MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 13,171
- 23,991
Baada ya zoezi la kupiga kura kumalizika Zanzibar, hakuna ubishi kuwa Ali Mohamed Shein ataendelea kuwa Rais wa Zanzibar.
Sitaki kuingia kwenye hoja ya uhalali wa zoezi la kupiga kura na matokeo ya kura. It’s a bygone conclusion.
Hoja iliyopo kwa sasa ni namna ambayo itamwingiza Hamad Rashid kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar. Pamoja na kwamba ni foregone conclusion lakini siyo vibaya kama tutaangalia matakwa ya kikatiba.
Kikwazo cha kikatiba kinachomsubiri Hamad Rashid kipo katika sehemu ya pili ya Katiba ya Zanzibar 1984, Ibara ya 39(1-3) ambacho kinasema;
Je, kura zisipotosha, zitatosheshwa? Zitatosheshwa kwa njia gani?
Je, ina maana huu ni mwanzo wa kifo cha Serikali ya Umoja wa kitaifa?
Ninasema hivyo kwa sababu Ibara ya 40 ya Katiba inampa Rais wa Zanzibar Madaraka ya kuteua mtu yoyote kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais kama vigezo vya ibara ya 39 havitakidhi.
Ibara ya 40(1) inasema;

Hoja ya msingi, itakuwaje kama kura hazitatosha?39.(1) Kutakuwa na Makamo Wawili wa Rais ambao watajuilikana kama Makamo wa Kwanza wa Rais na Makamo wa Pili wa Rais.
(2) Ndani ya siku saba mara baada ya kushika madaraka, Rais atateua Makamo wa Kwanza wa Rais na Makamo wa Pili wa Rais.
(3) Makamo wa Kwanza wa Rais atatakiwa awe na sifa za kumuwezesha kuchaguliwa kuwa Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi na atateuliwa na Rais baada ya kushauriana na chama kilichotokea nafasi ya pili katika matokeo ya kura ya Uchaguzi wa Rais.
Isipokuwa kwamba:-
(i) iwapo chama kilichotokea nafasi ya pili katika matokeo ya kura ya Uchaguzi wa Rais kimepata chini ya asilimia kumi (10%) ya kura zote za Uchaguzi wa Rais, au
(ii) endapo Rais atakuwa hana mpinzani, basi nafasi ya Makamo wa Kwanza wa Rais itapewa chama chochote cha upinzani kilichotokea cha pili kwa wingi wa viti vya Majimbo katika Baraza la Wawakilishi.
Je, kura zisipotosha, zitatosheshwa? Zitatosheshwa kwa njia gani?
Je, ina maana huu ni mwanzo wa kifo cha Serikali ya Umoja wa kitaifa?
Ninasema hivyo kwa sababu Ibara ya 40 ya Katiba inampa Rais wa Zanzibar Madaraka ya kuteua mtu yoyote kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais kama vigezo vya ibara ya 39 havitakidhi.
Ibara ya 40(1) inasema;
40.(1) Endapo nafasi ya Makamo wa Kwanza wa Rais au Makamo wa Pili wa Rais itakuwa wazi:
(a) kwa sababu ya kufariki au kujiuzulu; au
(b) ikiwa Rais amefuta uteuzi huo; au
(c) kwa sababu nyengine yoyote itakayomfanya ashindwe kuwa na sifa za Makamo wa Kwanza wa Rais au Makamo wa Pili wa Rais;
Rais atamteua Makamo wa Kwanza wa Rais au Makamo wa Pili wa Rais kutegemeana na nafasi iliyo wazi.