Vigogo AUWSA na Mkurugenzi wa Kiure engineering wapanda Tena Kortini

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
749
1,797
Kesi inayowakabili watu saba wakiwemo vigogo sita wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Jiji la Arusha{AUWSA} jana ilishindwa kuendelea kwa watuhumiwa hao kusomewa maelezo ya awali{Ph} kwa tuhuma mbalimbali zinazowakabili ikiwemo kujipatia fedha kiasi cha shilingi bilioni 5.3 kinyume na sheria baada ya taratibu za usomaji maelezo hayo kutokamilika.

Kesi hiyo iliyofunguliwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Arusha kwa watuhumiwa hao huku akiwemo aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka hiyo Mhandisi Ruth Koya Kwa kosa la matumizi mabaya ya madaraka, kula njama na kujipatia manufaa ya Kiasi cha shilinhi bilioni 5.3 kinyume Cha sheria.

Mbali na washtakiwa hao , pia Mkurugenzi wa Kampuni ya Kiure Engineering ltd ya Jijini Arusha,Omari Kiure Mkazi wa Jijini Arusha naye ni miongoni mwa washitakiwa hao waliofikishwa Mahakamani.

Vigogo wengine waliopanda kizimbani ni Benedict Kitigwa,James Mwambona,Steven Msenga , Godfrey Macha na Juma Mkwawa wote wakiwa wafanyakazi wa AUWSA.

Mwendesha Mashitaka wa Takukuru,Violet Machali jana alisema mbele ya Hakimu wa Wilaya ya Arumeru,Harieth Mtenga kuwa taratibu za usomaji wa maelezo ya watuhumiwa hao bado hazijakamilika hivyo aliomba tarehe nyingine ya kutajwa kwa kesi hiyo.

Baada ya maelezo hayo Hakimu Mtenga alihairisha kesi hiyo hadi octoba 13 mwaka huu kwa watuhumiwa hao kusomewa maelezo ya awali na watuhumiwa wote wataendelea kuwa nje kwa dhamana.

Awali alidaiwa Mahakamani hapo kuwa watuhumiwa hao Kwa pamoja walitenda makosa manne ya uhujumu uchumi na kujipatia fedha kiasi cha shilingi bilioni 5.3

Alidai kosa la kwanza linawahusu washtakiwa wote Kwa pamoja ambapo Kati ya Desemba ,2017 na Oktoba mwaka 2018 Katika eneo la Jiji la Arusha washtakiwa hao walikula njama kupitia Mradi wa Maji wa Kanda na kuipatia manufaa isiyostahili kampuni ya ujenzi ya Kiure Engineering ltd ya Jijjni hapa bila kufuata taratibu za manunuzi.

Alidai kosa la pili ni matumizi mabaya ya madaraka ambalo linalomhusu Mshtakiwa wa kwanza Mhandisi Ruth Koya ambaye inadaiwa akiwa mtumishi wa Umma na akijua kwamba ni kosa kisheria aliwezesha kampuni ya Kiure engineering LTD kupata mkataba wa ujenzi wa ofisi za Kanda za AUWSA kitendo kilichopelekea kampuni hiyo kupata manufaa ya sh, bilioni 5.3 kinyume cha sheria ya manunuzi ya mwaka 2011kifungu Cha 36(5).

Alidai shitaka la tatu na la nne linawahusu Mshtakiwa wa 1,2,3,4 na 5 ambao ni Ruth Koya, Benedict Kitigwa ,James Mwambona ,Steven Msenga na Godfrey Macha ambalo Kati ya mwezi Desemba 2017 na Oktoba 2018 wote Kwa pamoja walitumia vibaya madaraka.yao na kupelekwa kampuni ya Kiure engineering ltd kupata manufaa ya shbilion 5.3.

Watuhumiwa wote walikana mashitaka hayo na wako nje kwa dhamana kwa baada ya kudhaminiwa na wadhamini wawili akiwemo mtumishi wa umma mwenye kitambulisho na barua ya utambuzi kutoka kwa mwajiri wake,na Mdhamini atasaidi Bondi ya mali isiyohamishika yenye thamani ya shilingi milioni 20 na washitakiwa hao kwa pamoja wanatetewa na wakili Robert Rogati na Mnyiwala Mapembe.

IMG_20210831_143311_816.jpg
 
Back
Top Bottom