Vifurushi vya Internet

Vifurushi vya Internet

Arnomos

Member
Joined
Jun 5, 2015
Posts
30
Reaction score
25
Hivi jamani, pengine mi ndo ambaye sielewi labda ama vipi nitaomba mnieleweshe. Hivi kwanini siku hizi vifurushi vya Internet vinapanda bei sana? Yaani kwa sasa hivi kifurushi cha bei ya chini kabisa cha Internet kwa mitandao karibu yote ni shillingi 3,000 ambapo hapo unapata MB 700 kwa Zantel na Voda unapata Mb 500 vyote hivyo ni vya wiki. GB 1 kwa wiki sasa hivi inauzwa kuanzia shillingi 5,000 kwenda juu, na siku hizi ukinunua Kifurushi chochote cha kawaida tu unapewa either Mb 1 hadi 10 kwa mitandao tofauti hata kama ungenunua cha Mwezi ujazo wa data unakuwa unafanana wakati zamani kwa shillingi 500 tulikuwa tukijiunga na Extreme tunapewa dakika, sms na data mb 100, lakini siku hizi sijui hata nini kimetokea. Nikitafuta sababu mtandaoni ni kwanini sipati majibu ya moja kwa moja, nakutakana na nukuu (quotes) chache tu zinazodai kuwa kodi wanazotozwa ndizo zinazofanya wapandishe bei na wao, sasa hii serikali ya Tanzania itaacha lini ku survive kwa kupitia kodi tu, kwanini yenyewe kama entity isianzishe miradi yake kama biashara hivi then ikawa inajipatia faida huko kuliko kuishi kwa kodi tu, mfano huu UDART (Mwendokasi) si mradi wao, sasa kwanini wasianzishe project zao wenyewe zitakazo waingizia hela tofauti na kodi, maana kwa style hii ni kumuumiza Mtanzania ambaye gharama zote hizo zinamrudia yeye. Ofcourse kodi zitozwe lakini zisiwe excessive kiasi hiki jamani, hebu imagine kutokea 3,000 hadi 5,000 kwa GB 1 jamani hivi ni kweli kabisa. Na vishindo hivi vyote hutokea baada ya bunge la budget yaani lenyewe halijuagi kuacha kodi zilizopo, linachojua ni kupandisha kodi kila mwaka wa fedha, na hizi bei za sasa hivi kwa mwaka mwingine wa fedha wataongeza kodi tena, sasa hebu niambie hiyo ni nini. Hivi wanajua kuwa kodi nyingi nazo zina madhara yake, thamani ya fedha inashuka, kama ningeweza kupata kitu fulani kwa 10,000 basi nitahitaji 15,000 ili kuweza ku afford kitu ambacho hapo mwanzo ningeweza kukipata kwa 10,000. Jamani serikali, jitahidini mpate project za kuwaingia pesa kama wafanya biashara wanavyofanya biashara na kupata faida basi nyie pia fanyeni hivyo kwa maana hayo sio maisha bora kwa kila mtanzania, yaani hapa nawaza huo mwaka mwingine wa fedha sijui kama hatujanuna GB 1 kwa 10,000 bundle ya wiki tu.
 
Tafuta vocha za airtel za 1500 zinakuja na jb 1 dakika 145 za airtel na dakika 5 mitandao yote kwa wiki sinunui vocha zq jero jero sasahivi
Sipendi ujinga ujinga mimi
 
Natumia halotel Tshs 500 napata 600MB nilikuwa natumia Tigo Tshs 1000 nilipata 350MB
 
Tatizo siyo kodi mkuu, hizo ni cheche tu. Tanzania ni miongoni mwa nchi chache za mwisho mwisho kwa kutoza gharama kidogo za Data, expect more for the coming days.
Pili, haya makampuni ya simu yamefikia wakat sasa kwamba there is no new subscriber's, wateja ni wale wale , number of subscribers haiendi juu.. hao hao waliopo ndo wanagawana.. kwa hyo maana yake revenue haiongezeki... na unakuta bado hawajapata profit...so wht to do ndo unacholalamika ambapo bado bei haijapanda kisawa sawa... kodi siyo tatizo maana kampuni kama haipat faida..haitozwi kodi..na V.A.T hailipi kampun..analipa mtumiaji wa mwisho.
 
Nenda tigo shop waambie wakuuzie line mpya na wakuunganishe na huduma ya University offer/extreme. Kwa line mpya siku ya kwanza ni 3000 ila baada ya hapo utajiunga mwenyewe popote kwa 1500 dk 130 na 1GB kwa wiki. 300 MB 300 na dk za kutosha /500 MB 500 kwa siku.
500 kwa wiki MB 500
 
Eeeeh!! Mi nikajua vifurushi vya chuo ni mpaka mtu uwe eneo la chuo kumbe kuna na option ya line. Lakini si wanaweza kunitengenezea line yenye namba hii hii niliyo nayo?
 
