Vifo viwili vyenye utata mpaka leo majibu hajapatikana

m-boy

Senior Member
Aug 20, 2023
147
477
Habari wana JF,

Hakika ukistaajabu ya musa utaona ya virauni.

Kuna bint alikuwa single mother amepanga mtaa fulani ktk mji mmoja maarufu hapa jiji Dar.

Huyu bint alipopanga ilikuwa ni jirani na shangazi yake ambae alikuwa na mji mkubwa.

Huyu bint alikuwa akiishi peke yake kwa sababu mtoto wake mwenye umri wa miaka 5 alikuwa akiishi kwa dada yake ambapo palikuwa na umbali dk 60 kwa usafili wa umma (daladala)

Siku ya tukio alimuaga shangazi yake anakwenda kwa dada yake mara nyingi huwa akitoka anamuaga shangazi yake iwe kwa kumpigia cm au kwenda kuonana nae ana kwa ana.

Alipofika kwa dada yake akafanya shughuli zake mida ya saa 10 akaondoka lkn hakusema anakwenda wapi. Huyo bint alikuwa anakopesha mashuka kwa hiyo alikuja na bag dogo ambalo lilikuwa na baadhi ya nguo, (shuka)

Alipoondoka hapo hakupatikana tena na wala kwake hakurudi maisha yakasonga huku watu wahajui yupo wapi.

Baada ya wiki moja toka atoweke dada yake alipigiwa cm kutoka kituo cha polic cha kati akaambiwa mdogo wake yupo kituo cha polic hapo, lkn kwa cm ile ninahisi dada mtu aliambiwa jambo maana alipopokea cm baada ya mahojiano akapiga ukunga mkubwa sanaaa, baada ya hapo tukachagua vijana 2 waende huko.

Waliporudi wakatuambia kwmba bint amefariki dunia. Ilikuwaje?

Mama mmoja ambae ndio mwenye nyummba wakati anafanya usafi aligundua ya kwmba chumba kimoja cha mpangaji wake kimefungwa kwa nje lkn ndani kuna mtu amelala kitandani hili jambo likamtia mashaka, akaita sanaa bila mafanikio itabidi atoe tarifa kwenye selikali za mtaa polic wakaja kuvunja ndio wakakuta mait ipo kitandani, chini ya kitanda kulikuwa na mwalovela na bint alikuwa na mimba changa, mpangaji hajulikani alikpo kwa maana mpangaji alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na huyu bint.

Taarifa hii ilipoifikia familia wakasema wanamjua huku kijana ni mpole na mtulivu sana haijulikani nn kilitokea mpaka ikawa vile , kijana hapatikani kwenye cm na hawajui ndugu zake.

Polic wanasema walikuwa wanaangalia maiti zilizokaa muda mrefu wakazike kwa bahati ndio polic mmoja kakumbuka hii maiti ilikuwa na cm ndani wakaichaji na kuchukua namba na kupiga, mpaka anapigiwa dada yake huyu tayali ndugu 3 wa familia walikuwa wamepiwa cm kutaarifiwa juu ya jambo hilo, baada ya uchunguzi ndugu wakakabiziwa mait wakaenda kuzika.

No 2
Huyu bint alikuwa anamahusino ya kimapenzi na mume wa mtu kwa miaka 5 , kwa maelezo yake aligundua ya kwmba yule mwanamme ana mke baada ya miaka 2 toka waanze mahusiano.

Mwanamme alikuwa anamlazimisha sana mwanamke azae lkn mwanamke alikuwa hataki mwisho mwanamke akaamua kubeba mimba,
Japo matunzo yalikuwa hafifu lkn bint alifanikiwa kujifungua salama hospitali ya rufaa amana.

Baada ya miezi 3 toka mtoto azaliwe siku moja binti ameingia ndani kwake amemkuta mtoto wake yupo kwenye ndoo kubwa ya maji na yupo ktk hatua ya mwisho ya kugombania uhai wake, alipomtoa haikuchukua hata dk 2 mtoto akafariki.

Hapa ndio mimi pia nilipata kigugumizi,

Je, yeye alikwenda wapi?

Chooni au kuchota maji?

Nani aliingia ndani kipindi yeye hayupo?

Basi akapigiwa simu jamaa aliezaa nae akaja wakachukua mait wakaizika, toka pale hakuna mawasiano na mwanamme hata alipozikwa mtoto hapajui, bado yupo ndani mpka 40 ndio atatoka kuna maswali mengi natamani kumuuliza baada ya kutoka na kuonana nae ana kwa ana,hakika vifo hivi viwili kwangu bado sijapata majibu toshelezi.
 
Inahuzunisha sana. Kuna la kujifunza hapa.

Huyo wa kwanza huenda alitoa/alitolewa mimba kienyeji halafu akafungiwa kwa nje.

Hatari sana
 
Kesi ya vifo vya utata kama hivi kibongobongo ndio imeisha hyo,

lakini Kwa wenzetu watafanya juu chini mpaka wajue chanzo, na ikiwa Kuna wahusika au muhusika yeyote lazima atajulikana tuu.

Daah inahudhunisha sana
 
Back
Top Bottom