Richard
Platinum Member
- Oct 23, 2006
- 16,762
- 26,051
Kuna wanafunzi ambao wanaweza kwenda kusoma kozi mbalimbali katika nchi za Uingereza au Marekani, lakini huishia kulipa mamilioni na mamilioni ya fedha zikiwa ni gharama za masomo (Tuition fee) na malazi au "accommodation" na fedha za kujikimu.
Wakati mwingine kutegemea na chuo kikuu ulichochagua kwa kozi yoyote ya shahada ya kwanza, vyuo vingi hutoza gharama za masomo kwa mwanafunzi wa nje hadi kufikia pauni za Uingereza elfu 18,000 sawa na zaidi ya shilingi milioni 50 kwa miaka mitatu.
Lakini katika utafiti ulofanywa na kampuni moja iitwayo Fair FX ambayo inashughulika na ubadilishaji na uuzaji fedha, nchi za Ujerumani, Sweden na Afrika Kusini ndizo zinaongoza kwa ada ndogo na athamni ya fedha itolewayo yaani value for money.
Kwa mfano mwanafunzi anaetaka kwenda nchini Ujerumani kusoma anaweza kugharamia kiasi cha fedha za kitanzania milioni 18 kwa mwaka au sawa na Euro Zaidi ya elfu 7, wakati kwa nchini Sweden ni kiasi cha shilingi milioni 19 sawa na fedha za Sweden SEK au krona elfu 70.
Pia hata kwa Afrika Kusini kwa shilingi milioni 18 inaweza kuwa sawa na zaidi ya Rand laki moja.
Katika orodha ya vyuo vyenye gharama nafuu duniani ukiangalia utaona kwamba nchi ya Italy inaongoza kwa vyuo vikuu vyake viwili vya Scuola Superiore Sant’Anna na Scuola Normale Superiore di Pisa.
Wanafunzi waliofanya uzuri zaidi katika mtihani wa kuingia katika vyuo hivi hawalipi gharama za kozi na pia hupewa fedha za kujikimu. Hata hivyo huwa ni kwa ajili ya wale wanafunzi wa kutoka katika mataifa ya barani Ulaya.
Orodha ya vyuo 10 nafuu kwa ada duniani.
Nchini Sweden chuo kikuu cha KTH cha Royal Institute of Technology kinatoza Euro elfu 5 na mia mbili hivi.
Kusoma katika nchi za Marekani, Uingereza na Australia kwa sasa imekuwa ni ndoto kubwa kwa baadhi ya wale wanafunzi watarajiwa kwani Marekani ada pekee kozi moja na gharama zote za kujikimu kwa mwaka inagharimu kiasi cha dola zaidi ya elfu 58 sawa na shilingi za kitanzania zaidi ya milioni 127.
Australia wao wanatoza kila kitu kwa kozi ya mwaka mmoja zaidi ya dola za Australia elfu 31 sawa na zaidi ya shilingi za kitanzania milioni 51.
Hii pia ni orodha ya vyuo nafuu kabisa duniani kwa wale wanafunzi wenye angalau mpunga wa kutosha kuweza kwenda huko, kusoma.
Wanafunzi wanashauriwa kuangalia gharama za maisha kwa ujumla katika nchi wanazotaka kwenda kusoma vyuo na pia kuzingatia mabadiliko ya thamani ya fedha katika nchi hizo.
Pia ipo orodha inayoonyesha nchi ambazo ni ghali sana kwenda kusoma na ambazo zina maisha ya gharama za juu kabisa.
Nchi hizo zinaongozwa na Marekani na Australia na kama nilivyoeleza hapo juu nchi hizi pia zina utaratibu mgumu wa kuwaruhusu wanafunzi wa kimataifa kwenda kusoma kwenye vyuo vyao.
Nchi 10 ghali sana kusoma na kuishi duniani.
Hata hivyo bado katika orodha ya vyuo bora kabisa duniani au "Higher Education World University Ranking", chuo kikuu cha Oxford cha nchini Uingereza ndicho kinachoongoza kikifuatiwa na chuo kikuu cha California u California Institute of Technology.
Chuo kikuu cha Stanford kinashika nafasi ya tatu huku chuo kikuu cha Cambridge kikiwa kwenye nafasi ya nne.
Lakini bado kusoma katika vyuo bora kabisa duniani ni moja ya matamanio ya wanafunzi wengi waliofanya uzuri katika masomo yao ya kidato cha sita.
Nchi kama China nayo inajitahidi kuwafadhili baadhi ya wanafunzi mbalimbali wa kutoka katika nchi za Afrika katika Nyanja kama uhandisi umeme na kozi zingine ambao wapo hutoa nafasi.
Ila mwisho wa siku ni uwezo wa fedha ndiyo huamua usome katik vyuo vya aina gani, lakini pasipo na shaka yoyote mwanafunzi mtarajiwa akifanya utafiti wa kutosha, basi anaweza kufanikiwa kusoma katika chuo chenye gharama nafuu kabisa.
Chanzo: FairFX.