Uzi maalum: Nini kifanyike ili nchi isonge mbele kiuchumi

Tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
62,312
109,342
Ndugu wanajamvi, kuna uzi maalumu uko hapa jukwaani unaotaka wanajamvi kwa umoja wetu kwa yoyote mwenye jinsi nchi inavyohujumiwa. Mimi nimeona bora sasa nije na wazo endelevu, tukumbuke kwamba baada ya kutaja maovu bado nchi yetu itatakiwa kuwa na jambo endelevu kwa maendeleo yetu.

Ninaomba mwanajamvi yoyote mwenye wazo ambalo litawezesha kuchangia ukuaji wa nchi yetu anaweza kuliweka hapa kwenye uzi huu ili kulisaidia taifa, kwani wapanga sera na wadau wengine muhimu wanapita hapa jukwaani wanaweza kulifanyia kazi wazo hilo ili kutoa ajira na hatimaye kukuza uchumi wetu.

Baadhi ya michango hiyo na michanganuo yake inaweza kuwa ni ile inayolenga kwenye mambo yafuatayo
  1. Jinsi ya kuongeza wigo wa kukusanya kodi nchini
  2. Ni namna gani tunaweza kuanzisha viwanda vidogovidogo na vikubwa na wapi katika nchi yetu ili kukuza ajira.
  3. Wapi katika nchi yetu kuna fursa fulani na jinsi fursa hiyo inaweza kutumika ili kukuza uchumi.
Lengo la uzi huu ambao utakuwa endelevu utasaidia awamu hii ya tano kukuza uchumi hasa kwa uzalishaji. Wasiwasi wangu ni kwamba kwenye ule uzi wa majipu tunaweza kupoteza wakati na wakati huohuo baadhi ya watu wakatumia uzi ule kuchafuana kwa ajili ya tofauti zao za kibiashara nk. Lakini pia baada ya kumaliza kutaja hayo majipu je kama taifa ndio tutakuwa tumefikia mwisho wa matatizo yetu? Ni nini haswa kitaendeleza maisha yetu?

CC: kimweri, kiranga, Pasco, nguruvi3, lizaboni, mcubic, jokakuu, mzee mwanakijiji
 
Asilimia kubwa ya wananchi ni kundi la vijana na watoto, wengi wao ni wanafunzi na wategemezi.
Katika waliobaki asilimia kubwa ipo katika sekta ambazo hazijarasimishwa hii ni changamoto kubwa.
Kama mkulima mdogo hana jinsi ya kuomba mkopo au kuwa na bima ya afya au kusajiliwa na mifuko ya kijamii hapa tutakwama.

Magufuli anafanya vizuri kuwaangalia wengi lakini hawa wengi lazima nao wawajibike na watambulike. Elimu ya bure isiwe zawadi, huduma bora za afya ziwe ni matunda ya uwajibikaji wa kila mmoja. Ukimtaja muuza vitumbua kama mnyonge atajiona mnyonge na atasubiri mfanyabiashara mkubwa na mfanyakazi amuhudumie. Ukimuondoa pembeni ya barabara ataona anaonewa, mabondeni vilevile.

Tujenge jamii inayowajibika kila mtu kwa uwezo wake, kila pato likatwe kodi kuanzia madini na gesi hadi maandazi na mazao.
 
Fursa ziko kibao kila kona.Sasa hivi watanzania wanataka vitu bora.Ukiboresha tu vilivyopo unavuna pesa.Nitoe mfano biashara ya kuchoma chips kuku ni biashara ya kawaida ambayo usingetarajia kuwa aweza kuja mwekezaji akaona hiyo ni fursa wakati chips zinachomwa kila kona.Lakini mwekezaji kama STEERS na wengine wakagundua kuwa watanzania wanataka chips bora zilizochomwa mazingira bora.
Kaangalie watu wanavyojazana na kula Kwenye hotel za STEERS dunia nzima ikiwemo Tanzania.Fursa tu zilizopo zikiboreshwa ni fursa mpya!!!

