KWELI Video hii ya Tai na Duma imetengenezwa kwa AI

KWELI Video hii ya Tai na Duma imetengenezwa kwa AI

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Source #1
View Source #1
Mdau

Je, unaweza kutofautisha video halisi dhidi ya zile zilizotengenezwa kwa Teknolojia ya Akili Unde?

Mtu mmoja alichapisha video hii hapa chini katika mtandao wake wa kijamii na kueleza kuwa tukio hilo limetokea Afrika. Kipande cha video ambacho kimeibua maswali mengi kwa waliyoiona kuhoji uhalisia wake.

Tushirikishe vigezo ama nyenzo ulizotumia kubaini uhalisia.
1753341284739.png

 
Tunachokijua
Madai

Mtumiaji mmoja wa wa mtandao wa kijamii wa X amechapisha taarifa iliyoambatana na video na kisha kueleza kuwa tukio hilo limetoa barani Afrika.

Kipande hicho cha video kinamuonesha Tai akiwa amemchukua duma mdogo na baadaye Tai huyo kushambuliwa na Duma mkubwa huku watalii wakiwa wanamuangalia.

Uhalisia wa video hiyo

JamiiCheck imehakiki video hiyo na kubaini kuwa imetengenezwa kwa teknolojia ya Akili Unde.

Ufuatiliaji umebaini kuwa video hiyo ina matukio yanayokosa uhalisia ambayo yanadhihirirsha kuwa si video halisi.

Mathalani tukio la duma mdogo aliyenyanyuliwa juu na kubadilika kuwa kiumbe kingine. Rejelea pia tukio la Tai kung'atwa shingo lakini hakuna alama yoyote ya makovu ama damu ingawa manyoya yake ya shingoni ni meupe.

Aidha Tai huyo mwenye kichwa (Bald Eagle) cheupe asili yake siyo barani Afrika bali ni Tai mashuhuri huko Amerika ya Kusini hivyo kuhusianisha tukio hilo na bara la Afrika pia ni upotoshaji.
Back
Top Bottom