Uzi maalumu kwaajili ya Ethical Hackers.

Uzi maalumu kwaajili ya Ethical Hackers.

rootadmin

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2018
Posts
349
Reaction score
243
ETHICAL HACKER. ni mjuzi wa masuala ya I.T anae jua jinsi ya kutafuta udhaifu na matobo katika system ambayo ameidhamiria. Yeye anatumia njia na tools zile zile kama anazo tumia Black Hackers isipokuwa hawa Ethical Hackers wao wanavibari maalumu kwaajili ya kufanya uchunguzi huo katika system.

HIZI NI NJIA MAALUMU AMBAZO HAWA ETHICAL HACKERS WANATUMIA KWAAJILI YA KUFANYA UCHUNGUZI WAO KATIKA SYSTEMS.

1) KEYLOGGER

Keylogger ni software ambayo inarekodi kila kitu unacho type kwenye keyboard yako na kusave kitu kinaitwa log katika computer yako. Pia hizi logs huwa zinaweza kuwa na Email yako na passwords zako. inamaana kuwa kila unacho andika kutumia keyboard yako kinakuwa saved kwenye hyo log file.

Keylogger ni sababu mojawapo kwa zile system za online banking kutumia ile chaguo la kuandika kwa kutumia keyboards zao. nadhani kwa watumiaji wa nmb internet banking wanafaham hzi keyboards ambazo zipo katika website yao.

2)FAKE WAP.
Fake Wap ni njia ambayo inatumika kutengeneza Wireless Access Points za uongo ambazo maranyingi huwa ni Open Wifi Networks. Mara tu utakapo jiunga au kuconect na hizi fake wap hackers wanaweza kuaccess data zako zote ulizo nazo katika kifaa chako. So kwakujilinda na hii attact hata ukiconect na Open wifi networks hakikisha kuwa unatumia VPN service.

3) PHISHING
Phishing ni njia mojawapo ya kudukua. ambayo yenyewe mdukuzi hutengeneza website ambayo inafanana kila kitu na website ambayo ni Halisi ambay mdukuaji hutuma link ambayo ameunganisha na hiyo phishing page yake. Maranyingi phishing pages huwa zinataka ulogin mara mlengwa ukisha login username yako na password yako itakuwa saved kwenye database ya huyo hackers. nadhani wale tunao wekeza katika vortex profits mmeelewa hii juzi kati kuna site ilikuwa inazunguka na kututaka tulogin. ile ilikuwa ni mfano wa hii phising.

4)VIRUS, TROJAN , BACKDOORS ETC
Virus au Trojans ni software programs ambazo mara zitakapo kuwa installed kwenye computer au simu yako itaanza kutuma data zako kwa hackers. pia zinaweza hata kufungia mafaili yako na kukudai hela ili ufungue. mfano ile attack iliyo tokea mwaka 2017 mwez wa 5 ambayo iliathiri kampuni kubwa sana duniani.

5)COOKIE THEFT.
katika browser kuna kitu kinaitwa Cookies. cookies zenyewe huwa zinakazi ya kusave au kutunza data zetu muhimu kama browsing history,username na password kutoka sites mbali mbali ambazo umezifungua. Pale hacker atakapo pata mwanya wa kuiba cookie zako anaweza akalogin katika browser kwa kutumia info zako.
 
Back
Top Bottom