Uzi maalum: Growth Hacking

HEADS UP! Update mpya
👇👇👇

***UPDATE II
USHAURI: Chukua kabisa kinywaji ukipendacho kikusindikize wakati unasoma, maana naongelea mbinu moja tu ila naiongelea sana kama nahubiri vile!

Ivi - umeshawahi 'kufilisika' kwasababu ya kodi? I mean - ushawahi kufikiria kufunga biashara kwasababu TRA wamekukalia kooni? Kama bado - jiandae. Juzi tu nimeona mtandaoni kada mmoja wa kile chama ambae alikuwa kwenye 'system' iliyopita na sasa yuko benchi - alijitahidi akafungua nursery school. Sasa dhahama lililomkuta ni kwamba TRA wamemshukia kama mwewe!!! Kwanza alipigwa kodi ya milioni kama 250 ivi, akakata rufaa - wakamwongezea, akakata rufaa tena - wakaongeza tena, mara ya mwisho nimeona ameomba msaada wa waziri.

Siku nyingine nilibahatika kuiona post ya ndugu yetu wa damu kabisa aitwae Isaya Yunge - alitoa ya moyoni juu ya nini kiliifelisha 'startup' yake ya 'Soma Technologies'. Japo ilikuwa ni post ya maandishi lakini niliweza kumsikia 'anavyolalama' na kuufokea 'mfumo' wa nchi yetu. Kwa jinsi alivyoufokea mfumo mpaka yeye mwenyewe alijishtukia akafuta ile post haraka sana kabla wapwa hatuja-sceenshot.

Haya mambo ni kawaida sana hapa nchini na pengine afrika kwa ujumla. 'MIFUMO' yetu sio mizuri kwa ujasiriamali. Kuanzia sera, sheria, kanuni, mitazamo ya jamii, uongozi na mazingira kwa ujumla wake... vyote vimekaa mkao wa kumfelisha mjasiriamali yeyote anaejaribu kupiga hatua kubwa tangu siku ya kwanza. Whether ni makusudi au la - mimi sijui, ila naamini tunakubaliana kuwa mifumo si rafiki.

Kama unafikiri natania; Nenda Njombe, ukifika muulizie mzee anaitwa Mzee Pwagu... sikiliza simulizi yake. Kisha nenda Mbeya, muulizie yule fundi gereji aliyetengeneza helikopta, ukimpata - sikiliza simulizi yake. Kama huko ni mbali, ingia Instagram - muulize Wema sepetu au Alberto Msando au Freeman Mbowe - wote wana kitu kimoja kinachofanana; kuna wakati biashara zao ziliingia matatizoni kwasababu moja tu - walikuwa nje ya 'system'. Ivi sijui mnanielewa?

Sasa waneni husema; "Mwenzako akinyolewa, zako tia maji." Kizazi kipya tunasema;"Jifunze kutokana na makosa - ya wengine."(Sio lazima yakukute wewe ndio ujifunze.) Unapoona kila mjasiriamali anaulalamikia 'mfumo, au anailalamikia serikali, au anailalamikia TRA, au anazilalamikia sheria, sera, kanuni au anamlalamikia Mungu, au pengine anamlalamikia mke wake, watoto wake, blah blah blah.... wewe unafanyaje ili kukwepa hayo yanayowaumiza wenzako?!?!?

Twende taratibu... ni vizuri kuwadanganya wengine lakini usijaribu kujidanganya kuwa hayatakukuta, kwasababu hata Marehemu Kapteni John Komba alipokuwa anaimba ile 'Mbele kwa mbele' nashawishika kuamini kuwa hakuwahi kufikiria kuwa ipo siku 'mfumo' utamgeuka. Vivyo hivyo mzee wa 'goli la mkono' na 'Bunge recorded and edited' - sidhani kama wakati anafanikisha kupatikana kwa goli la mkono aliwaza kuwa ipo siku 'mfumo' utamgeuka. Umeanza kunielewa elewa eeh?

Basi hebu vaa kofia ya ujasiriamali, darasa huru na liendelee;

MBINU YA 9: USIUPIGE MFUMO, PIGANA NDANI YA MFUMO. (DON'T FIGHT THE SYSTEM - FIGHT IN THE SYSTEM.)
Hakuna wa kukuonea huruma hapa, kwahiyo usitie huruma. Kuna wengine kule nyuma hawajasikia.... nimesema hivi... NOBODY GIVES A F*** what you are going through bro, you either compete or die.

Pia lawama siku zote hazijengi, kwahiyo usijaribu kumlaumu yeyote; yaani hata wewe mwenyewe usijilaumu - futa kabisa neno lawama kwenye kamusi yako. Kulalamika pia ni rahisi sana, kila mtu anaweza kulalamika - na ndo mwisho wa siku tunajikuta tumekuwa nchi ya walalamikaji; Mwananchi anamlalamikia kiongozi wake, kiongozi anailalamikia mamlaka iliyo juu, mamlaka iliyo juu inamlalamikia Mungu, Mungu tu ndo sijawahi sikia amelalamika hata siku moja. Swali la kijinga unaloweza kuniuliza ni kwamba - kwahiyo tufanyaje? Ntakujibu - pambana ndani ya mfumo.

Sikia, wakati UBER inaanzishwa ilikutana na upinzani mkali toka kwa madereva taksi za kawaida na mamlaka za kiserikali. Madereva taksi walikuwa wanalalamika kuwa madereva wa UBER wanapiga hela ndefu wakati hawana leseni za biashara za 'udereva taksi' ambazo ni gharama. Mamlaka za kiserikali zilikuwa zinaibana UBER iwatambue madereva wake kama wafanyakazi rasmi na sio 'wakandarasi'. Pia mamlaka zilikuwa zinashindwa kuamua UBER iwekwe kundi gani; Taxi company au Technology company?. Kwa ambae haelewi - UBER haiajiri madereva, inatoa mikataba ya muda mfupi. Kwamba umejisajili UBER haimaanishi umeajiriwa na UBER. Kwahiyo, kwasababu haiwaajiri madereva imeepuka kuwa responsible kama mwajiri. Wengi wetu tunafahamu - waajiri wana mambo mengi ambayo wanapaswa kuyatimiza kwa wafanyakazi wao - UBER walikwepa hiyo since day 1. *Hiyo ndo inaitwa DISRUPTION / Challenging the status quo.

Sasa, kufika hapa walipo leo, UBER wamefanya mambo mengi sana nyuma ya pazia ambayo wengi hawajapata fursa ya kuyasikia. Siwezi kuelezea yote maana ni mengi, lakini nitakupa mbinu moja ambayo UBER waliitumia 'kupigana ndani ya mfumo'. Ilikuwa hivi;

UBER ilipata upinzani mkubwa pindi walipoanza ku-scale (Yaani kuipanua bishara yao katika nchi tofauti duniani). Serikali nyingi zilikuwa zinawanyima vibali kwasababu tofauti tofauti. UBER wakatumia mbinu moja.... wakaanza kujipenyeza kimya kimya bila ya serikali za nchi husika kujua. Lengo lao lilikuwa moja... kuhakikisha wanapata wateja wengi (Traction) kwa namna ambayo watakaopenda kuomba kibali serikalini, serikali ishindwe kuwazuia kwasababu ya wingi wa watu ambao tayari wanaitumia UBER (Too good to resist). Kuna mtu hajaelewa, ngoja nijaribu hivi;

Fikiria unataka kuanzisha biashara ya kutoa huduma jijini Dar ambayo unajua fika ukienda kuomba kibali utanyimwa. Cha kufanya, wewe anza kuitoa hiyo huduma kimya kimya, mdogo mdogo - bila matangazo, bila mbwembwe, unapata wateja through word of mouth - acha wateja wasimuliane wenyewe. Unaifanya hiyo biashara kwa muda fulani na hatimaye unapata wateja kama Milioni 2 hivi wanaotumia huduma yako. Ndiposa unatoka na takwimu zako hizo zilizoshiba, unaenda kuomba kibali. Kwamba mimi XYZ nina biashara ABC ambayo ina mpaka sasa ina watumiaji wa moja kwa moja Milioni 2. Watakunyima?

Weee acha ubwege - ndio, wanaweza kukunyima na unaweza kujikuta unapewa kesi ya uhujumu uchumi kwa kufanya biashara kinyume na sheria. Na ndio maana ili uweze kupigana ndani ya mfumo wowote, ni LAZIMA uhakikishe kwanza unazielewa vizuri SHERIA ZOTE ZA MCHEZO kisha unaanza kuzivunja like nobody's business. {Ssssh sogea nikunong'oneze.... si unamfahamu Chenge mzee wa vijisenti? Ivi unakumbuka kila dili kubwa na yeye yumo lakini hajawahi kupatikana na hatia popote? Sasa yule bwana ndo mfano halisi wa hii kanuni ya kuelewa kwanza siri ya mchezo kabla hujaanza kucheza rafu za kukata na shoka. Lakini ibaki siri yetu, usimwambie mtu, umesikia!?!?!?}

Well, kiuhalisia ni vigumu kuzielewa sheria za mchezo kwa muda mfupi, kama wewe hujasomea sheria; mbaya zaidi kuna waliosomea sheria lakini bado ni mtihani kwao kuzielewa sheria za michezo vizuri. Na ndio maana wapo wataalamu, wanaogopwa wakiwa mbele ya pilato; akina Kibatala, Lissu, Msando na wengine a.k.a Mawakili Wasomi. Pointi ni kuwa hakikisha unasema na watu wa kada hii vizuri kabla hujaanza kuucheza huu mchezo ili ujue wapi unaweza ku-take advantage ya udhaifu wa sheria. Kama huna rafiki hata mmoja ambae ni wakili msomi - anza kum-find ASAP.

Kuna wakati UBER walitengeneza version ya UBER app ambayo ilikuwa mahsusi kwaajili ya watu wa vyombo vya ulinzi na usalama tu. Yaani ilikuwa hivi; Kama wewe ni polisi, au FBI, au CIA basi ujue app ya UBER utakayo-download sio ile halisi. Ukiitisha gari linakuja lakini dakika chache kabla ya kukufikia dereva ana-cancel. Polisi wa huko mbele mbele washatembea sana kwa miguu na wakati UBER zilikuwepo za kumwaga. Sasa usiniulize waliwezaje kuwatambua hao wanausalama, ila ninachojua ni kuwa teknolojia inakua kwa kasi ya ajabu. You have to be ahead of the game.

Najua, wengi huwa wana-opt kutumia siasa. Yaani unachukua kadi ya chama, unaweka bendera ya chama katika maeneo yako yote ya biashara, na pengine unagombea uongozi kwa lengo moja; kujihami dhidi ya mfumo. Tatizo ni kwamba, siasa ni si-hasa na ni mchezo wa hovyo sana; wakati na saa usioijua siasa inakutema na kukuacha unapambana na mfumo bila huruma. Kawaulize vibopa wa enzi za Kikwete wako wapi siku hizi, kisha kawatafute wote walioshikamanisha biashara zao na siasa... wako wapi? Ukishikamanisha biashara zako na siasa manaake wewe umechagua kuishi maisha ya ujanja ujanja. Sasa siku ukitoka kwenye siasa au chama lako likitoka kwenye siasa ndo utaelewa ninachoongea.

Bado hujaelewa namna ya kupambana kwenye mfumo? Well sikia hii; Makampuni mengi makubwa duniani, na hata hapa kwetu huwa yanakwepa kodi. Lakini hayawezi kushtakiwa, unajua kwanini? Yanacheza na sheria. Unakumbuka wakati taasisi za kidini zinapata msamaha wa kodi - ikazuka kawaida ya watu kuagiza bidhaa nje ya nchi kwa jina la taasisi fulani ya kidini ili kutolipa kodi! Ile sheria ya msamaha wa kodi kwa taasisi za kidini ilikuwa ni fursa kwa wajasiriamali wajanja.

Wengine wanatumia mfumo wa Holding company - yaani unakuwa na kampuni mama ambayo haijasajiliwa hapa nchini. Hiyo kampuni mama unaenda kuisajili katika nchi ambayo ina unafuu mkubwa wa kodi na mazingira yake ya kibiashara yako vizuri (Kuna utulivu wa kisiasa na sheria imara). Kisha unakuja unafungua kampuni dada (Subsidiary) hapa nchini. Kisha unahakikisha assets zote zinamilikiwa na ile kampuni mama, then kampuni dada inafanya kuazima au kukodisha.

Baada ya hapo mapato yote na faida unahakikisha zinahifadhiwa katika akaunti za kampuni mama za huko huko ughaibuni. Na unahakikisha pia kampuni dada inalipa gharama za kukodisha assets n.k. Unacheza na namba kwa namna ambayo kampuni dada mwisho wa siku inaweza kuonekana haizalishi faida yoyote. Na ukishapiga shekeli za kutosha, unairipoti kampuni dada kama imefilisika - na auditors wakicheki vitabu vyako wanakuta kweli mzee mapato yako yote yalikuwa yanalipa madeni kwa kampuni mama. Uzuri ukifilisika, umefilisika... unaondoka taratiiibu huku ukitabasamu kimoyo moyo - usitabasamu usoni bro maana utafungwa... ohooo!!!

BOTTOM LINE:
Sahau vyote nilivyosema katika mbinu hii ya 9 ila kumbuka kitu kimoja - siku zote tafuta mbinu za kucheza kwa kutumia sheria zilizopo. Usikatishwe tamaa na mfumo, tafuta namna ya kucheza ndani ya mfumo pasipo kukanyaga waya. Na zaidi ya yote, changamoto ni fursa kwa mjasiriamali; kwahiyo kama kuna changamoto nyingi maanake kuna fursa nyingi.

Tatizo nini bro?.. rushwa? - buni njia ya kuondoa rushwa, utapiga mamilioni. Hakuna ajira? - Fungua kampuni yako ili ujiajiri. Tatizo nini, mtaji? Kama huwezi kutumia TZS 10,000/= kuanzisha biashara basi hata ukipewa TZS 10m utafeli tu - huna DNA za ujasiriamali. Hata kama huna hata mia, bado sio sababu ya kufeli; watu wana pesa - unachotakiwa ni kutafuta namna ya kuwafanya watoe hizo pesa kukupa wewe.

Well, mimi sio motivational speaker - kwahiyo sisemi kuwa hizi changamoto ni ndogo, la hasha. Lakini najua maisha ni kuchagua - kwa kila kinachotokea una options za kuchagua. Na unapochagua kimoja unapoteza kingine... that's a fact! Na ukisema huchagui chochote, nature itakuchagulia by default.

Chagua kuacha kulalamika, chagua kuacha kuwalaumu watu wengine, chagua kuacha visingizio, chagua marafiki wazuri wenye faida, chagua aina ya ushauri unaosikiliza, chagua kupambana mpaka kieleweke, chagua kufurahi siku zote, chagua kula vizuri, chagua kuwajali wengine, chagua kutazama fursa kila mahali, chagua kuona nyota zinazong'aa badala ya giza, chagua kutokuogopa kukosea kwa kuwa ni fursa ya kujifunza, chagua kutokimbia matatizo, chagua, chagua, chagua... chagua kupambana ndani ya mifumo hii hii tuliyonayo.

Kama si wewe, nani? Kama si sasa, lini?

***Itaendelea***
Virus
July I, MMXX
 
Back
Top Bottom