technology imekuwa ikibadilika kwa kasi sana, hata mifumo ya TRA lazima iendane na Technolojia. sasa hivi kuna uhakiki wa TIN, zoezi hili ni kwa ajili ya kuboresha taarifa za walipakodi(data clean up). lengo la kwanza ni kuwa na data/taarifa halisi na sahili za walipakodi. lakin pia kufanya taarifa hizo ziweze kufanya kazi katika mifumo ya kisasa.
TRA katika ukusanyaji kodi wapo vizuri sana, lazima tukubali kwamba mifumo ya kutuma ritani, mifumo ya malipo, mifumo ya uingizwaji na uondoshwaji wa bidhaa nchini, na mifumo mingine ambayo inatumika kwa namna moja au nyingine imeboreshwa sana.
sisi watanzania tumekuwa na kawaida ya kuzima moto yaani tunasubiri dakika za mwisho ndo tunataka jambo letu lipite tena kwa wakati.mfano mzuri n dar es salaam ambako zoezi la uhakiki wa TIN lilianza tokea mwez wa 9 kama sikosei....lakini huwezi kuamin deadline ya mwanzo ilikuwa mwezi wa 11, watu wakawa wengi sana vituoni. TRA wakaamua kuongeza muda hadi jan,31, 2017. mwezi wote wa kumi na mbili na wakwanza mwanzoni vituo vilikuwa tupu kabisa....lakin ilipofika kwenye tarehe 20, watu wakawa wengi sana na kuanza kuilaumu TRA. sasa hapa tunapaswa kuona ni sisi wananchi tulikosea au n TRA.
Kwa maoni yangu kama watu wangefika kwa wakati zoezi lingeenda vizuri sana.....lakini kwa zile tafrani za mwisho sijui hata mafanikio yake...
Nashauri zoezi likianza tufike kwa wakati, na ni vizuri kuwa na mawazo chanya kwamba kuna nia njema katika project hiz....wanatumia hela nyingi sana lazima zoezi linaumuhimu mkubwa. asanteni.