Vigeugeu vya wanasiasa

Jul 29, 2015
47
14
Mimi itikadi yangu ni CHADEMA, nimeokoka na ninampenda MUNGU.

Napenda kuwasisitizia sana ndugu zangu wana JamiiForums, biblia inasema hakuna mamlaka isiyowekwa na Mungu. Kwa jinsi ninavyojua na uhakika nilionao mimi, Tanzania kwa sasa inaongozwa na Mungu mwenyewe aliyeziumba Mbingu na nchi.

Wanasiasa kwa asili ni waongo, ni watu wenye kutafuta masilahi yao, huwa na fitina wao kwa wao na wanapo ona kuna maslahi yao huungana na kusahau tofauti zao mfano William Ruto na Kenyatta huko nchini Kenya.

CHADEMA kukubaliana na Lowassa mwaka huu kwa lengo la kushika dola japo walimwita fisadi, na Dr. Kaburou au Saidi Arfi kurudi CCM baada ya kupoteza mwelekeo CDM.

Jaman,i tutumieni akili za kawaida, hivi Lowassa au Sumaye angepitishwa na NEC kugombea urais wangehama CCM? Wasingekuwa wanaishambulia CHADEMA sasa?

Na UKAWA wangekuwa wamewachafua kiasi gani mpaka sasa?

Na Lowassa angechaguliwa NEC, Kingunge angehama CCM au kuishambulia?

Pia, Dr. Slaa angepewa kugombea urais UKAWA angejiuzulu siasa na kuitukana CHADEMA?

Wananchi tumieni akili na mwongozo wa Mungu kumchagua rais, na pia muwe tayari kupokea matokeo kwa kuwa huyu rais anayekuja amechaguliwa na Mungu.
 
Ndugu zangu,Tafiti za Twawezwa na Ipsos zisitutoe katika "Mstari" wa kutafakari "AHADI" za CCM za mwaka 2010 na Zile mpya za John Magufuli kama zisizotekelezeka.Ukitaka kujua kama Magufuli atatekeleza ahadi zake ANGALIA kama CCM ya Kikwete ilitekeleza walichowaahidi WATANZANIA wanaowaita "Wapumbavu, Malofa, Mbumbumbu na Kunguni kwa kuwa tu wepesi KUSAHAU!!!

Kwa kuwa ninyi mpo sehemu mbalimbali TANZANIA thibitisha kama ahadi hiyo imetekelezwa ama kuna ahadi aliahidi sijaiweka hapa na HAIJATEKELEZWA!!!!

1. Kujenga reli mpya kutoka Dar es Salaam mpaka mikoa ya Kanda ya ziwa-Nzega, Tabora (HAJATEKELEZA)
2. Mkoa wa Tanga kuwa Jiji la Viwanda- Tanga mjini (HAJATEKELEZA)
3. Tabora kutumia maji ya Ziwa Victoria- Igunga (HAJATEKELEZA)
4. Kulipa madeni ya chama cha Ushirika mkoa wa Shinyanga (SHIRECU)- Shinyanga (
HAJATEKELEZA)
5. Kumaliza migogoro ya Ardhi nchini- Dodoma
(HAJATEKELEZA)
6. Wakulima kuacha kutumia jembe la mkono-Dodoma mjini
(HAJATEKELEZA)
7. Kuwapatia trekta wakulima -Kata ya Mrijo, Dodoma (HAJATEKELEZA)
8. Wananchi kutoondolewa kwenye Ranchi ya Misenyi-Kagera (HAJATEKELEZA)
9. Kujenga Uwanja wa Ndege Misenyi- Kagera (HAJATEKELEZA)
10. Kupanua Uwanja wa Ndege Bukoba- Bukoba Mjini (HAJATEKELEZA)
11. Kujenga uwanja wa ndege mkubwa Kigoma - Kigoma Mjini (HAJATEKELEZA)
12. Mtukula kupatiwa umeme kutoka Uganda- Kagera
(HAJATEKELEZA)
13. Mikoa ya Kagera, Kigoma, Lindi, Rukwa na Ruvuma kuunganishwa katika gridi ya taifa ya umeme- Kagera
(HAJATEKELEZA)
14. Kuimarisha Takukuru kwa miaka mitatu- Kagera
(HAINA MENO KABISA NA IMEJAA RUSHWA)
15. Hukumu kwa waliopatikana na hati ya kuua albino- Mbeya (MAUAJI YANAENDELEA)
16. Kununua meli kubwa kuliko MV Bukoba- Kagera (HAJATEKELEZA NA ZILIZOPO MBOVU HAZIFAI)
17. Kuanzisha benki ndogondogo kwa ajili ya wajasiriamali (HAJATEKELEZA)
18. Serikali kuvisaidia vyama vya ushirika- Mwanza (HAJATEKELEZA NAVYAMA VILIVYOPO VINA HALI MBAYA NA VINGI VIMEKUFA KABISA)
19. Kuimarisha usalama Ziwa Victoria na Ziwa Tanganyika kwa kupeleka kikosi maalum chenye vifaa kupambana na wahalifu-Mwanza
(HAJATEKELEZA)
20. Wilaya ya Geita kuwa hadhi ya mkoa Januari mwakani- Geita (
21. Kulinda muungano kwa nguvu zote- Pemba
(KERO HAZIJATATULIWA)
22. Kuwajengea nyumba waathirika wa mafuriko Kilosa-Morogoro
(HAJATEKELEZA)
23. Kununua meli mpya kubwa Ziwa Nyasa- Mbeya mjini
(HAJATEKELEZA)
24. Kujenga bandari Kasanga –Rukwa (HAJATEKELEZA)
25. Kumaliza tatizo la walimu miaka mitano ijayo - Songea (HAJATEKELEZA NA WALIMU WAMEPUUZWA WANAULIZA -SHEMEJI UNATUACHAJE?)
26. Kufufua mgodi wa makaa ya mawe Kiwira -Mbeya (HAJATEKELEZA)
27. Kuzuia hatari ya kisiwa cha Pangani kuzama- Tanga
(HAJATEKELEZA)
28. Kununua bajaji 400 kwa ajili ya kubeba wajawazito hasa vijijini- Iringa
(HAJATEKELEZA)
29. Kujenga barabara yenye kiwango cha lami kutoka Same mpaka Kisiwani –Kihurio na kuiunganisha na barabara kuu ya Moshi - Dar es salaam- Same mkoani Kilimanjaro
(HAJATEKELEZA)
30. Kumaliza tatizo la maji katika wilaya ya Same-Same Mjini
(HAJATEKELEZA)
31. Kuboresha barabara za Igunga -
Tabora (HAJATEKELEZA)
32. Kusambaza walimu 16,000 katika shule za sekondari zenye upungufu makubwa wa walimu- Kisesa Magu (AMETEKELEZA)
33. Kununua vyandarua viwili kwa kila kaya- Mbeya Mjini (HAJATEKELEZA)
34. Kuzipandisha hadhi hospitali maalumu saba nchini kuwa za rufaa ili kuipunguzia mzigo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MHN)- Hydom Manyara (HAJATEKELEZA)
35. Kulinda amani nchini kwa kuzuia chokochoko za kidini, kikabila na kisiasa-Musoma (HAJATEKELEZA CCM NDIO CHANZO CHA CHOKOCHOKO)
36. Kulinda haki za walemavu- Makete (HAJATEKELEZA,WANATUMIKA KWENYE KAMPENI TU)
37. Kujenga baabara ya Njombe- Makete kwa kiwango cha lami,urefu wa kilomita 109- Iringa mjini (HAJATEKELEZA)
38. Kujenga barabara Musoma–Mto wa Mbu Arusha-Arusha (HAJATEKELEZA)
39. Kuanzisha jimbo la Ulyankulu- Shinyanga Mjini (HAJATEKELEZA)
40. Kujenga barabara ya lami Manyoni- Kigoma– Kaliua,Tabora (HAJATEKELEZA)
41. Kukarabati barabara ya Arusha Moshi- Arusha Mjini
(ANGALAU JAPO KIWANGO HAKIRIDHISHI)
42. Kuboresha barabara ya Handeni, Kondoa,mpaka Singida-Dodoma
(HAJATEKELEZA)
43. Kuwafidia wanakijiji ng'ombe waliopotea wakati wa ukame mwaka 2009- Longido
(HAJATEKELEZA)
44.Vijiji vyote vilivyoko kilomita 15 kutoka kwenye bomba kuu la mradi mkuu wa maji wa Ziwa Victoria-Shinyanga-Kahama kuunganishiwa maji - Shinyanga
(HAJATEKELEZA)
45. Tatizo la umeme kufikia kikomo Novemba mwaka huu 2010 mkoani Arusha – Arusha mjini
(HAJATEKELEZA NCHI IPO GIZANI KWA MGAO AMBAO HAUJATANGAZWA)
46. Kukopesha wavuvi zana za kilimo- Busekera, Wilaya ya Musoma, .
(HAJATEKELEZA)
47. Kuwapatia maji wakazi wa Wilaya ya Longido- Longido (HAJATEKELEZA)
48. Kujenga barabara ya lami kupitia pembezoni mwa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti – Ngorongoro (HAJATEKELEZA)
49. Utekelezaji wa mpango wa maendeleo ya kilimo kuwasaidia wafugaji kuweza kupata na kutunza mifugo yao vizuri- Mbulu mkoani Manyara
(HAJATEKELEZA)
50. Kusambaza maji nchi nzima-Babati vijijini (HAJATEKELEZA)
51. Kusambaza umeme, utoaji wa huduma za afya, na uboreshaji wa kilimo cha umwagiliaji na utoaji ruzuku kwa wakulima. mwaka 2010-2015-Babati vijijini Kuongeza mara tatu idadi ya wananchi wanaonufaika na ruzuku ya pembejeo za kilimo kwa mfumo wa vocha.-Iringa
(HAJATEKELEZA NA HALI NI MBAYA SANA)
52. Kuhakikisha Isimani inapata maji ya uhakika- Iringa
53. Kuiwekea lami barabara inayokwenda katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, ambayo ndiyo hifadhi kubwa kuliko zote Tanzania- Iringa
(HAJATEKELEZA)
54. Kulinda usalama wa wananchi kwa ujumla ili kudumisha amani na sifa ya nchi-Ifunda (HAJATEKELEZA - CHOKOCHOKO ZA CCM ZINAHATARISHA AMANI)
55. kutokomeza malaria 2015-Bunda,mkoa wa Mara (HAJATEKELEZA)
56. Kuwapa wanawake nafasi zaidi- Kilolo ,Iringa (ANGALAU)
57. Ahadi kuisadia Zanzibar kuendeleza miradi mbalimbali ya kijamii-Kibandamaiti Mjini Zanzibar
(HAJATEKELEZA)
58. Kuipandisha hadhi hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar kuwa ya rufaa- Kabandamaiti mjini Zanzibar (HAJATEKELEZA)
59. Kuisaidia Zanzibar kila panapohitajika msaada-Kibandamaiti (HAJATEKELEZA)
60. Serikali kujenga upya bandari ya Mbambabay-Ruvuma
(HAJATEKELEZA)
61. Ununuzi wa Meli mpya yenye uwezo wa kubeba tani 400-Mbambabay Ruvuma
(HAJATEKELEZA)
62. kufufua chama kikuu cha ushirika cha wakulima wa Mbinga(MBICU) –Ruvuma
(HAJATEKELEZA)
61. Ahadi Rais wa Marekani Barack Obama kuimwagia misaada Tanzania –Ruvuma
(MISAADA YA VYANDARUA NA VYOO KWA MSAADA WA WATU WA MAREKANI)
62. Ahadi hakutakuwa na umwagaji wa damu baada ya uchaguzi-Dar es Salaam (HAJATEKELEZA)
63. Mtwara kuwa mji wa Viwanda –Mtwara (HAJATEKELEZA)
64. Ahadi ujenzi wa kwanda cha dawa ya kuua viluilui vya mbu-Kibaha
(HAJATEKELEZA)
65. Hospitali ya Tumbi kuwa ya mkoa- Kibaha. (HAJATEKELEZA)
66.Halmashauri ya manispaa ya Kibaha kutenga eneo maalumu la viwanda -
Kibaha (HAJATEKELEZA) N.K

