa ni viongozi wa ccm hapo hakuna suala la majipu, hapo ni sawa na kujitoboa jicho mwenyewe lazima itashindikana
 
Aisee hao vigogo ni wangapi wanao husika na na uuzaji wa hiace ya milion 19 sijui ,nilijua vigogo wa ccm wanao husika na madawa ya kulevya ama ujangili wa tembo
Ufisadi ni kama dhambi hakuna dhambi ndogo wala kubwa zote ni dhambi tu
 
Hakuna kigogo anaye hangaika na ishu ya milioni 19 ,hao ni vibaka tu na wataisoma namba,vigogo njoo Epa,Escorow,Richmond, mabilioni ya uswisi,vitalu vya wanyama,mamlaka ya ngorongoro ,miradi ya halmashauri nk
Ccm ni kama nzi akiona kinyesi akiachi bilakukilamba kwa hiyo usidhani wanaacha hela yoyote
 
mkiambiwa msipende kula nyama za miguu ya kuku hamsikii!!! ona sasa ulivyomtembezi!!! duuh kutoka ufipa hadi lumumba kisa umbea!!? utavishwa kanga shauri yako
 
Magufuli aliwahi kesema "mtu unamkamata ledi handed halafu unafanya uchunguzi, uchunguzi wa nini wakati umemkamata LEDI HANDED? Peleka mahakamani akafungwe" Hayo ndio yalikua maneno yake sasa hawa wanao fanya uchunguzi usio isha ndio wanamuangusha magu.
 
Ccm sawa na mtu mchafu anayevunja kioo kisa kimemuonyesha uchafu badala ya kuwashukuru wapinzani wanaanza kugombana nao
 
Back
Top Bottom