Wizara ya Ardhi
Senior Member
- May 14, 2024
- 133
- 100
Wizara ya Ardhi inakualika kufuatilia uzinduzi rasmi wa Sera ya Taifa ya Ardhi ya Mwaka 1995 (Toleo la Mwaka 2023) kupitia YouTube Live! 📺
📅 Tarehe: 17 Machi 2025
🕘 Muda: Kuanzia saa 2:00 Asubuhi
📍 Mahali: Mubashara kupitia YouTube channel ya Ardhi TV
Mgeni Rasmi: Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan
Jiunge nasi kushuhudia tukio kubwa la Kihistoria Nchini. Usikose!
🔴 Tazama moja kwa moja kupitia
Viongozi pamoja na wageni mbalimbali wakiwa katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete Convention Center jijini Dodoma, 17 Machi,2025 Tayari kwa ajili ya uzinduzi wa Sera ya Taifa ya Ardhi ya Mwaka 1995, Toleo la Mwaka 2023 ambapo Mgeni Rasmi ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Deogratius Ndejembi akisalimiana na Viongozi na Wageni mbalimbali waliofika katika Uzinduzi wa Sera ya Taifa ya Ardhi ya Mwaka 1995 Toleo la Mwaka 2023.
Rais Samia Suluhu Hassan amekabidhi magari 70 pamoja na vitendea kazi vingine kwa ajili ya kuimarisha usimamizi wa ardhi nchini.
Magari na vitendea kazi hivyo yamekabidhiwa kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Deogratius Ndejembi mkoani Dodoma, wakati wa hafla ya uzinduzi wa Sera ya Taifa ya Ardhi ya mwaka 1995 toleo la 2023.
Makabidhiano ya magari pamoja na vitendea kazi hivyo ni sehemu ya jitihada za Serikali katika kuhakikisha kunakuwa na usimamizi bora wa ardhi, huku sera hiyo mpya ikitarajiwa kuleta mabadiliko makubwa katika sekta ya ardhi.
Pia, amezindua rasmi mfumo wa kidigitali wa E-Ardhi kwa utoaji wa hati za umiliki wa ardhi, unaounganisha NIDA, BRELLA, na TRA. Mfumo huo tayari unatumika Dar es Salaam, Dodoma, na Arusha, huku Mbeya ikitarajiwa kuanza hivi karibuni. Baada ya uzinduzi, Rais Samia alikabidhi hati iliyochapishwa kutoka kwenye mfumo huo.
"Hii tukimaliza, itatuwezesha kuchora ramani mpya ya Tanzania, ramani ya mwisho ya Tanzania, ilichorwa mwaka 1978, kwa kiasi kikubwa kuna mabadiliko makubwa hata ukichua tu, Jiji la Dar es Salaam, la mwaka 1978 na leo tofauti, mfumo huu utatuwezesha kutengeneza mipango ya kidijitali,"
"Kwa kutambua changamoto za sekta hiyo, imeongeza bajeti ya Wizara ya Ardhi kutoka shilingi bilioni 133.6 mwaka 2020/21 hadi kufikia shilingi bilioni 171.4 mwaka 2024/25. Hatua hii imewezesha kuimarika kwa usalama wa milki za ardhi, upimaji wa viwanja, mashamba makubwa, pamoja na kupima mipaka ya vijiji. Pia, imefanikisha kufanyika kwa sensa ya majengo kwa mara ya kwanza tangu Tanzania ipate uhuru zaidi ya miaka 60 iliyopita."
📅 Tarehe: 17 Machi 2025
🕘 Muda: Kuanzia saa 2:00 Asubuhi
📍 Mahali: Mubashara kupitia YouTube channel ya Ardhi TV
Mgeni Rasmi: Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan
Jiunge nasi kushuhudia tukio kubwa la Kihistoria Nchini. Usikose!
🔴 Tazama moja kwa moja kupitia
Viongozi pamoja na wageni mbalimbali wakiwa katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete Convention Center jijini Dodoma, 17 Machi,2025 Tayari kwa ajili ya uzinduzi wa Sera ya Taifa ya Ardhi ya Mwaka 1995, Toleo la Mwaka 2023 ambapo Mgeni Rasmi ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Magari na vitendea kazi hivyo yamekabidhiwa kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Deogratius Ndejembi mkoani Dodoma, wakati wa hafla ya uzinduzi wa Sera ya Taifa ya Ardhi ya mwaka 1995 toleo la 2023.
Makabidhiano ya magari pamoja na vitendea kazi hivyo ni sehemu ya jitihada za Serikali katika kuhakikisha kunakuwa na usimamizi bora wa ardhi, huku sera hiyo mpya ikitarajiwa kuleta mabadiliko makubwa katika sekta ya ardhi.
Pia, amezindua rasmi mfumo wa kidigitali wa E-Ardhi kwa utoaji wa hati za umiliki wa ardhi, unaounganisha NIDA, BRELLA, na TRA. Mfumo huo tayari unatumika Dar es Salaam, Dodoma, na Arusha, huku Mbeya ikitarajiwa kuanza hivi karibuni. Baada ya uzinduzi, Rais Samia alikabidhi hati iliyochapishwa kutoka kwenye mfumo huo.
Tanzania yaanza mchakato wa kuchora ramani yake mpya
Rais Samia amesema mara ya mwisho ramani ya Tanzania ilichorwa mwaka 1978 huku vitu vingi vikibadilika."Hii tukimaliza, itatuwezesha kuchora ramani mpya ya Tanzania, ramani ya mwisho ya Tanzania, ilichorwa mwaka 1978, kwa kiasi kikubwa kuna mabadiliko makubwa hata ukichua tu, Jiji la Dar es Salaam, la mwaka 1978 na leo tofauti, mfumo huu utatuwezesha kutengeneza mipango ya kidijitali,"