Vifungu mbalimbali vya Biblia vinavyopingana na ndoa ya Flora 'Kusekwa'

Hivi punde

JF-Expert Member
Apr 1, 2017
2,554
8,581
Baada ya kukutana na mijadala kwenye mitandao ya kijamii kuhusu Ndoa ya Daudi Kusekwa na Mwinjilishaji Madamm Flora kwa mara ya pili na imani ya kikristo,nikajaribu kurudi kwenye maandiko yanavyosema,Na haya ndio maandiko yasemavyo:

"Na mke akimwacha mumewe na kuolewa na mtu mwingine azini"Marko 10:12,

"Imenenwa pia mtu akimwacha mkewe na ampe hati ya talaka, lakini mimi nawaambia kila mtu amwachaye mkewe isipokuwa kwa habari za uasherati amfanya kuwa mzinzi na mtu akimwoa yule aliyeacha azini", Mathayo 5:31-32,

"Basi mafarisayo wakamwendea na kumuuliza, Je?ni halali mtu kumwacha mkewe? Huku wakimjaribu. Naye akajibu akawaambia Musa aliwaamuru? Wakasema Musa alitoa ruhusa kuandika hati ya talaka na kumwacha, Yesu akawaambia kwa sababu ya ugumu wa mioyo yenu aliwaandikia amri hii. Lakini tangu mwanzo wa kuumbwa Ulimwengu aliwafanya mume na mke.Kwa sababu hiyo mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe na hao wawili watakuwa mwili mmoja, hata wamekuwa sio wawili tena bali mwili mmoja, basi alichounganisha Mungu mwanadamu asikitenganishe.
Hata nyumbani tena wanafunzi wakamuuliza habari ya neno hilo. Akawaambia kila mtu atakayemwacha mkewe na kuoa mwingine azini juu yake, na mke akimwacha mumewe na kuolewa na mtu mwingine azini". Marko 10:2-12

"Kwa maana mwanamke aliye na mume amefungwa na sheria kwa yule mume wakati anapokuwa yu hai, bali akifa yule mume amefunguliwa ile sheria ya mume, basi wakati awapo hai mumewe kama akiwa na mume mwingine huitwa mzinzi, ila mumewe akifa amekuwa huru, hafungwi na sheria hiyo, hata yeye sio mzinzi ajapoolewa na mume mwingine"Warumi 7:2-3

"Wasimwoe mwanamke aliye kahaba na huyo aliye mwenye unajisi, wala wasimwoe mwanamke aliyeachwa na mumewe kwa kuwa yeye kuhani ni mtakatifu kwa Mungu wake"Mambo ya Walawi 27:1.

"Ndio alivyo aingiaye kwa mke wa jirani yake, kila mtu amgusaye huyo atakuwa na hatia"Mithali 6:32

"Lakini nawaambia wale wasioowa bado na wajane, ni heri wakae kama mimi nilivyo, lakini ikiwa hawawezi kujizuia na waoe, maana ni afadhali kuoa kuliko kuwaka tamaa, lakini waliokwisha kuoana nawaagiza wala hapo sio mimi ila Bwana, mke asiachane na mumewe lakini ikiwa ameachana nae na akae asiolewe au apatane na mumewe, tena mume asimwache mke" 1 Wakorintho 7:8-11

"Mwanamke hufungwa maadamu mumewe yu hai, lakini ikiwa mumewe amefariki yu huru kuolewa na mtu yoyote amtakaye katika bwana tu"1 Wakorintho 7:39.

Ukiolewa huna nafasi tena ya kuachika na kuolewa tena na ukioa ndo ushamaliza huna nafasi ya kuacha na kuoa tena.ikiwa mtaachana subili mpaka mmoja wenu afe ndio uoe tena.
 
1493718373033.png
kwa kifupi kwa maelezo niliyoyasoma hapo juu Frola hayupo sawa
 
Mbona mmemwandama huyu dada ndo wa kwanza kuolewa ndoa ya pili? Hebu tumwache atahukumiwa na Mungu wake.maana dhambi si moja hapa duniani ati kuolewa mara ya pili ndo kafanya dhambi kubwa sana,
Wangapi wanazini, wanasema uongo, na dhambi zingine kibao tu.
 
Mbona mmemwandama huyu dada ndo wa kwanza kuolewa ndoa ya pili? Hebu tumwache atahukumiwa na Mungu wake.maana dhambi si moja hapa duniani ati kuolewa mara ya pili ndo kafanya dhambi kubwa sana,
Wangapi wanazini, wanasema uongo, na dhambi zingine kibao tu.
Ishu isingejadiliwa sana kama angefunga ndoa ya bomani lkn kanisani, hapana hiyo siyo ndoa ni kujifurahisha tu
 
Mbona mmemwandama huyu dada ndo wa kwanza kuolewa ndoa ya pili? Hebu tumwache atahukumiwa na Mungu wake.maana dhambi si moja hapa duniani ati kuolewa mara ya pili ndo kafanya dhambi kubwa sana,
Wangapi wanazini, wanasema uongo, na dhambi zingine kibao tu.
Tatizo yeye aliwaimbia watu; UVUMILIVU
 
Biblia siyo ya wakatoliki pekee.
Yes. Ila mtoa mada anadai ni maoni ya wakatoliki. Mimi nikiwa mmojawapo naelewa hayo sio maoni ya wakatoliki ni mafundisho ya biblia kuhusu ndoa na talaka! Hao wakatoliki wameyatolea wapi hayo maoni? Hatuna utamaduni wa kucomment kwenye ndoa individual za watu.
 
Kwa hiyo hizo nukuu ni za wakatoliki au biblia?
Nukuu ni za biblia na zimenukuliwa kiusahihi. Ninachosema ni kwamba kanisa katoliki halihusiani na ndoa ya flora maana yeye mwenyewe sio mkatoliki. Kumbuka heading inawataja wakatoliki kwa sababu anazojua mketa thread peke yake.
 
Back
Top Bottom