Tatizo siyo kodi mkuu, hizo ni cheche tu. Tanzania ni miongoni mwa nchi chache za mwisho mwisho kwa kutoza gharama kidogo za Data, expect more for the coming days.
Pili, haya makampuni ya simu yamefikia wakat sasa kwamba there is no new subscriber's, wateja ni wale wale , number of subscribers haiendi juu.. hao hao waliopo ndo wanagawana.. kwa hyo maana yake revenue haiongezeki... na unakuta bado hawajapata profit...so wht to do ndo unacholalamika ambapo bado bei haijapanda kisawa sawa... kodi siyo tatizo maana kampuni kama haipat faida..haitozwi kodi..na V.A.T hailipi kampun..analipa mtumiaji wa mwisho.
Kwa Tanzania ilivyo ninavyoijua mimi, siky zote wana terget sehemu yenye wingi wa watu ndo inaelekeza hapo kodi zote, toka nimeanza kusikiliza bunge la budget sijwahi ona wakishusha kodi, mara nyingi wanapandisha tena sana sana kwenye hizi luxury needs.
 
Tatizo siyo kodi mkuu, hizo ni cheche tu. Tanzania ni miongoni mwa nchi chache za mwisho mwisho kwa kutoza gharama kidogo za Data, expect more for the coming days.
Pili, haya makampuni ya simu yamefikia wakat sasa kwamba there is no new subscriber's, wateja ni wale wale , number of subscribers haiendi juu.. hao hao waliopo ndo wanagawana.. kwa hyo maana yake revenue haiongezeki... na unakuta bado hawajapata profit...so wht to do ndo unacholalamika ambapo bado bei haijapanda kisawa sawa... kodi siyo tatizo maana kampuni kama haipat faida..haitozwi kodi..na V.A.T hailipi kampun..analipa mtumiaji wa mwisho.
Sasa ukiongelea Subscribers kupanda na kushuka, I think they re better off kushusha gharama ya Internet kwasababu hapo ndipo watakapofanya biashara kubwa kuliko kwa bei hizi. Ofcourse vitu kama Internet ni luxury needs, so mtu anaweza ishi bila kuwa navyo, so bei inapopanda, maana yake purchasing power ya watu inapungua, ambapo kwa mfano kama hapo mwanzo walikuwa wanapata wateja 100 wanaojiunga na vifurushi hapo mwanzo, sasa hivi watapata wateja 60-70, kwa namba hii, ina maana kama ni profit utaipata kwa watu hao tu, lakini bei zingekuwa ni zile nzuri basi atleast wangejiunga wengi and instead of 60 now wangejiunga 90, sasa imagine, kukusanya hata kama ni tsh 50 kwa watu 90 versus kukusanya 100 kwa watu 60 and less kwa siku na wangeshindana kwa style hiyo, hata hao new subscribers wangetokea. Ni sawa na wewe unauza sukari Tsh 1,800 na mwenzako anauza Tsh 2,000. Wewe wa 1,800 unapata faida ya shillingi hamsini kwa kila kilo moja na mwenzako anapata faida ya Tsh 200 kwa kilo moja, katika hali ya kawaida, wewe wa 1,800 unaweza uza viroba kumi vha sukari wakati yeye mwenzako yuko na kiroba kile kile kimoja, sasa piga mahesabu kati ya wewe wa 1,800 na mwenzako wa 2,000 nani anafanya biashara kubwa na nani anazungusha hela nyingi kwa mwezi.

Kwa mfano bundle zingekuwa affordable, kila mtu angekuwa ananunua which means more money for them, lakini kwa style hii, wanaonunua ni wachache na bundle tunazonunua haziendani na thamani ya hela tunayotoa na wala hazitoshi kwa smartphone zetu ambazo ni kubwa, zenye application nyingi zinazotumia data na smartphone zenye 4g.

Bundle zingekuwa kwa mfano 2,000 naweza pata GB kwa wiki, ningekuwa na uwezo wa kuunganisha hata mbili kwa wiki moja kwasababu GB 1 kwa simu yangu kwa wiki hazitoshi, au hata kama ingekuwa 2,500 napata 1GB kwa wiki basi ningejiunga, na najua kisingemaliza wiki ningejiunga tena, so bila kujua ndani ya wiki moja, walikuwa na uwezo wa kupata 5,000 kutoka kwangu lakini siko radhi kutoa 5,000 kwa GB 1 tu kwa wiki nzima. Sasa kwa style hii wananikosa mimi na wengine ambao tunaweza kaa siku tatu bila bundle pamoja na kwamba tuna smartphone.
 
kama hujashtukia, siyo Data tu imebanwa...bali hata normal text..cku hzi watu hawapg pig simu tu ovyo for no reason.... utajikuta unanua 30 minutes for 24hrs ila unakuta karbu 15minutes zinaexpire.. tht means matumiz ya ya voice calls yamepungua.. watu sa hv ni whatsap.. na texts kwa sana.. hata wewe inawezekana toka asubuh hujapga simu...ila ushatumia nusu saa nzima kufanya activities znazoihusisha inernt... sasa kwann wasibane humo?? Hata ungekuwa manager wa tgo leo...watu wanatumia muda mwing internet kuliko kupga cm...cha kufanya ni kubana kwenye data.. ndiyo maana hv karibun umeona karbu mitandao yote sasa wameweka 4g... wanaboresha zaidi... wamewekeza billions for that... kwa hyo usijarbu kuihusisha serikali hata tone...serikal ilitoza kodi kwenye tgo pesa...m.pesa nk.. ndiyo maana tarrifs zilipanda ghafla...kodi hyo imetuathir sisi cyo wao..
TARAJIA BEI ZA INTERNET KUONGEZEKA MARA DUFU...
 
Back
Top Bottom