Vidume tuliopitia kwa ngariba bila ganzi tukutane hapa kukumbushana yale maumivu!

mpenda arage

JF-Expert Member
Nov 10, 2015
1,676
3,805
Ni miaka mingi imepita tangu niondolewe hili pulizo. Najiskia fahari sana kufanyiwa hii huduma bila ganzi. Niliumia ila leo najivunia.
Ilikuwa asubuhi yenye baridi kali. Kama saa kumi na mbili kasoro. Nikashtuka mlango wa nyumba niliyokuwa nimelala na wenzangu unafunguliwa. Mjomba wangu na vidume viwili vilivyoshiba vikaingia. Nilikuwa na taarifa kuwa leo govinda linarestishwa in pisi, ila sikutegemea ingekuwa kwa mtindo huu.
Nikaamrishwa kupanda mgongoni kwa njemba mojawapo, nikatii. Nlivyokwisha panda mgongoni, nikafunikwa na shuka na safari ikaanza!!
Sikujua naelekea wapi, nilishtukia tu nimefika mahali naskia sauti za watu. Ile nashangaashangaa, nkashtukia nimeshushwa chini na kukalishwa mahali(baadae nlikuja kugundua kuwa ni kitanda cha telemka tukaze), nilivyokalishwa juu ya kitanda, nilipigwa pini kwa miguu ambayo hadi leo naiheshimu.
Nkashtuka dushe inashikwa, kutahamaki! Ile naanza kulia..maaa...!! Ngariba kamaliza. Haikuchukua muda nikapona tena bila bandeji wala plasta!
Naamini tupo wengi tuliopitia hii huduma bila ganzi. Nimekaa nikaona tutafutane ili ikiwezekana huu utaratibu tuupigie kelele urudi. Naamini hospitali ndio chanzo kikubwa cha mfumko wa vibamia na mashoga nchini! Karibuni.
 
Nakumbuka ilikuwa siku flani ya mwanzo wa kikupwe, mwezi wa sita miaka hiyo ya 90's.
Ilikuwa ni asubuhi ya saa kumi na mbili, ni siku nisiyoisahau.

Ingawa tulikuwa na taarifa ya nini kitatokea siku nne zijazo, ile asubuhi zile mishemishe zake zilituogofya sana. Tuliamshwa na mzee, na
tukapewa GR na mwelekeo. Tukafika, tukawakuta wenzetu pia.

Tukakutana na ngariba wa Kimatumbi, tukapigwa timbwili la nguvu, bila ganzi, bila kushikiliwa, goma likaisha. Wa kulia walilia, wa kukomaa tukakomaa, goma likaisha. Baada ya siku zisizozidi saba, kidonda kikapona, maisha yakaendelea.

Kuenzi hii kitu, wiki iliyopita mtoto wangu wa kwanza naye nimempa doso la asubuhi kweupeeee, kavukavu bila ganzi, ila leo kashapona na yupo sawa kabisa. Kitu cha bila ganzi kidumu.....kidumu!
 
Sisi wakurya tunasimama uwanjani tena unasimama wima kama bendera ya taifa inapandishwa au kushushwa

Hapo ngariba abaweza kukata govinda kwa visu 3 ama vi4....... maana anakata kidogo kisha anapunzika kana dk3 ama 4.... huku anaenda kumwa pombe, anakuacha wewe umesimama bila kutikisika

Hapo ndo unachukuliwa kama mwanaume...

Mimi nilikatwa visu 2,,,, lani nilikuwa naona dunia inazunguka kabisa...... bahatu nzuri nilisimama hadi kumaliza na kuwa mwanaume kamili....

Lani nikikumbuka siku hiyo.... hata sipendi kukumbuka kabisa
 
Ha ha kuna jamaa alimwaga mbonge la kimba aisee, kwa sasa ni bosi maeneo flani, tukikutana mara chache wik end tukikumbushana mambo ya zamani, nikimchomekea hiyo kitu kukauka mbavu kwa kicheko,lakini kwa sasa na hili tishio la ukimwi, vile vitendea kazi si salama tena...kwa kweli sishauri..Hospitary ni best option.
 
Sisi wakurya tunasimama uwanjani tena unasimama wima kama bendera ya taifa inapandishwa au kushushwa

Hapo ngariba abaweza kukata govinda kwa visu 3 ama vi4....... maana anakata kidogo kisha anapunzika kana dk3 ama 4.... huku anaenda kumwa pombe, anakuacha wewe umesimama bila kutikisika

Hapo ndo unachukuliwa kama mwanaume...

Mimi nilikatwa visu 2,,,, lani nilikuwa naona dunia inazunguka kabisa...... bahatu nzuri nilisimama hadi kumaliza na kuwa mwanaume kamili....

Lani nikikumbuka siku hiyo.... hata sipendi kukumbuka kabisa
Sasa si uonevu huo? , ngariba wa kweli ni ndani ya dk 3 ashamaliza kazi..
 
Mimi naikumbuka yangu miaka ya 80's..hatari sana
Jando ya bila ganzi inatengeneza usugu wa kichwa cha ub..oo kiasi kwamba ukiwa unapiga mambo ngumu sana kushusha wazungu mapema,sbb mishipa fulani ya hisia pale mbele inakuwa imekufa/sizi.

Sisi tulikuwa tunaitwa 'Wanyamlusi" unapewa na kifimbo kidogo kanaitwa "sungururu" ambapo uume ukisimama basi unapiga fimbo sehemu ya enka ili ilale.

Baadae nikapewa kazi ya kuwa nataili,ndio chanzo cha jina Ngaliba Dume ,mengine siwezi sema sbb za miiko ya jando
 
Aisee hivi kumbe nyie mnaruhusiwa kutoa siri za jandoni,sisi mbona tunaambiwa kuwa ni mwiko kutoa siri za unyagoni? Kweli mfumo dume hautaisha Afrika.
Tupe kidogo ilikuwaje huko kwenu?
 
Nadhani mfumo ungekuwa hatarishi kwa mazingira ya sasa kutokana na wingi wa magonjwa yaliyopo, ila kiukweli maumivu yake kipindi hicho bora watoto wa ganz wa kipindi hch
 
mmh hivi wanaume mnaruhusiwa kumbe kutoa siri za jandoni ingekua mwanamke tungekuita msungo ila wanaume sijui mnaitwaje
 
Back
Top Bottom