Kodi ni kutumia EFD kwenye biashara zote zenye shughuli nyingi kama mabaa,MASOKONI.VIWANJA,MAHALL ya sherehe,Matamasha yenye viingilio na vyombo vyote vinavyotumia barabara vilipe kodi kuanzia baiskel,mikokoteni nk Wakati wa Mkoloni kila baskeli ilikuwa inalipiwa kodi na anaweka kibati kwenye usukani kuonyesha Kalipa,

Mifugo yote inayozurura kula majani inatakiwa ilipiwe kodi hasa ng'ombe ,mbuzi na kondoo.Zinamaliza na kuharibu mazingira.Walipiwe kodi kwa mwaka kwa kila mfugo
 
1. KATIBA MPYA IMARA. ILI: 2. CCM ITOKE MADARAKANI NA KASUMBA ZAKE ZA KIKOLONI. 3. UTALII, MADINI, NA GESI NDIVYO VIJENGE BAJETI YA NCHI NA SIYO KUPANDISHA KODI NA KUANZA KUJISIFU KWA MAKUSANYO. HUU NI UJINGA NA HAUTAKUBALIKA. NA KWA HIYO: 4. KODI ISHUSHWE KABISA! MAANA KUKWEPA KODI KWA SASA SIYO KUHUJUMU UCHUMI ISIPOKUWA NI KUNUSURU MAISHA. 5. NA KADHALIKA....
 
Bila kusahau malipo yote ya ndani ya nchi lazima yalipwe kwa fedha yetu sh ili kuipa thamani
 
Kitu kitakachotusaidia ni kubadilisha fikra kwanza kutoka katika utegemezi kwenda katika utendaji kazi na hapo itakayosaidia ni elimu.. watu wasisome ili kuja kuwa wafanyakazi maofisini akikosa kazi ofisini basi maisha yamegoma, zitolewe elimu za kutosha kuhusu uzalendo,biashara,ujasiriamali na stadi za maisha. kusoma kuwe ni kupata ujuzi tu sio mkombozi wa kipato chako. Tukirekebisha hapo mambo mengi yataendelea... Kodi itapanda sababu watu wote watakuwa na elimu ya ulipaji kodi na umuhimu wake,Viwanda vitafunguliwa sababu watu watakuwa wazalendo watapenda kutumia vya kwao ili kuinua uchumi wa nchi na kumsaidia mtanzania mwingine afanikiwe kutokana na bidhaa anazotengeneza.Fursa zitaonekana sababu kila biashara na ujasiriamali utakaoanza utakuwa wa uhakika na wenye manufaa hivyo fursa zitaonekana sana sababu biashara ni watu na watu ndio fursa zenyewe....
 
Ndugu wanajamvi, kuna uzi maalumu uko hapa jukwaani unaotaka wanajamvi kwa umoja wetu kwa yoyote mwenye jinsi nchi inavyohujumiwa. Mimi nimeona bora sasa nije na wazo endelevu, tukumbuke kwamba baada ya kutaja maovu bado nchi yetu itatakiwa kuwa na jambo endelevu kwa maendeleo yetu.

Ninaomba mwanajamvi yoyote mwenye wazo ambalo litawezesha kuchangia ukuaji wa nchi yetu anaweza kuliweka hapa kwenye uzi huu ili kulisaidia taifa, kwani wapanga sera na wadau wengine muhimu wanapita hapa jukwaani wanaweza kulifanyia kazi wazo hilo ili kutoa ajira na hatimaye kukuza uchumi wetu.

Baadhi ya michango hiyo na michanganuo yake inaweza kuwa ni ile inayolenga kwenye mambo yafuatayo
  1. Jinsi ya kuongeza wigo wa kukusanya kodi nchini
  2. Ni namna gani tunaweza kuanzisha viwanda vidogovidogo na vikubwa na wapi katika nchi yetu ili kukuza ajira.
  3. Wapi katika nchi yetu kuna fursa fulani na jinsi fursa hiyo inaweza kutumika ili kukuza uchumi.
Lengo la uzi huu ambao utakuwa endelevu utasaidia awamu hii ya tano kukuza uchumi hasa kwa uzalishaji. Wasiwasi wangu ni kwamba kwenye ule uzi wa majipu tunaweza kupoteza wakati na wakati huohuo baadhi ya watu wakatumia uzi ule kuchafuana kwa ajili ya tofauti zao za kibiashara nk. Lakini pia baada ya kumaliza kutaja hayo majipu je kama taifa ndio tutakuwa tumefikia mwisho wa matatizo yetu? Ni nini haswa kitaendeleza maisha yetu?

CC: kimweri, kiranga, Pasco, nguruvi3, lizaboni, mcubic, jokakuu, mzee mwanakijiji
Simple, ili hii nchi iendelee, hichi chama cha viwavi jeshi (ccm) kinatakiwa kiondoke madarakani na kife kabisa. Kikiendelea kushikilia madaraka tutaishia kila siku kuanzisha threads na kujiuliza nchi hii ifanye nini ili iendelee. Hivi ki ukweli kabisa the likes of Magufuli, Nape, Kigwangala (Dr. Zero), Suluhu, Majaliwa na wengine wa dizaini hiyo kweli wanaweza kusimamia mabadiliko ya kiuchumi katika nchi hii? kama tunadhani wanaweza then, sisi watanzania tuna shida kuliko the likes of Nape Nnauye.
 
Serikali ianze mara moja utaratibu wa kuua wapumbavu na wajinga,, na kufunga wengine bila kusita kwenye majela yenye mateso makali.
tatizo la taifa hili ni wizi uliokithiri wa mali za umma na ukandamizaji kwa end users kwa manufaa ya familia chache,, hizi familia chache zinatakiwa ziadabishwe kuliokoa taifa hili...mfano pale usalama wa taifa na uhamiaji kuna familia chache za kinyakyusa zimejazana kule, pale tra,hazina na fedha kuna familia chache za watu fulani kutoka kaskazini zimejazana kwa maslahi ya familia zao.. kuna haja ya complete system overhaul kwenye taasisi nyeti na kuweka watu wa makabila na dini tofauti kwa uwiano ulio sawa... Ni wakati pia wa kutoa adhabu kali kwa wezi mfano kuua au majela ya chini ya ardhi kunusuru taifa na kwa future ya next generation..
 
Kwa upande wangu naona kilimo na viwanda haswa vidogovidogo ndio wangalau ndani ya miaka hii mitano vinaweza kubadilisha maisha ya wananchi walio wengi na kuleta mabadiliko ya haraka katika maisha ya wananchi. kwa mfano ni rahisi kuleta viwanda vidogovidogo na kuwakopesha vikundi mbali mbali kwenye uzalishaji wa zao fulani. Kwa mfano, maeneo wanayolima nanasi, machungwa, embe nk mashirika kama nssf badala ya kujenga majumba makubwa mijini na kusabibisha foleni ni bora pesa zao wakanunua na kujenga viwanda vidogovidogo kwa udhamini wa serekali. Nimezunguka kwenye vijiji vingi nchini nimekuta watu wamehasika vijana kwa wamama kujiunga na vikundi mbalimbali, hawa itakuwa rahisi sana kuwapatia viwanda vidogovidogo vya kusindika mazao mbali ili kuyapandisha thamani. Hebu nenda huko vijijini unaweza kulia wakati wa mazao jinsi wakulima wanavyopoteza mazao mengi kwa kushindwa kuyasindika na matokeo yake kuishia kulaliwa na madalali wa mazao.

Jeshi letu la wananchi ni taasisi ambayo kwa muda mrefu imekaa bila kuwa wazalishaji, kwa kuwa sasa ni muda wa amani ni bora jeshi letu likatumika kwa uzalishaji. Tuna mapori mengi, iwapo jeshi letu lingepatiwa pembejeo lingewesha kuzalisha chakula na malighafi nyingi na kuliongezea taifa kipato pamoja na hakiba ya chakula. Pia jeshi hili lingeweza kutumika kujenga nyumba za bei nafuu kwa kufuata mipango miji kuliko huu mtindo wa watu kujenga kiholela na kuishia kuvunjwa nyumba zao.

Iwapo baadhi ya mapendekezo yangu hapo juu yasipofanyiwa kazi tutaishia kuona maendeleo yakipelekwa Dar pekee yake na miji mikubwa hasa yenye upinzani wa kisiasa. Ukiuliza inakuwaje kila kitu ni Dar utaambiwa ndio walipa kodi wakubwa, sijui ndio kioo cha nchi na sababu nyingine zisizo na tija kama hizo. Kwa bahati mbaya watunga sera wote wanaishi Dar kiasi kwamba upeo wao wa kufikikiri unaishia hapohapo Dar. Lakini kiukweli kama tunataka nchi yetu ibadilike kwa haraka ni kuboresha kilimo kinachotoa ajira kwa watu wengi na kuwapa viwanda hasa vidogovidogo ili kupandisha thamani ya mazao yetu. Ndani ya kipindi cha miaka mitano tutakuwa na mabadiliko makubwa na miaka mingine tutaenda hatua nyingine ya viwanda vikubwa na kuwa na uchumu mkubwa zaidi.
 
Back
Top Bottom