Vibaka wanavyoitesa mitaa ya Nyakasa, Ilemela mkoani Mwanza

Vibaka wanavyoitesa mitaa ya Nyakasa, Ilemela mkoani Mwanza

Magha

Member
Joined
Jan 29, 2019
Posts
10
Reaction score
11
Imekuwa kama ni kawaida sasa katika mitaa ya Nyasaka wilaya Ilemela mkoa wa Mwanza kuzungumuzia vibaka kwani hakuna ambaye hawajamwingilia katika maeneo hayo

Huku uongozi ukionekana kutochukua muhimu mkubwa katika suala hilo.

Tunaomba Mbunge wetu wa Ilemela alione hili kwani vibaka wanataka kuharibu taswira ya Nyasaka ilivyo na kuwa kama makazi yao.
 
Mbunge wa kazi gani hapo mkuu? Hiyo nyasaka nikajua ipo Dar....uweni tu mkuu kwa kuanzia mfano kesho kukipambazuka vibaka 10 mmewapiga viberiti watapotea wote
 
Mbunge Hakuna Ilemela, Kama Watu wanataifishwa Nyumba na ardhi na amekaa kimya na taarifa anazo Leo atashughulika na vibaka???? Labda kwa kuwa kuna chaguzi za serikali ya mtaa...

Sent using Jamii Forums mobile app
ana shida gani wakati anajua uchaguzi atapita piga ua magufuli ndio mchaguaji ndio tume ndio mpiga kura.. kwa nini asijijenge tu na familia yake
 
Imekuwa kama ni kawaida sasa katika mitaa ya Nyasaka wilaya Ilemela mkoa wa Mwanza kuzungumuzia vibaka kwani hakuna ambaye hawajamwingilia katika maeneo hayo

Huku uongonzi ukionekana kutochukua muhimu mkubwa katika swala hilo. Tunaomba Mbunge wetu wa Ilemela alione hili kwan vibaka wanataka kuhalibu taswila ya nyasaka ilivyo .na kuwa kama makazi yao
Msukuma hawezi kuniibia mm. Huko hakuna vibaka
 
Nyie mjiorganize muweke kikundi cha ulinzi muwale Target hao vibaka Mbunge awanyie kila kitu sasa hivi yupo mbunge anapiga hela Tatizo watanzania tunawapa kipaumbele wanasiasa huku wenyewe wanaangalia matumbo yao , Hiyo ni fursa kabisa ningekuwa huko naandaa na kampuni ya ulinzi kila kaya wanalipa shilingi2000 kwa Mwezi Hela yote hiyo ,Changamkia Fursa Hiyo Mkuu,Matatizo ndio Fursa upige hela achana nawanasiasa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Zamani nilikuwa nina roho ya huruma sana nionapo mwizi akishushiwa kipigo kitakatifu, lakini kwa sasa nauwezo wa kumkabili mwizi pekeyangu ni nikamchinja kabisa na nikamkata kata kama samaki...tangu siku nilipokuwa na njaa nikaomba deiwaka ya hapo buja kwa mshkaji kufika kipande cha ubena pale tena sa kumi na moja kasoro asubuhi, wakadandia gari, wakakata sili na king'amuzi na mzigo wakaugusa bila mimi kujua...usumbufu nilioupata nilitamani ningezaliwa somalia
 
Imekuwa kama ni kawaida sasa katika mitaa ya Nyasaka wilaya Ilemela mkoa wa Mwanza kuzungumuzia vibaka kwani hakuna ambaye hawajamwingilia katika maeneo hayo
Kuna jamaa na marafiki nimewasiliana nao huko, hujawa mkweli hapo kwenye bluu mkuu.
 
Nyie si ndio mnajiita wanaume wa mkoani! Mnalia na vibaka? Siku hizi huku Dar tuna ulinzi shirikishi tena si sungusungu bali tunalinda wenyewe kwa zamu.

Huku bunju kuna maeneo ikifika saa tano usipite kama huna maelezo ya kueleweka na kufahamika. Tumekubaliana mtu akisikia chochote tunashtuana wote kwa simu alafu tunatoka kwa pamoja, mwenye mguu wa kuku, panga, mkuki, upinde n.k kupitia njia tofauti hadi assembly point tulipokubaliana.

Kutegemea polisi kwa uchache wao na changamoto zingine ni ujinga. Pangeni mikakati wenyewe. Siku mkikamata kibaka mnamfanya mfano.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom