Vichaa ndani ya ndege

Vichaa ndani ya ndege

charger

JF-Expert Member
Joined
Nov 21, 2010
Posts
2,320
Reaction score
1,373
Vichaa kutoka asylum moja wanapelekwa nchi jirani kwa ndege kucheza mechi ya kirafiki na vichaa wenzao huko.

Kwenye ndege hakukaliki,mara huyu kamrushia mwenzie mpira,mara huyu ka inflate life jacket basi tabu tu.

Kocha kajaribu kuwatuliza ikashindikana,lakini kuna kichaa mmoja yeye alikuwa ametulia anasoma gazeti.Kocha kachoka kaamua kwenda seat ya mbele akalala.

Mara kocha kustuka anaona ukimya umetawala kwenye cabin,akaamua ageuke nyuma.Huko nyuma kamwona yule kichaa aliyekuwa anasoma gazeti.Ikawa kama hivi

KOCHA:We! wenzio wakwapi?

KICHAA:Nimeona wanakusumbua nimefungua mlango nikawatupia mpira wakachezee nje.
 
Sawa tu, huyu atakuwa keshapona. Usumbufu ukizidi watoe nje! Teh
 
Hii sio jokes kabisa mkuu huwezi kufungua mlango wa ndege ikiwa angani na ikafika salama
 
Binafsi nimeipenda, sababu inaitwa "joke". Bila kucheka kidogo? Itakuwaje na mapressure ya ugumu wa maisha?? Big up sana mtu wangu. Endelea kuturushia jokes tuongeze umri wa kuishi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom