Uzi maalumu kwa wote walio wahi kutapeliwa

Youngstunna

JF-Expert Member
Jul 5, 2016
261
295
Habarini wakuu poleni na majukumu ya kazi,Pongezi pia kwa jitihada za ujenzi wa taifa

Moja kwa moja niende kwenye mada husika kama kichwa cha uzi huu kinavyosema ,Katika maisha huwa tunapitia changamoto mbalimbali ambazo huturudisha nyuma kiuchumi ,kiakili na hata kisaikolojia moja kati ya changamoto hizi ni pamoja na kutapelewa najua kuna baadhi yetu tulishawahi au walishawahi kutapeliwa fedha , nyumba , gari na kadharika naomba tupeane kisa ili iwe funzo kwa wasomaji juu ya mbinu mbali mbali wanazotumia matapeli ,Ili kutusaidia kuwa makini

Nianze na kisa hiki sio mimi ila ilimtokea rafiki yangu mmoja dar es salaam ambaye alikua anasumbuliwa na ugonjwa fulani ( sio vizuri kuutaja kwa hadhira ) kama unavyo kuna kipindi ukipatwa na tatizo lazima utatumia mbinu yoyote ili kujikomboa katika tatizo hilo haswa likizidi kuwa kubwa sana na pale ambapo umeshindwa kupata suluhisho kwa muda mrefu sasa katika harakati za kutafuta tiba rafiki yangu huyo akawa amezunguka sehemu nyingi bila kupata tiba kanisani hospital ndipo siku akakutana na tangazo la waganga wale wa Instagram akachukua namba na kumcheki WhatsApp.

Ambapo jamaa akamuuliza shida na kumwambia anadawa kwamba huyo rafiki yangu ana majini sasa inabidi achukue udi karatasi nyeupe na markepen nyekundu na maneno mganga akamwambia alafu achukue na kiasi cha fedha kwamba jamaa nyota yake sijui ipoje ambayo kiasi chake cha fedha ni laki nne na nusu apakae ile pesa unga wa udi alafu ajifute jasho kuanzia chini hadi juu na zile hela alafu kuna maneno hayataje huku akiendelea kujipangusa ( sijui nyie majini mniache afu cjuii nn nimesahau apo )

Akimaliza zile hela azifunge kwenye ile karatasi halafu ataje maneno yale kisa akazitume kwenye namba ya yule jamaaa, huku yule jamaa akifanya taratibu za kuongea na maluani sijui maruani ndo majini yenyewe alafu yampe maelekezo akishatuma pesa hizo (hao jamaa cjui huwa wanatumia madawa maana hakajikuta anafuata maelekezo yale na kutuma pesa )

Baaada ya kutuma jamaa akamwambia tena kumbe amekosea kisomo nyota yake ni ya 95 kwahyo atume laki nne na nusu tena, Rafiki yangu nae akafanya hivyo tena (na hela hiyo nyingine alikopa hahah) jumla akawa ametuma kama laki tisa sasa kila akimpigia jamaa, jaama anasema yupo busy na mgonjwa mara anasindikiza wageni mara ampigie kesho.

Kesho yake tena akaomba pesa hapo rafiki yangu akajua tayari kaishatapeliwa hahaha ,very ridiculous ila ndo kama hivyo jumla alitapeliwa kama million1 so thank me later ,ila thanks lord jamaa kapona now ila kuweni makini na waganga wa mitandaoni watu wanasaka pesa kila kona au wahubiri pia wamtandaoni kuweni makini.

Karibuni na nyie tushare experience.....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
.wote wo Tb Joshua /Gwajima/mwamposa...na mzee wa upako shekh sharifu majini wote wezi tu
 
Ukiwa huna imani, unatumiwa ka pepo kwanza, then kazi inaendelea, kuanzia apo mganga akiomba chochote wew ujanj huna tena, tayar usha tumiwa kapepo na hela utatoa tu upende usipende.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom