1. First App: WELCOME APP
Sasa tunaenda kuunda app ya kwanza ambayo ina hatua chache tu za kufuata, kabla ya kuunda hii app kwanza tuelewe baadhi ya sehemu za Android Studio ili iwe rahisi huko tuendapo.
Box namba moja, ni sehemu ambayo ina onyesha mipangilio ya contents zitakavyotokea katika screen ya simu, kwa mfano kwenye hiyo screen hapo ni Relative Rayout ambayo ni muonekano ambao child elements zinaonekana katika relative position na mtangulizi wake.
Pia kuna layout mbalimbali kama unavyoona kwenye box 1, tutajua kadri tunavyoendelea kujifunza. Layout unaweza kuzibadili kwa kuandika katika xml file au unadrag na kudrop.
Box namba 2: Hii ni sehemu ambayo ina vitu ambavyo vinaweza kuwekwa katika screen, kwa mfano unataka kwenye app yako ionekane maandishi(Text) basi utachagua aina ya widget unayohusiana na maandishi kwa hapo utachagua aidha smal, medium au large text , na kisha una drag na kuidrop kwenye position ya screen unayoitaka, hivyo hivyo kwenye widgets zingine kama image, buttons, checkbox na zingine kama zinavyoonekana kwenye box.
Box namba 3: Hii ni sehemu ambayo inaonyesha components ambazo zinapatikana katika screen ya simu. kwa mfano hapo tulichagua relative layout na yenyewe itatokea hii sehemu, baaada ya hapo tukachagua button na kuiweka kwenye basi na yenyewe itaonekana hii sehemu.
Box namba 4: Hii ni sehemu ambayo inahusisha vitu ambavyo vitaweza kumodify components za kwenye screen, kwa mfano ukiwa umedrop (umeachagua) widget ya small text neno ambalo litakalotokea ni "hello world"! kubadilisha hili utaenda kwenye device screen (part 3) na kuchagua TextView na kisha unarudi sehemu hii ya property na kushuka mpaka sehemu imeandikwa text na kisha kuandika neno unalolitaka.
Box namba 5: Hii ni sehemu inayohusisha sourcecodes ambazo ni za java, images ambazo utazozitumia kwenye app, resource files nk, tutajua kadri tunavooenda mbele.