Viashiria hivi ni vibaya - Wahusika fanyieni kazi

infinite_

Senior Member
Sep 10, 2013
127
125
1. Kwa miaka yote iliyopita ukienda mahali popote pale duniani na ukisema mbele za watu kwamba umetokea Tanzania basi ni neno moja tu utokea mawazoni mwao haraka haraka kwamba Tanzania ni nchi ya Amani, upendo, yenye demokrasia na ni nchi ya kuigwa barani Afrika na duniani kote.

2. Amani ni hali ya raha na usalama bila ugomvi; kwa ufupi ni kinyume cha fujo au vita. Vile vile Demokrasia ni mfumo wa serikali ambapo wananchi wote ni sawa mbele ya sheria na wanashiriki kwa namna moja au nyingine katika kufanya maamuzi ya kitaifa.

3. Mkufunzi wa maswala ya Kiusalama anae julikana kama Walter Dorn alishawahi kusema yafuatayo "The world can never be at peace unless people have security in their daily lives" aliendelea kusema mengi sana yakiwemo maswala ya Political security kwamba Taifa lolote duniani likicheza na maswala haya (including Human Security) basi mjue mnapeleka mahali pabaya mataifa yenu na ni jukumu la vyanzo vya Ulinzi na usalama kutambua indicators hizi mapema na kuziondoa haraka sana. Akaendelea kusema, kama mkishindwa kuziondoa indicators hizo mapema basi ugeuka threats kwa Usalama wa Mataifa yenu.

4a. Hivi karibuni kumetokea matukio/tetesi za watu kutekwa, mara kukamatwa, wengine kutishiwa silaha hadharani, vituo vya Radio/TV kuvamiwa na wengineo kupotea gafla hapa nchini huku jamii ikikosa uhuru wa kuzungumza na kuingiwa na uwoga mkubwa.

4b. Napenda kujiuliza ni nani anayefanya matendo yote hayo?? Kwanini yote hayo yanatokea nchini hivi sasa?? Ni kikundi gani kinafanya matendo yote hayo?? Ni kwa faida ya nani au kwa faida ipi?? Je ni kikundi cha ndani ya nchi? Au ni kikundi toka nje ya nchi kilikuwa as a sleeper cell na hivi sasa kimekuwa activated?? Je inawezekana kuna kikundi kinataka kuipeleka Tanzania mahali pabaya? Je yanayo tokea hivi sasa ni mikakati ya kuandaa watu kimtazamo kwenda huko wanapotaka kutupeleka? Maswali haya yote ni mawazo huru kwa Raia yoyote anaye lipenda Taifa lake na ni haki yangu ya msingi kujiuliza.

5. Matendo yote hayo yanayotokea hivi sasa yanaleta sura mpya ya Tanzania kwenda kwenye Mataifa mengineyo (International Community), Sura ambayo ni mbaya mbaya sana na vitu ambavyo SIO sifa ya Tanzania na wala SIO sifa ya Watanzania, Matukio yote hayo tulizoea kuyasikia kutokea kwenye Mataifa mengine na matukio haya ndio yamenipa maswali mengi mimi kujiuliza.

6a. Leo sipendi kusema sana ila ningewaomba sana sana DGIS Kipilimba, DDGIS.Msalika, Afande CDF Mabeyo, COS.Mwakibolwa, IGP Mangu, DIGP Kaniki pamoja na vijana wenu wote walio chini yenu (including the whole intelligence community); Kumbukeni mliapa kuitetea Katiba na kulinda Taifa la Tanzania na watu wake kwa nguvu zenu zote basi nawaomba mshirikiane kwa pamoja kuondoa hizi indicators na kuzitokomeza kwa gharama yoyote.

6b. Mkimaliza kuzitokomeza hizo indicators za sasa; Please nawaomba tena myafanyie kazi maneno ya mwisho ya Mch.Mtikila wiki chache kabla hajafariki.

7. Tanzania SIO ya kizazi cha sasa peke yake tu bali Tanzania pia ni ya kizazi kijacho na kijacho na ni jukumu letu Watanzania wote kuiweka nchi yetu salama siku zote na ni jukumu letu kuilinda Tanzania ndani na nje dhidi ya adui yoyote kwa gharama zozote wakati wowote.

Wengine tumeshazeeka kwa sasa tusingependa kuiona Tanzania ikipotea au kuelekea inapo elekea. Tuilinde Tanzania na watu wake, Wote Tukatae indicators hizi mbaya za Sasa kwa faida ya kizazi kijacho.

Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika.
----------------------------------------------

Mimi SIO Mwanachama wa Chama chochote cha Siasa, Sina upande wowote ule, Tanzania ndio kila kitu kwangu. Naomba tutoe maoni ya kujenga kwa manufaa ya Tanzania yetu na SIO maoni ya Kisiasa.
 
Mkuu ,
Maelezo mazuri yanajitosheleza,ila subiri waje wapotoshaji.
 
Back
Top Bottom