Vifo ugonjwa wa ajabu vyaongezeka hadi 11

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,696
2,253
Ummy-Mwalimu.jpg


IDADI ya watu waliofariki kutokana na kuugua ugonjwa wa ajabu ulioripotiwa mkoani Dodoma, imefikia 11.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, alisema hayo jana katika taarifa yake aliyoituma kwa vyombo vya habari kupitia kurugenzi ya mawasiliano ya wizara hiyo.

Alisema kwamba, idadi ya walioripotiwa kuugua ugonjwa huo nayo imeongezeka na kufikia 43 hadi kufikia Julai 3, mwaka huu baada ya ugonjwa huo kuripotiwa Juni 13 mwaka huu.

“Ugonjwa huo uliripotiwa Juni 13, mwaka huu wilayani Chemba, Mkoa wa Dodoma na hadi kufikia jana (juzi), kulikuwa na wagonjwa 43 na vifo 11.

“Mbali na Mkoa huo wa Dodoma, Mkoa wa Manyara nao umeripotiwa kuwa na wagonjwa wa aina hiyo.

“Katika Halmashauri ya Chemba, kumeripotiwa kuwepo wagonjwa 34, Kondoa wanne, Dodoma Manispaa mmoja, Chamwino mmoja na Kiteto watatu.

“Vifo 10 viliripotiwa katika Halmashauri ya Chemba na kifo kimoja kiliripotiwa katika Halmashauri ya Kiteto,” alisema Ummy katika taarifa hiyo.

Pamoja na hayo, alisema uchunguzi wa awali wa kimaabara uliofanywa kwa baadhi ya vyakula walivyotumia wagonjwa, ulibaini kuwa vyakula hivyo vilikuwa na sumu kuvu iitwayo aflatoxins.

Chanzo: Mtanzania

Wakuu cha msingi hapa tuchukue tahadhari maana haya magonjwa yanayozuka kila mara yanatishia amani
 
Back
Top Bottom