Venezuela yafunga mpaka wake na Brazil

Venezuela yafunga mpaka wake na Brazil

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,881
Reaction score
6,374
Rais wa Venezuela Nicolas Maduro ameamuru kufungwa kwa mpaka wa kusini mwa nchi yake, ambao unaitenganisha na Brazil. Hatua hii imeanza kutumika usiku wa kuamkia leo (saa za Venezuela).

Uamuzi huu umechukuliwa kutokana na kile rais wa Venezuela amekiita "uchokozi" kutoka serikali ya mrengo wakulia ya Brazil.

Venezuela pia inafuatilia kwa karibu hali kwenye mpaka wake na Colombia, rais wa Venezuela ameongeza.

"Sitaki kuchukuwa aina hiyo ya maamuzi, lakini ninajifunza uwezekano wa kuchukuwa hatua kama hiyo, kufunga mpaka wa Venezuela na Colombia," amesema Maduro.

Colombia na Brazil wamejiunga na upinzani wa mrengo wa kulia nchini Venezuela kwa msimamo wao mmoja wa kumtimuwa rais Maduro na chama ccha Kisoshalisti cha PSUV.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wameufunga kwasababu marekani inataka kuingiza maroli ya misaada kwa nguvu.
 
... huyo Maduro naye hamnazo! Yaani anagombana na kila taifa except mabwana zake Urusi na kwa mbaali China!
 
Back
Top Bottom