CCM HAIAMINIKI TENA, WAKATI UMEFIKA CCM INAPASWA ITOLEWE KWA NJIA YA KURA MADARAKANI?..KWA NINI WASITEKELEZE AHADI HIZI KABLA YA KUAHIDI ZINGINE?.
...CHAGUA LOWASSA..CHAGUA UKAWA (CHADEMA/CUF/NLD/NCCR MAGEUZI)
 
Kazi yako na nafasi yako kama wakili wa Mungu hapa Tanzania ulitakiwa kuwa kwenye maombi kuliombea taifa na sio kutupa madongo kwa viongozi hawa awe Magufuli au Lowassa! halafu nani kakuweka kuwa mwamuzi juu yao?

Mungu atawatumia watanzania hawahawa unaowaona kuchagua kiongozi maana yeye ni MUNGU PAMOJA na wanadamu sasa ukianza na wewe kupiga ramli na kumulika ya wenzako tena ukionyesha upande wako wazi wazi HUJAOKOKA nenda kwa mchungaji wako akakuongoze sala ya toba!
 
Hujui siasa wewe.

Siasa haina rafiki wala adui.

Siasa sio ndoa ambayo unaishi kwa shida na raha.

Siasa ni kuangalia wapi patakupeleka sehemu unayotaka.

Mwanasiasa lazima atumie fursa iliyo mbele yake.
 
Hapa nimeongelea wanasiasa pande zote, tatizo la chadema ndugu zangu tumeshajazwa chuki, hatuna subira ni wepesi wa kutukana. Na hili bila shaka laweza kutu cost kupata baraka za mwenyezi Mungu kushika dola. Bahati nzuri zimebaki siku kumi mpaka matokeo.

Sijui ndugu zangu CDM tutajifichia wapi matokeo yasipo kuwa kama tunavyotaka. Tukana kama unavyotaka, kuokoka si ujinga tena ni heshima mbele za Mungu. Ni swala la muda tu ila matokeo yatashangaza wengi kuwa kinyume na matarajio yao.
 
Back
Top Bottom