Uzuri wa evelyne wa burkinafaso

Uzuri wa evelyne wa burkinafaso

LIKUD

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2012
Posts
19,899
Reaction score
37,699
Mnamo mwaka 1993. Mwanamuziki kutoka DRC , Aurlus Mabele, na bendi yake ya LOKETO, walitoa wimbo ujulikanao kama EVELYNE.." Baadhi ya maneno yanayo patikana katika wimbo huo ni pamoja na :

" Amsiba luwe Amsimba Luwe Lobolobo, Ambonge Luwe Lubo Lubo"...Kiitikikio kinaimbwa " Evelina Evelina evelina, evelina pike yaya Burkinafaso ". Sina uhakika kama maneno haya nimeyaandika kwa usahihi...Nilikuwa ninaupenda sana huu wimbo and still bado ninaupenda hadi leo, hii but sielewi alicho kuwa anakiimba Aurus Mabele though nina guess ameimba kumsifia msichana aitwaye Eveline ambaye anaishi Burkinafaso...

Kuhusu chanzo cha Aurus Mabele kuimba wimbo huo, kuna jamaa aliwahi kutuambia Aurus Mabele aliimba wimbo huo kama zawadi kwa mpenzi wake aitwaye Evelina ambaye walikutana Burkinafaso. Anasema Aurus Mabele alivyo kuwa ameenda kufanya show Wagadugu, alikutana na huyo msichana evelina na kutokea kumpenda sana, wakaanzisha uhusiano wa kimapenzi. Jamaa akamwambia, nikirudi Kinshasa ( Au Paris? ),

nitakusurprise na zawadi. Kweli jamaa alivyo rejea Kinshasa ( Paris ?) akatoa wimbo huo uitwao Evelina...Kuna ukweli wowote kuhusu maelezo ya huyu jamaa? Kuna mtu anaye jua kuhusu maana ya huu wimbo na chanzo cha Aurus Mabee kutoa wimbo huu?. Tufahamishane wadau.


Click here to listen the song : Aurlus Mabele - Evelyne - YouTube


" Ujasiri wa mkurya huwa unapimwa kwa kuzingatia umbali uliopo kati ya makazi anayo ishi na kilipo choo chake. Kwa kawaida mkurya hawezi kuweka choo cha ndani kwenye nyumba yake kwani hiyo ni sign ya uoga. Choo cha mkurya hujengwa umbali wa kuanzia hatua mia kutoka nyumba yake ilipo. Mtu ambaye choo chake kipo mbali zaidi kutoka nyumba anayo ishi, anachukuliwa kuwa ndio jasiri kuliko wote katika jamii husika "...........Tales From Kurya People.
 
Du hata mimi naupenda sana wimbo huu, hivi hakuna hata mtu anayeweza kuutafsiri kweli?
 
ni moja kati ya nyimbo ambazo zinajenga historia yangu.Kwa kweli kila niusikiapo nakumbuka mbali saaaaana
 
Pepe kalle naye aliimba wimbo wa 'Hidaya' kwa heshima ya dada mmoja wa Kitanzania aliyekutana nae Arusha
 
Aurlus Mabele ni raia na mzaliwa wa Congo Brazzaville.


Sent from my iPhone using JamiiForums app
 
data zaidi jf si ni kisima cha datas
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom