Habari Wanajanvi.
Leo nina Furaha sana kwani nimefikia malengo niliyojipangia.
nilipanga kutafuta Kura za uhakika zisizopungua 50 zitakazompigia Lowassa na UKAWA.
Nilianza na wafanya kazi wenzangu wasioupongua 25 kati ya hawa 20 hawakunipa tabu kuwapata.
Watano kati yao walikua wana CCM kiukweli lakini nashukuru Mungu mpaka leo wote nimewatia Mkononi.
Kura 25 nyingine nimezipata mitaani kwenye Vijiwe mbalimbali vikiwemo vijiwe vitatu vya CCM.
Haikua kazi raisi lakini kwa kusukumwa na roho ya mabadiliko nimeweza kutimiza lengo langu.
Kwasababu nimetimiza lengo mapema nitaongeza lengo na kufikia angalau kura 100.
Kura hizi 50 natarajia kuzipata kupitia Mitandao ya Kijamii ikiwepo Jamii Forum.
Jiandaeni kwa Episode yangu Ijayo.
Mabadiliko Yanawezekana Tafuta Kura na Tupe Riport.