Uzi wa Mashabiki Butuabutua Qator FIFA WC2022

Ng'wanamangilingili

JF-Expert Member
Aug 22, 2015
5,705
4,739
Aisee kwanza niombe radhi kuna mwamba humu aliletaga uzi wa kunanga kuwa kombe la dunia mwaka huu Qator haina amsha amsha halafu tukampinga, na wengine tukasema apige kimya coz hana ticketi.

Tulitegemea mambo yatakuwa tofauti, sisi wengine ni events chaser, kombe langu la dunia la nne hili kuhudhuria, nilijua nikifika Qator na wana tunaoendaga nao (tuko kama wana 7 hivi huwa tunasave na kujipanga kabisa tukivizia bookings za mwanzo kabisa)kikubwa na kucheki soccer mechi chache na kupiga gambe hasa zone fans, aisee pamepoa, kuna ambience ya mpira imewekwa na teknolojia ya hali ya juu sana kuanzia kufika tu airport ila kitaa ni kama vile tumekuja kulazimisha, sie watu wa gambe kama tuko kifungoni hivi yaani papatu papatu ni nyingi na nina uhakika kama ikiendelea hivi wanywa gambe lazima wakinukishe tu,

hawa waarabu kama walikua hawataki mambo haya wasingekubali kuandaa manake hata uwanjani marufuku kunywa na unless uko VVIP seats tena zilizojificha na huoni mpira hewani. Ilaumiwe FIFA na Platin na wajumbe waliokula mlungula. Najuta najuta.

NB: Walioko huku tupeane updates....,napatika na kwenye makazi ya muda ya kwenye maji huku cruise ships. Kisses are , condoms are available at a high cost.

Sent from my LM-Q730 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom