Wakuu nimekutana na hii video katika mitandao ya kijamii na kudaiwa kuwa ni ya mtawala wa Mongolia (Black Khan) alipoitembelea China mwaka 1440 katika utawala wa Ming (Ming Dynasty).
Je, uhalisia upoje?
Your browser is not able to display this video.
Tunachokijua
Utawala wa Ming (Ming Dynasty) inayojulikana rasmi kama Great Ming, ilikuwa nasaba ya kifalme ya China iliyotawala kuanzia mwaka 1368 hadi 1644, baada ya kuanguka kwa Yuan Dynasty iliyokuwa inaongozwa na Wamongolia. Ming ilikuwa nasaba ya mwisho ya kifalme nchini China iliyotawaliwa na Han Chinese, ambao ni kundi kubwa zaidi la kikabila nchini humo.
“Khan” ni cheo cha kihistoria cha watu wa Turkic na wa Mongolia kilichoanzia miongoni mwa makabila ya wahamaji katika maeneo ya nyika za Eurasia ya Kati na Mashariki, kikimaanisha mfalme au kiongozi mkuu.
Madai
Kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii ikiwemo Facebook, X na Instagram kumekuwa na video isiyo na rangi, inayosambaa kuanzia 2025 na kudaiw akuwa ni video ya zamani iliyopatikana ikimuonesha Mtawala wa Mongolia wakati huo aliyeitwa Black Khan akiwa ameutembelea utawala wa Ming nchini China kwa mara ya kwanza mwaka 1440.
Uhalisia wa madai hayo
Ufuatiliaji umejirdhisha kuwa video hiyo inayosambazwa na madai ya kuhusishwa na miaka ya 1400 ni Potoshi.
Kwa kutumia nyenzo ya google ya reverse imebainika kuwa video hiyo imekuwa ikisambaa katika mitandao ya kijamii kuanzia mwaka 2025 ikiwa na madai yanayofanana. Mathalani video za awali zilichapishwa kati ya mwezi April 2025. Tizama hapa, hapa na hapa
JamiiCheck imebaini kuwa video hiyo imehaririwa kutoka katika video halisi ya mtayarishaji wa maudhui ya Youtube, Darren Jason Watkins Jr. (IshowSpeed) akiwa nchini China mwaka 2025 na kuichapisha katika Youtube Yake Aprili 7, 2025.
Lakini pia hakuna kumbukumbu zinazoonesha kuwa Mongolia ilishawahi kuwa na mtawala (Khan) aliyefahamika kwa jina la Black. Aidha kwa mwaka 1440 hakukuwa na kamera bado hivyo si kweli kusema kuwa ni video ya mwaka huo.