Video: Compare and Contrast

Video: Compare and Contrast

HT

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2011
Posts
1,897
Reaction score
414
Hope for fair Comments and no abusive language!

Mwl. J.K. Nyerere

Dr. J.M. Kikwete

Text:

Sijafanikiwa kupata Text ya Mwalimu but nimepata ya Dr. Jakaya (Full Text hapa)

Uhusiano wa Waislamu na Wakristo
Ndugu Wananchi;Jambo la pili ninalopanga kulizungumzia siku ya leo ni uhusiano wa Wakristo na Waislamu hapa nchini. Kwa miezi kadhaa sasa tangu mwaka wa jana kumekuwepo na matukio kadhaa yanayosababisha mifarakano na kupandikiza chuki baina ya waumini wa dini ya Kikristo na Kiislamu. Matukio ya kauli na vitendo vya kudharau dini za wengine, kunajisi vitabu vitakatifu vya dini hizo, kuchoma moto nyumba za ibada na mzozo kuhusu nani achinje. Kumekuwepo na matumizi mabaya ya radio na simu za mkononi na mifumo mingine ya mawasiliano iliyoeneza maneno na ujumbe wa chuki na vitisho kwa waumini na viongozi wa dini zetu hizi kubwa hapa nchini. Kauli na matendo hayo, katika baadhi ya maeneo yamekuwa chanzo cha uhasama na magomvi baina ya waumini na hatimaye kusababisha vifo kama ilivyotokea Buseresere Mkoani Geita na Beit-el-Ras, Zanzibar.Ndugu zangu; Watanzania hatujawahi kuwa hivi, kumetokea nini? Miaka yote Watanzania ni watu tunaotambua na kuheshimu tofauti za dini zetu mbalimbali tunazoabudu. Watanzania ni waelewa na kwa ajili hiyo tumekuwa tunavumiliana kwa tofauti zetu na ndiyo maana tumekuwa tunaishi pamoja kidugu, kwa umoja na kushirikiana kwa mambo yote yanayotuhusu maishani isipokuwa wakati kila mmoja anapoingia kwenye nyumba ya ibada kumuomba Mola kwa misingi na taratibu ya dini yake.Watanzania wa dini zote na makabila tofauti wanaishi nyumba moja, wanasoma pamoja, wanafanya kazi pamoja kwa udugu, upendo, umoja na ushirikiano. Kuna koo na familia zenye watu wa dini tofauti, wengine Waislamu na wengine Wakristo. Wapo Waislamu na Wakristo wameoana, wamezaa na wamejukuu na kila mmoja amebakia kuwa mfuasi wa dini yake. Wapo pia ambao hawakuoa lakini wamezaa watoto na wanashirikiana kulea watoto wao. Hayo ndiyo maisha ya Watanzania na hiyo ndiyo Tanzania yenye amani na utulivu tuliyozaliwa, kukua na kuishi. Nawasihi sana Watanzania wenzangu, tuienzi na kuidumisha tunu hii waliyotujengea mababu zetu.

Ndugu Wananchi;
Kuna wenzetu kwa sababu wanazozijua wao na kwa manufaa wanayoyajua wao wanataka kutuvurugia nchi yetu hii nzuri. Tusiwape nafasi wachochezi hawa kwani hawatutakii mema na wala hawazitakii mema dini zetu na nchi yetu. Sisi katika Serikali hatutasita kuwachukulia hatua wale wote wanaochochea chuki za kidini, wanaodharau vitabu vitakatifu vya dini nyingine na wanaokejeli dini nyingine.Nimewakumbusha Polisi na mamlaka husika kote nchini wasifanye ajizi kwenye matukio ya namna hiyo. Wawachukulie hatua stahiki wale wote wanaohusika. Nimewataka wazingatie msemo wa Kiswahili usemao:"Ajizi nyumba ya njaa". Wachochezi wa mifarakano na chuki za kidini wasipodhibitiwa ipasavyo wataleta maafa kwa Watanzania wasiokuwa na hatia. Nimewakumbusha Wakuu wa Wilaya na Mikoa kama walinzi wa amani wa maeneo yao ya uongozi, watimize ipasavyo wajibu wao. Pia nimewataka Polisi wakamilishe mapema upelelezi wa makosa ya vurugu za kidini na wahusika wafikishwe haraka kwenye vyombo vya sheria ili iwe fundisho kwa wengine.

