kalulukalunde
JF-Expert Member
- May 27, 2016
- 1,056
- 1,083
“WALIOZOEA elimu ya mkato wasahau hilo sasa kwa sababu nimepewa jukumu la kuhakikisha elimu ya Tanzania inakuwa bora zaidi na yenye kuleta manufaa. Ni lazima utaratibu ufuatwe,”ni kauli ya Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako.
Anasema, Watanzania wanapaswa kufaidi matunda ya usomi wao na kwamba, hilo litawezekana endapo wataipata elimu bora katika kila ngazi, kuanzia shule ya msingi, sekondari na vyuoni.
Kwa mujibu wa Profesa Ndalichako, ili kufika hapo ni lazima yafanyike mabadiliko kwa ushirikiano na wananchi. “Mabadiliko katika sekta ya elimu yanataka ushirikiano wa kutosha kati ya Waziri wa Elimu, wizara anayoisimamia na wananchi.
Vinginevyo kuyapata ni vigumu,”anasema. Anasema, anafahamu kwa hali ya kawaida na kwa asili binadamu hapendi mabadiliko, hivyo unahitaji kufanya ayakubali, ayapokee na kuyazoea. Kwa mujibu wa Profesa Ndalichako, ili elimu ya Tanzania iwe na tija ni lazima afanye mabadiliko ili kuhakikisha kuwa kila kitu katika sekta hiyo kinakwenda sawa na wananchi wanafaidika.
Anabainisha kuwa, katika sekta ya elimu, Tanzania ilikuwa imefika mahali kila mtu alikuwa akijifanyia mambo yake bila kuzingatia utaratibu. Anawatuhumu waliopewa dhamana ya kuisimamia sekta hiyo kuwa walifanya kazi kiholela na kuruhusu njia za mkato.
Anasema, wanafunzi, walimu, wadau wa elimu na wasimamizi wa sekta hiyo nao wamekuwa wakitafuta njia za mkato kufanikisha masuala yao na matokeo yake wamesababisha elimu iwe holela.
“Kwa sababu hali hiyo ililetwa na mifumo pia katika sekta ya elimu, kuibadili kunahitaji nipewe ushirikiano na kila mmoja ili, pamoja na kuhakikisha ubora wa elimu kwa ngazi zote, niondoe mambo ya mkato mkato,” anasema Profesa Ndalichako. Anawaomba Watanzania wamuelewe na kufahamu kuwa, hana nia mbaya na wala hajapanga kumwonea au kumpendelea mtu kwa kubadilisha mifumo iliyopo.
Kwa kuzingatia maelezo ya Waziri Ndalichako, nia ya mabadiliko katika mifumo ya sekta ya elimu ni njema ya kuleta mifumo mizuri na thabiti itakayochochea mabadiliko chanya katika sekta ya elimu nchini ili vijana na Watanzania wote waone matunda ya kuelimika kwao. Anasema, anataka elimu ya Tanzania isimame katika ubora wake, kwa sababu sasa kuna malalamiko kuhusu sekta hiyo.
“Ninataka vijana wawe na mchango katika taifa na watu wafurahie matunda ya elimu wanayoipata na si kulalamika,”anasema Profesa Ndalichako. Soko la pamoja la EAC Professa Ndalichako anasema, kwa sababu tuko katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na kwa kuwa linaanzishwa soko la pamoja la jumuiya hiyo, ni lazima vijana wa Tanzania wajengewe mazingira wapate elimu bora ili wanufaike na soko hilo hasa la ajira na uchumi kwa ujumla.
EAC ina nchi sita wanachama ikiwemo Tanzania, Rwanda, Burundi, Kenya, Uganda na Sudan Kusini. Profesa Ndalichako anasema, kwa kuwa yeye ni Waziri wa Elimu, anawajibika kuhakikisha anafahamu Tanzania itasimama wapi katika soko la EAC kwa kuweka mazingira ya elimu bora, itakayowawezesha hasa vijana kunufaika na fursa zinazopatikana huko.
“Sitaki Watanzania wawe wasindikizaji tu katika soko hilo la Jumuiya ya Afrika Mashariki ndio maana naomba ushirikiano wao katika kuibadili mifumo iliyopo. Ninawaahidi kuwa dereva mwaminifu kuliendesha hili gari vizuri lifike linakotakiwa kwa usalama,” anasema.
Anawaomba Watanzania wawe abiria wema na wenye nia ya dhati kutaka sekta ya elimu ifikie mafanikio yanayokusudiwa na wala si kuanza kulitoa gari hilo upepo kwa sababu kufanya hivyo kutalifanya likwame kabla ya kumaliza safari.
Lugha ya kufundishia Kuhusu lugha ya kufundishia, Waziri Ndalichako anasema, ingawa Kiswahili ni lugha ya taifa la Tanzania, Kiingereza kinaendelea kutumika ili kuwawezesha Watanzania kushindana kwenye soko la ajira ndani na nje ya nchi. Anasema, kumekuwa na mitazamo tofauti miongoni mwa Watanzania na hasa wadau wa elimu kwa kuwa wengine wanataka itumike lugha ya taifa kufundishia kuanzia shule za awali hadi vyuo vikuu na wengine wanataka kitumike Kiingereza.
“Suala la lugha linatugawa Watanzania kwa kweli. Sisi wizara tumekuwa tukipeleka maoni ya Watanzania kwenye mijadala ya lugha ipi itumike kufundishia lakini mara zote tunapowafikia wataalamu inakuwa ni vigumu kufikia maoni mwafaka,” anasema Profesa Ndalichako.
Anasema, kwa sasa suala hilo limeachwa wazi kuruhusu mijadala iendelee kwa sababu, wakati wengine wakitaka Kiswahili, wengi wanatoa maoni kuonesha wanahitaji Kiingereza kitumike kuwawezesha wananchi kuwasiliana katika kipindi hiki ambacho dunia imekuwa kama kijiji kwa sababu ya utandawazi.
Chanzo: Habari leo