Barbarosa
JF-Expert Member
- Apr 16, 2015
- 22,584
- 27,811
Utengenezwaji wa Gari aina ya Land Rover Defender umesitishwa rasmi na sasa hivi gari hiyo iliyo na historia ndefu hasa hapa Barani Afrika haitatengenezwa tena!
============
Rover ambae ndio mzalishaji wa kwanza aliunda gari kipindi cha vita kuu ya pili ya dunia. Mwaka 1947, wakulima wa kiingereza walihitaji gari nafuu na inayoweza kutembea sehemu ambazohazina barabara na Rover ikawatengezea kwa malighafi zilizokuwa zinapatikana wakati huo wa vita. Kutokana na uhaba wa chuma, bodi ilitengenezwa na aluminiam nafuu. Rangi za jeshi zilikuwa nyingi hivyo iliwezekana kuchagua rangi yoyote ambayo ina asili ya kijani. Miaka ya 1950 ikawa alama ya uzalendo kwa waingereza, gari ambalo lilizingatia zaidi dhana ya ufanyaji kazi kuliko burudani.
Iliboreshwa mwaka 1991 na kuitwa Diffender ikiwa na damu ya mtangulizi wake, ilikuwa na makelele mengi na ukiosha gari kwa kutumia bomba linalotoa maji kwa kasi basi utayakuta ndani yameingia. Defender inahitimisha miaka 67 kwa gari ambazo kumbukumbu yake haitasahaulika kwa Tanzania kuanzia uhuru, matumizi maarufu kwa vyombo vya usalama na sehemu ambazo hazikuwa rahisi kufikika kulingana na hali ya barabara zetu.