VIDEO:Kafulila (NCCR), Hassanali CHADEMA wakijibu Maswali ya wapigakura Kigoma Kusini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

VIDEO:Kafulila (NCCR), Hassanali CHADEMA wakijibu Maswali ya wapigakura Kigoma Kusini

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by bagamoyo, Oct 1, 2010.

 1. b

  bagamoyo JF-Expert Member

  #1
  Oct 1, 2010
  Joined: Jan 14, 2010
  Messages: 4,522
  Likes Received: 2,108
  Trophy Points: 280
  • Kero Daraja la Mto Malagarasi linahitaji Tshs. Billioni 22 tu.
  • Rais Bush mwaka 2003 aliahidi mabilioni ya shillingi kufua umeme kwa kutumia mto Mlalagarasi, pesa hizo zipo wapi na kazitafuna nani, kwani fedha zilishatiwa ktk akaunti ya serikali ya Tanzania?
  • Mto Malagarasi Megawati 80 zinaweza kuzalishwa
  • Kisomo cha watu wazima kimesaulikwa wakati kina mama wengine jimboni hawajui kusoma na kuandika
  • Jembe la Mkono limepitwa na wakati
  • Kipaumbele Maendeleo Vijijini
  • Mwafaka wa kitaifa baina ya wananchi na wanasiasa
  • miundo mbinu Kigoma majimbo ya CCM Kilometa 7 tu za lami na Jimbo chini ya Chadema kilomita 93 lami.
  Video clip kwa hisani ya TANGIBOVU wa YOUTUBE
  Part 1

  Part 2
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 2. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #2
  Oct 1, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Mgombea anajidani akiwa amevaa Cap!
   
 3. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #3
  Oct 1, 2010
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,221
  Likes Received: 7,340
  Trophy Points: 280
  Ukiangalia kwa makini hii ni 'propaganda'' ya kafulila. Nimesikiliza sehemu yote sikumsikia mgombea wa Chadema isipokuwa katika maswali na majibu. Anyway, kuna hata ninayoona yana uwalakini.
  1. Katiaka agenda nne za Kafulila suala la afya hakulitaja na kwahiyo halipo katika agenda za chama chake. Ametaja afya katika majibu baada ya kumsikia Hassanali akisema agenda zake ni Afya,Elimu na kilimo. Hili linatosha kuonyesha kuwa Kafulila ni ''ambitious but not objective''
  2.Kafulila kasema ataanzisha mfuko wa jimbo wa elimu na atachangia 30% ya mshahara wake. Tatizo la maendeleo haliwezi kutatuliwa na fedha za mtu mmoja. Hii ni ghilba kwa wananchi kwasababu 30% ya mshahara wa Mbunge kimaandishi ni apprx 600,000 sawa na posho za siku 4 za mbunge Dodoma. Huu ni udanganyifu kwasababu posho za wabunge zinafikia Mil 8.[kukwepa kodi, eti mshahara ni 2M]
  3. Amesema atatumia ushirika kuleta mapinduzi ya kilimo kwa kuwawezesha wakulima wapate mikopo ya umwagiliaji. Kafulila nenda Kilimanjaro ukaone, watu wamekuwa na irrigation schemes Milimani kabla ya mjerumani hajaja. Tatizo la irrigation sio pesa ni mwamko na uelewa wa watu. Kama watu hawajui kwanini wanatakiwa kuwa na irrigation scheme, pesa haziwezi kusaidia lolote. Kafulila anadhani maendeleo ni pesa!
  4. Ametaja serikali shirikishi kama agenda, hakufanunua shirikishi kivipi na itasadia vipi kumkomboa yule mwananchi maskini asiye na elimu na mwenye afya mbaya pale kigoma.
  5. Amesema kigoma ilitoa manamba wengi kwasababu walikuwa na nguvu. Huu ni uongo wa kiwango cha juu. Kama wangekuwa na nguvu kuliko watanzania wengine basi tungewaona enzi hizo wakiwa katika ajira kama polisi au majeshi. Kafulila, watu wa kigoma walikuwa manamba kwasababu ya uduni wa elimu. Elimu iliwafanya wawe wanyonge hata mbele ya watanzania wenzao. Nenda katika mikoa yenye mabaki ya kambi za manamba, utagundua kuwa hali za maisha kwenya kambi za manamba ni duni licha ya nguvu za watu wa sehemu hizo. Ni sehemu ambazo elimu ni duni sana, kafulila nenda Tanga utathibitisha ninayosema. Manamba anaowasifu kafulila walikuwa exploited na watanzania wenzao kwasababu ya kukosa elimu. Kama kukosa elimu ndio nguvu anyozungumzia kafulila, basi hoja yake ni kweli vinginevyo arejee maktaba kutafuta ukweli.

  Kwa mtazamo wangu ambao si lazima umpendeze kila mtu, kafulila hafai kuwa mbunge, hana vision, ni kasuku aliyekariri mistari. Siwezi kumfananisha kafulila na J.Mtatiro, J.Mnyika, Z.kabwe, H.mdee. kwa uchache. Katika nchi kama Tz huwezi kuwa na agenda bila kutaja afya! Kafulila kabeba ilani ya chama chake bila kujua matatizo ya watu wake. Ninachoweza kumsifu kafulila ni uwezo wa kuongea kama mwanasiasa kwa mikono na misemo. Ningependa sana kuwa na wabunge wapinzani wengi,lakini si akina Kasuku Kafulila! Ni mtazamo wangu.
   
 4. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #4
  Oct 1, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Kafulila amekuja na agenda nne
  1: Elimu
  2: Maendeleo vijijini
  3: Muafaka wa Kitaifa
  4: Miundo Mbinu

  ambapo anataka kutuambia kuwa kila kisichoanishwa kinaingia kwenye Elimu (afya itaboreka kwa kuboresha elimu pekee?!)
   
 5. makoye2009

  makoye2009 JF-Expert Member

  #5
  Oct 1, 2010
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,646
  Likes Received: 500
  Trophy Points: 280
  Kafulila hana sera yenye mashiko na kwa maana nyingine NCCR hawana sera kuanzia mgombea wao wa Urais Hashim Rungwe.
  NCCR na hasa ukimsilikiza mwenyekiti wao wa Taifa Mbatia anaonekana kama ni kibaraka wa CCM.

  Mbatia mara nyingi nilishamsikia akiwabeza wapinzani wenzake kama CHADEMA,CUF na vyama vingine hasa zenye upinzani wa dhati.
  Kama Kafulila angelikuwa kwenye chama cha cha CHADEMA au CUF watu wangempa kura kwa wingi.
   
 6. N

  Nasolwa JF-Expert Member

  #6
  Oct 1, 2010
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,830
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Kafulila KAFULIA
   
 7. Technician

  Technician JF-Expert Member

  #7
  Oct 1, 2010
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 843
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Thanks for the video i requested.
   
 8. M

  Mkulima JF-Expert Member

  #8
  Oct 1, 2010
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 698
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 60
  Naona Kafulila kanolewa vizuri sana na Zitto na anaelewa anaongelea nini, amefanya homework yake na ana data.

  Ila hao wawili watagawana kura na kuifanya CCM ishinde kirahisi.
   
Loading...