Verkys vs Luambo. Nani zaidi?

Ziroseventytwo

JF-Expert Member
Mar 27, 2011
8,502
15,357
Nimesikiliza miziki/nyimbo zao nikagundua hawa jamaa walikuwa wakali sana.

Franco Luambo Makiadi akiwa na TP OK JAZZ alirekodi miziki mingi iliyotamba si Africa tu bali mpaka bara ulaya. Alifanikiwa kupiga muziki akiwashirikisha baadi ya wanamuziki nguli (si wasanii) wakiwemo Tabu Ley roucherou, Nyiboma Mwandido Sam Mangwana na wengine wengi. Anatajwa kuwa ndio mwanamuziki bora kabisa kutoke nchini congo zamani zaire. Moja ya vibao vyake vilivyompatia umaarufu ni pamoja na Mario.

Kyambomana Matete Yazelambongo maarufu Verkys yeye alikuwa anamiliki bendi zaidi ya 3. mojawapo ni orchestra veve. Hii bendi nayo ilitamba miaka ile ya mwisho ya 70. hawa jamaa walikuwa ni nourma linapokuja swala la alla za upepo. Verkys na veve walitamba na vibao vyao vilivyotikisa na vinavyoendelea kutikisa. Mikolo mileki mingi, Baluti, ndowe na vingine kibao.

Kwangu mimi verkys ndio alikuwa mkali kuliko Lwambo Makiadi.

Tusemezane.
 
Back
Top Bottom