WAPENDANAO KUZAWADIWA
Kampuni ya Push Media Mobile itatoa zawadi ya gari aina ya Vitz lenye thamani ya sh8 milioni kwa mshindi wa kampeni maalum ya kuadhimisha sikukuu ya wapendanao Valentine Day itakayoadhimishwa Februari 14.
Hayo yalisemwa na Meneja Mauzo na Masoko wa Push Media Mobile, Rodney Rugambo katika uzinduzi wa kampeni hiyo.
Rugambo alisema kuwa wameamua kutoa zawadi kubwa hiyo ili kuwafanya wapendanao wengi kushiriki na kupata nafasi ya kushinda. Alisema kuwa ili kuingia katika droo ya shindano hilo, unatakiwa kutuma neno Penzi kwenda namba 15678 na kujibu maswali mbalimbali yahusiyo masuala ya mapenzi na mahusiano, na siku ya Valentine yenyewe.
Hii ni promosheni ya kwanza kubwa hapa nchini Tanzania na mshindi kujishindia gari, lengo kubwa ni kutoa ufahamu kuhusiana na sikukuu ya wapendanao na vilevile kuwazawadia wadau wao kwa kushiriki katika shughuli zao za ujenzi wa taifa, alisema Rugambo.
Alisema kuwa mbali ya zawadi hizo, washiriki wa promosheni hiyo pia watapata nafasi ya kushinda kompyuta (Laptop) aina ya HP yenye thamani ya sh1.5 milioni, simu aina ya Blackberry Curve yenye thamani ya sh500,000 na Home Theartre yenye thamani ya sh400,000.
Source by; Mwananchi.