Vichaa Mirembe

Elisha Ray

JF-Expert Member
Joined
Mar 19, 2012
Posts
323
Reaction score
94
Siku moja daktari wa wodi ya vichaa pale Mirembe hosp aliamua kwenda kuwapima wagonjwa wake aone nani amepona ili awaruhusu kutoka hospitali. Alipofika wodini akafunga mlango kisha akaenda upande mwingine wa wodi kwenye ukuta akachora mlango. Akawaambia kama wamepona basi watoke waende makwao. Basi wawili wakaanza kugombania kutoka katika ule mlango uliochorwa na mwingine alikuwa amekaa akiwaangalia huku akiwacheka. Kuona hivyo daktari akafarijika na akahisi 'huyu ndo kapona!' Akamuuliza 'we vipi mbona hutaki kuondoka?' Yule mgonjwa akamwambia huku akicheka 'wale vichaa kweli dokta, yani hawatapita pale mimi ndo nina ufunguo hadi niwafungulie..!!' Dokta akazimia.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…