Ndugu Wananchi;
Naendelea kuwasiliana na viongozi wa dini kuzungumza nao juu ya wajibu wao maalum wa kuhakikisha kuwa wafuasi wao hawawi chanzo au sehemu ya tatizo na mifarakano miongoni mwa waumini wa dini mbalimbali nchini. Hali kadhalika naitumia nafasi hiyo kuwakumbusha umuhimu wa kuzungumza na wenzao wa upande mwingine kutatua tofauti au matatizo yanayoathiri uhusiano mwema baina yao.Ndugu Wananchi;Kuna msemo maarufu usemao: "Mjenga nchi ni mwananchi na mbomoa nchi ni mwananchi". Naomba tuwe wajenga nchi na kamwe tusikubali kuwa wabomoa nchi. Hivi tukiibomoa nchi yetu tutakwenda wapi? Tutaishi wapi? Tusikubali kugeuka wakimbizi ndani ya nchi au nje ya nchi yetu.Kwa mara nyingine tena, napenda kutumia nafasi hii kuwapa mkono wa pole makanisa, familia, ndugu na jamaa wote wa Mchungaji Kachila na Padri Mushi. Sote tunafahamu machungu waliyonayo kwa kuondokewa na wapendwa wao. Serikali na wapenda amani wote nchini wapo pamoja nanyi katika kipindi hiki kugumu. Vile vile natoa rambirambi zangu nyingi kwa waumini wote wa Kanisa la Pentekoste Assemblies of God na Kanisa Katoliki Tanzania kwa kuondolewa ghafla na viongozi wao. Tuzidi kumwomba Mwenyezi Mungu azipumzishe kwa amani roho za viongozi wetu. Amin.
 
Last edited by a moderator:
Hapo hamna comparison hata moja. Ni contrast tupu. Mf. Mwalimu haukua legelege, hakua na udini alikemea jambo lolote na kuchukua hatua stahiki kabla na hata baada ya tukio lililoonekana kuwagawa Watanzania kwa misingi ya Udini, ukabila.Tofauti na ilivyokua kwa Mwalimu siku hizi ni kundekeza siasa za chuki,makundi, kutoa majibu mepesi kwa mambo yanayohatarisha amani ya nchi mfano vurugu za udini mpaka sasa hakuna hatua zozote zilizochukuliwa dhidi ya walioharibu maisha ya viongozi wa dini pamoja na mali ya taasisi za dini hali inayoonyesha kuwa kuna mkono wa ''mtu''. Mwalimu asingeruhusu hali hii iendelee hapa Tanzania kama ilivyo sasa...
 
huyu jjamaa aliniaachaga hoi pale aliposema Zanzibar sasa shwari.........teh teh teh!!! Hivi Zanzibar shwari jamani?

Juzi juzi akaibuka tena akasema Arusha sasa shwari.

Mr president, dont be naive.
 
Kumbe suala la udini linashamiri tunapokuwa na marais waislamu- rejea mwembe chai ilikuwa mwaka gani.. rejea kipindi tuliyopo ya Dr. JK,.......rejea hotuba fupi ya rais mtarajiwa kwa chama cha CUF. Prof. Ibrahimu Lipumba, unategemea nini
Kwa kweli ni mawazo ya kipumbavu mtu mzima kutanguliza dini kama kigezo ya kuwa first class person....in the country.
 
we TAAHIRA MAUAJI YA MUEMBECHAI YALIKUWA KIPINDI CHA MKAPA, 1998. DONT MISLEAD.
 
Hapo hamna comparison hata moja. Ni contrast tupu. Mf. Mwalimu haukua legelege, hakua na udini alikemea jambo lolote na kuchukua hatua stahiki kabla na hata baada ya tukio lililoonekana kuwagawa Watanzania kwa misingi ya Udini, ukabila.Tofauti na ilivyokua kwa Mwalimu siku hizi ni kundekeza siasa za chuki,makundi, kutoa majibu mepesi kwa mambo yanayohatarisha amani ya nchi mfano vurugu za udini mpaka sasa hakuna hatua zozote zilizochukuliwa dhidi ya walioharibu maisha ya viongozi wa dini pamoja na mali ya taasisi za dini hali inayoonyesha kuwa kuna mkono wa ''mtu''. Mwalimu asingeruhusu hali hii iendelee hapa Tanzania kama ilivyo sasa...

WOTE niwakopaji wazuri, mfano nyerere alienda kukopa mpaka nchi iliyokuwa masikini kipindi hicho, yaani Brazil, japokuwa hatujui hela hizo zilifanya nini? Afadhali za Kikwete tunaona hata barabara.
 
Kumbe suala la udini linashamiri tunapokuwa na marais waislamu- rejea mwembe chai ilikuwa mwaka gani.. rejea kipindi tuliyopo ya Dr. JK,.......rejea hotuba fupi ya rais mtarajiwa kwa chama cha CUF. Prof. Ibrahimu Lipumba, unategemea nini
Kwa kweli ni mawazo ya kipumbavu mtu mzima kutanguliza dini kama kigezo ya kuwa first class person....in the country.

Mwembechai - Rais alikuwa MWINYI Nakumbuka VIZURI saana sababu NILIKUWA na NYUMBA maeneo hayo niliiacha na ndio Mwanzo wangu ulionifanya niihame NCHI yangu niliyoipenda kwa ARI na MOYO.. CCM ILINILEA not now not now!!!
 
WOTE niwakopaji wazuri, mfano nyerere alienda kukopa mpaka nchi iliyokuwa masikini kipindi hicho, yaani Brazil, japokuwa hatujui hela hizo zilifanya nini? Afadhali za Kikwete tunaona hata barabara.

Nimekuambia na ninarudia WAKATI wa NYERERE BRAZIL ilikuwa inatawaliwa na MADIKTETA wa KIJESHI; Nyerere alikuwa hajihusishi na MADIKTETA

Na sababu kubwa iliyosababisha amwachie Urais Rais Mwinyi 1985 pia ni yeye kutokutaka KUKOPA kwa Masharti Magumu WORLD BANK na IMF... ikabidi aachie ngazi...

Kumbuka sana --- NYERERE enzi hizo alikuwa PRO REVULUTION - PRO PALESTINE sio sasa hivi KIKWETE haongelei hata Mapinduzi yao...

cc cj21125
 
Kikwete aanze na huyu ndugu yetu aliyeshindwa siasa, eti anajiita rais mtarajiwa sijui, muda wote kuzunguka na kina sheikh ponda msikitini akitafuta huruma ya ndugu zetu waislamu!
 
Mbona unalinganisha Mlima na Kichuguu, Ukisikiliza Hotuba hizo 2 na Body Language, unapata jibu.

Hope for fair Comments and no abusive language!

Mwl. J.K. Nyerere

Dr. J.M. Kikwete

Text:

Sijafanikiwa kupata Text ya Mwalimu but nimepata ya Dr. Jakaya (Full Text hapa)

Uhusiano wa Waislamu na Wakristo
Ndugu Wananchi;Jambo la pili ninalopanga kulizungumzia siku ya leo ni uhusiano wa Wakristo na Waislamu hapa nchini. Kwa miezi kadhaa sasa tangu mwaka wa jana kumekuwepo na matukio kadhaa yanayosababisha mifarakano na kupandikiza chuki baina ya waumini wa dini ya Kikristo na Kiislamu. Matukio ya kauli na vitendo vya kudharau dini za wengine, kunajisi vitabu vitakatifu vya dini hizo, kuchoma moto nyumba za ibada na mzozo kuhusu nani achinje. Kumekuwepo na matumizi mabaya ya radio na simu za mkononi na mifumo mingine ya mawasiliano iliyoeneza maneno na ujumbe wa chuki na vitisho kwa waumini na viongozi wa dini zetu hizi kubwa hapa nchini. Kauli na matendo hayo, katika baadhi ya maeneo yamekuwa chanzo cha uhasama na magomvi baina ya waumini na hatimaye kusababisha vifo kama ilivyotokea Buseresere Mkoani Geita na Beit-el-Ras, Zanzibar.Ndugu zangu; Watanzania hatujawahi kuwa hivi, kumetokea nini? Miaka yote Watanzania ni watu tunaotambua na kuheshimu tofauti za dini zetu mbalimbali tunazoabudu. Watanzania ni waelewa na kwa ajili hiyo tumekuwa tunavumiliana kwa tofauti zetu na ndiyo maana tumekuwa tunaishi pamoja kidugu, kwa umoja na kushirikiana kwa mambo yote yanayotuhusu maishani isipokuwa wakati kila mmoja anapoingia kwenye nyumba ya ibada kumuomba Mola kwa misingi na taratibu ya dini yake.Watanzania wa dini zote na makabila tofauti wanaishi nyumba moja, wanasoma pamoja, wanafanya kazi pamoja kwa udugu, upendo, umoja na ushirikiano. Kuna koo na familia zenye watu wa dini tofauti, wengine Waislamu na wengine Wakristo. Wapo Waislamu na Wakristo wameoana, wamezaa na wamejukuu na kila mmoja amebakia kuwa mfuasi wa dini yake. Wapo pia ambao hawakuoa lakini wamezaa watoto na wanashirikiana kulea watoto wao. Hayo ndiyo maisha ya Watanzania na hiyo ndiyo Tanzania yenye amani na utulivu tuliyozaliwa, kukua na kuishi. Nawasihi sana Watanzania wenzangu, tuienzi na kuidumisha tunu hii waliyotujengea mababu zetu.

Ndugu Wananchi;
Kuna wenzetu kwa sababu wanazozijua wao na kwa manufaa wanayoyajua wao wanataka kutuvurugia nchi yetu hii nzuri. Tusiwape nafasi wachochezi hawa kwani hawatutakii mema na wala hawazitakii mema dini zetu na nchi yetu. Sisi katika Serikali hatutasita kuwachukulia hatua wale wote wanaochochea chuki za kidini, wanaodharau vitabu vitakatifu vya dini nyingine na wanaokejeli dini nyingine.Nimewakumbusha Polisi na mamlaka husika kote nchini wasifanye ajizi kwenye matukio ya namna hiyo. Wawachukulie hatua stahiki wale wote wanaohusika. Nimewataka wazingatie msemo wa Kiswahili usemao:“Ajizi nyumba ya njaa”. Wachochezi wa mifarakano na chuki za kidini wasipodhibitiwa ipasavyo wataleta maafa kwa Watanzania wasiokuwa na hatia. Nimewakumbusha Wakuu wa Wilaya na Mikoa kama walinzi wa amani wa maeneo yao ya uongozi, watimize ipasavyo wajibu wao. Pia nimewataka Polisi wakamilishe mapema upelelezi wa makosa ya vurugu za kidini na wahusika wafikishwe haraka kwenye vyombo vya sheria ili iwe fundisho kwa wengine.

Ndugu Wananchi;
Naendelea kuwasiliana na viongozi wa dini kuzungumza nao juu ya wajibu wao maalum wa kuhakikisha kuwa wafuasi wao hawawi chanzo au sehemu ya tatizo na mifarakano miongoni mwa waumini wa dini mbalimbali nchini. Hali kadhalika naitumia nafasi hiyo kuwakumbusha umuhimu wa kuzungumza na wenzao wa upande mwingine kutatua tofauti au matatizo yanayoathiri uhusiano mwema baina yao.Ndugu Wananchi;Kuna msemo maarufu usemao: “Mjenga nchi ni mwananchi na mbomoa nchi ni mwananchi”. Naomba tuwe wajenga nchi na kamwe tusikubali kuwa wabomoa nchi. Hivi tukiibomoa nchi yetu tutakwenda wapi? Tutaishi wapi? Tusikubali kugeuka wakimbizi ndani ya nchi au nje ya nchi yetu.Kwa mara nyingine tena, napenda kutumia nafasi hii kuwapa mkono wa pole makanisa, familia, ndugu na jamaa wote wa Mchungaji Kachila na Padri Mushi. Sote tunafahamu machungu waliyonayo kwa kuondokewa na wapendwa wao. Serikali na wapenda amani wote nchini wapo pamoja nanyi katika kipindi hiki kugumu. Vile vile natoa rambirambi zangu nyingi kwa waumini wote wa Kanisa la Pentekoste Assemblies of God na Kanisa Katoliki Tanzania kwa kuondolewa ghafla na viongozi wao. Tuzidi kumwomba Mwenyezi Mungu azipumzishe kwa amani roho za viongozi wetu. Amin.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom