Za masiku wanajamvi, Leo nitaendelea la somo la kutengenea application inayohusiana na Audio Player.
Application ninazoenda kuzielez zituwa tatu, ya kwanza nitaita JF Audio hii nitacompile ikiwa na audio file ndani yake.
Application ya pili na yenyewe itahusiana na audio player ambayo nimeipa jina la JF audio2 hii tutaongea feature ya scratching hii feature ni nzuri kwa wale ambao wana plan ya kutengeneza DJ scratching applications.
Na application ya tatu pia ni ya audio player ila hii itakuwa advanced ambapo tutaonyeshana jinsi ya kuacess audio files ambazo umezihifadhi kwenye simu yako au memory card yako ya simu
Applications zetu zitatumia logo za JamiiForums(
JamiiForums nitaumia logo yenu kwa malengo ya kielimu tu na si vinginevyo) kama launch icon na screen logo, pia nitatumia mp3 audio ya wimbo wa usije mjini.
Pia kwako ww unaweza tumia images na audio yoyote ile unayotaka uzuri wa Android inasapoti aina nyingi za audio.
Hatua ya kwanza ni kutengeneza User Interface, Inteface itakuwa ni ya kawaida tu na haitakuwa na vitu vingi kama unavyoweza kuona hapo juu.
1. Chagua layout ambayo ungependelea kuitumia, mimi Hapo nimetumia GridLayout lakini kurahisisha kazi kwako ww nakushauri uitumie default Layout ambayo ni RelativeLayout. Tutakachokifanya ni kudrag na na kudrop.
2. Tunatakiwa tuongeze image(picha) ambayo itatokea kwenye screen yako ya simu kama launch icon. tumia image yoyote.
Kushoto kabisa mwa screen ya android studio kuna sehemu imeandikwa app, ili kuweka lauch icon right click hiyo sehemu ya app itakuja menu utachagua "New" ni option ya kwanza, kisha itatokea machagua mengine utachagua image Asset, kiufupi App>New>Image Asset>Asset Type>Image, kisha utachagua image kutoka kwenye kompyuta yako.
kitu kama hiki kitatokea.
3. Tutaanza ku-drag na ku-drop features kwenye screen yetu ambayo ina feauters za Button,ImageView na SeekBar.
Delete neno new text kwenye screen. kwa kuwa kitu cha kwanza tunachotaka kitokee ni logo ya JF hivyo tuta-drag ImageView kutoka sehemu ya widgets na kuiweka sehemu husika ambayo inaonekana hapo juu image ya kwanza.
Halafu Copy image ambayo utaitumia kama logo kisha paste kwenye forder iliyoandikwa drawable, inabidi tuipe id lakini default Id iliyotumika hapo inaitwa "imageview" kwa sasa sio muhimu sana.
Upande wa kulia kwa chini sehemu ya Properties kama inavyoonekana hapo juu tunatakiwa tuiweke image yenyewe husika utashuka chini mpaka sehemu iliyoandikwa src halafu kwenye sehemu iliyoandikwa @drawable/jfmm huwa iko empty ila hiyo ni address ya image yangu niliyochagua ili na ww uchague click hiyo sehemu kulia kuna button inatokea ikiwa na vinukta vitatu halafu itakupeleka sehemu nyingine na options bonyeza sehemu iliyoandikwa drawable halafu utatafuta image kwenye list image zitakazoenekana, click baada yapo image itatokea kwenye screen.
4. Kutoka upande wa widget kwa mara nyingine drap and drop kitu kinaitwa "seekBar" kwenye program languages zingine hutambulika kama progressbar, hii i-drop kwa chini ya image kama inavyoonekana image ya kwanza kabisa inavyoonekana, lengo la progress bar hapa ni kwa ajili ya ku-control sauti tu.
5. Hatua ya mwisho kutoka kwenye widget tena nenda sehemu iliyoandikwa button na u-drag na ku-drop buttons mara tatu na uzi-place sehemu yoyote kwenye screen. Kikawaida ukiweka button kwenye screen huwa zinaambatana na neno "new button" kubadilisha hayo maneno na kuweka neno ulitakalo click button kwenye screen nenda kulia kwenye upande wa Properties shuka chini tafuta sehemu imeandikwa "Text" kicha click na uandike neno unalitaka kama "play" nk, utafanya hivyo kwa kila button.
Kinachofuata sasa ni kufanya programming, na kama kawaida tunatumia java programming, bila kusahau tunapaswa audio file ambalo tutatumia, kuongeza audio file upande wa kushoto right click forder ilioandikwa "res" kama inavyoonekana hapo juu halafu chagua new directory na ulipe jina la "raw", kisha copy audio file lolote na ulipate kwenye hilo forder la "raw"