Vifo vilivyosababishwa na Polisi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vifo vilivyosababishwa na Polisi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by 2mbaku, Sep 5, 2012.

 1. 2mbaku

  2mbaku JF-Expert Member

  #1
  Sep 5, 2012
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 317
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  1. Januari 5, mwaka jana, saa tano wakati Jeshi la Polisi mkoani Arusha lilipoamua kutawanya maandamano ya wafuasi na mashabiki wa Chadema walioandamana kilomita moja kutoka Hotel ya Mount Meru kwenda Viwanja wa NMC. Wakati wakiwatawanya maandamano hayo, vijana watatu akiwamo mmoja kutoka Kenya walifariki dunia na wengine kadhaa kujeruhiwa.
  2.
  Wiki iliyopita, polisi mkoani Morogoro walisababisha kifo cha mtu mmoja, Ally Zona na wengine wawili kujeruhiwa katika harakati za kuvunja maandamano ya Chadema.
  3. Kifo cha kutisha cha Mwangosi kilichotokea Mkoani Iringa.
  nk.

  Tume zimeudwa.
  Asante kwa hilo.Lakini haziaminiki.
  Vipi kuhusu ripoti za tume hizo mbona kimya, na mbaya zaidi wauaji wako wazi?
  Damn Tanzania!!!!
   
 2. Domy

  Domy JF-Expert Member

  #2
  Sep 5, 2012
  Joined: Dec 12, 2011
  Messages: 4,702
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Kuna siku itafika watatoa report kwa lazima,shenzy zao
   
 3. Bishop Hiluka

  Bishop Hiluka Verified User

  #3
  Sep 5, 2012
  Joined: Aug 12, 2011
  Messages: 4,100
  Likes Received: 1,424
  Trophy Points: 280
  Unategemea nini kama muuaji ni polisi na tume inaundwa na polisi
  wenyewe ili kujichunguza? Ni nani anaweza kujichunguza na kutoa
  ripoti kuwa ana hatia? Hiki ni kiini macho...
   
 4. B

  Bahati Risiki JF-Expert Member

  #4
  Sep 5, 2012
  Joined: Jun 20, 2012
  Messages: 531
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Tanzania inaongozwa na wahuni. Kila siku kuwaua raia wasio na hatia? Hivi ni lini viongozi wetu watamwogopa Mungu? Ni lini hawa polisi wataongea na watoto wao kama binadamu? Unawezaje kuuwa mzazi mwenzio na kisha kwenda nyumbani kufurahia maisha na mkeo na watoto wako?
  Ni kwa nini serikali haidhubutu hata kukemea mauwaji haya? Hadi dunia inatushangaa lakini halipo linalofanyika? Ni kwa nini CDM inakuwa tishio sana kwa polisi? Je hawa polisi tu ndiyo walioahidiwa maisha bora katika kuwaangamiza raia wenzao? Je watoto wao wanaepuka shule za kata? Je wakiugua wanatibiwa India? Je wao wana TANESCO yao? Je sisi tunapohangaika hata huduma muhimu kwa binadamu kama maji wao serikali inawanyeshea mvua?
  Imefika wakati tujifikirie mara mbili. Haya mambo ya wachache kutumia nguvu waliopewa na serikali hii dhalimu kuwaua wenzao inakaribia ukomo.
  Polisi hawa itafika siku watashindwa hata kuvaa uniforms zao kwani raia watawachinja kama kuku. Itafika siku hawatadhubutu kunyoosha mkono kujikusanyia hongo kwani watanzania watawakata hiyo mikono. Nguvu ya umma ni kubwa na inajigenga kila siku. Hiyo siku ikifika hata kikwete ataingia kwenye handaki kama Sadam.
   
 5. MANGUNGO

  MANGUNGO JF-Expert Member

  #5
  Sep 5, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 1,538
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 133
  Gun can't kill people but people kill people..........siwezi kuwalaumu polisi hawa wanatekeleza agizo la serekali na viongozi wa cccm kama nape.
   
Loading...