Vidume 18 kupima DNA kwa Makonda

Vidume 18 kupima DNA kwa Makonda

kirerenya

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2013
Posts
1,698
Reaction score
2,262
DNA.jpg
​

Makonda alisema hatua hiyo imefikiwa na wanasheria na maofisa ustawi wa jamii baada ya kuhoji wanaume waliodaiwa kuwatelekeza watoto, katika malalamiko yanayoendelea kutolewa na wanawake kuanzia Jumatatu katika ofisi hizo, Ilala.

Mkuu wa Mkoa Makonda alisema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuelezea maendeleo ya zoezi linalomalizika leo.

"Jumla ya wanaume 18 ambao walibisha kuwa watoto sio wao wamekubali kwenda kupimwa DNA kwa Mkemia Mkuu ili kupata uthibitisho wa uhalali wa mzazi na hao ni kati ya wanaume 198 walioitikia wito na kuja ofisini kwangu," alisema Makonda.

Kadhalika, alisema kati ya wanaume 198 waliofika katika ofisi hizo baada ya kuandikiwa barua za wito, 179 walikubaliana na wanawake waliozaa nao mikakati ya kulea watoto husika.

"Familia 179 zimefikia muafaka," alisema Makonda na "haya ni mafanikio makubwa. Kama watu waliokuwa hawahudumii familia na leo hii wamekubali kuhudumia na kurudi nyumbani kwa amani, kazi hii imezaa matunda."

Makonda alisema kati ya wanaume 198 waliofika katika ofisi hizo kutafuta mwafaka, 19 kati yao mashauri yao yamepelekwa mahakamani ili kutafuta suluhu.

"Kazi inaendelea vizuri, tunaona mafanikio kwa sababu wanawake waliojitokeza ni wengi wanaokosa huduma kutoka kwa wanaume zao," alisema. "Wanaume waliopewa barua za wito nao wamekuja wakasilikizwa na mwafaka ukapatikana."

Pia alisema wanawake 1,498 wamejitokeza katika siku tatu kwa ajili ya kutoa malalamiko yao na kupewa msaada wa kisheria.Makonda alisema kutokana na kuwapo kwa idadi hiyo kubwa ya wanawake, wameongeza wanasheria 200 na maofisa ustawi wa jamii 60 na kusababisha kuwapo kwa watoa huduma 378.

"Kwa sababu ya mwitikio mkubwa wa wanawake, tumelazimika kuongeza wanasheria na maofisa ustawi wa jamii ili kazi hii ifanyike kwa haraka," alisema Makonda.

ZAMU YA WANAUMEAidha, Makonda alisema baada ya kusikiliza wanawake waliotelekezwa, kanzia Jumatatu itakuwa zamu ya wanaume ambao wameandikiwa barua za wito.

"Ingawa wapo baadhi ya wanaume ambao wameandikiwa barua za wito na wameshakuja kusikiliza walichoitiwa, kuanzia Jumatatu itakuwa ni siku ya kuwasikiliza baada ya kuwasikiliza wanawake," alisema Makonda.

Alisema wanaume ambao wamepewa wito huo wanatakiwa wajitokeze kusikiliza na endapo watakaidi hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

Makonda pia aliwataka wanawake na wanaume wenye matatizo ya kutelekezewa watoto kweli wajitokeze katika ofisi hizo ili wapate msaada wa kisheria bure badala ya kuandika kwenye mitandao ya kijamii.

"Kama kweli mtu ana matatizo ni wajibu wake kuja hapa ili asikilizwe na kupatiwa msaada bure badala ya kuandika kwenye mitandao ya kijamii ambako hakuna majibu," alisema Makonda.

Leo ni siku ya mwisho ya kutoa msaada wa kisheria kwa wanawake ambao walitelekezewa watoto na wanaume waliozaa nao.

Chanzo: Nipashe
 
Kwahiyo anatuambia problem solved?! In 5 days tatizo zito la kijamii kama hili limekuwa solved?

Kuna hatua zozote ameziweka kuhakikisha kuwa waliotelekeza hawatelekezi tena?

Kwani walikuwa wanatoa msaada wa kisheria au kifamilia? Maana kusema familia zimefikia muafaka maana yake hakuna hatua za kisheria hapo, ni maongezi tu.
 
order ya kupima DNA inatolewa na makonda au mahakama?.
wanasheria mnisaidie hapo.
Hapo hajazungumza kama Mc-Onder Mkuu,
Bali Naibu Raisi.
By the way ili kuondoa mkanganyiko hii huduma ya DNA wangeiondolea mikwara mingi katika kuipima, yaani ingekua kama kupima malaria tu
 
order ya kupima DNA inatolewa na makonda au mahakama?.
wanasheria mnisaidie hapo.
Lazima kutakuwa na makubaliano na maridhiano. THen unayaweka hayo kwenye legal paper, baadae sample inatoa majibu.
 
Naomba tukishamaliza kupima Wanaume DNA basi kwa ' Ubora ' huo huo pia zipatikane Mashine za kupima Wanaume wenye ' Hips ' na ' Bums ' kisha tupate maelezo ya Kutosha ya ' Kitabibu ' kwamba nini kimesababisha Wao kuwa hivyo.
 
Naomba tukishamaliza kupima Wanaume DNA basi kwa ' Ubora ' huo huo pia zipatikane Mashine za kupima Wanaume wenye ' Hips ' na ' Bums ' kisha tupate maelezo ya Kutosha ya ' Kitabibu ' kwamba nini kimesababisha Wao kuwa hivyo.
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] great thinker
[emoji13] [emoji12]
 
Nchi hii kuna mambo mengi ya kijinga, mojawapo ni hili!
 
Back
Top Bottom