Uzalendo wa Rais huyu umenishangaza sana!

Mchokoo

JF-Expert Member
Jul 28, 2015
1,179
1,579
Ndiyo,
Ni leo hii; wakati nikielekea katika mihangaiko yangu, katika kujitafutia riziki; nilipofika pale banana ili nipate usafiri, nikashangaa kukuta watu wengi wakisemezana makundi kwa makundi kumhusu mheshimiwa rais.

Dah!
Ukweli ni kwamba; japo navutiwa sana na maongezi haya ila naona ni bora niondokea maana nitachelewa kwenda kazini.
Kwa shida najilazimisha kuchukuwa basi la kariakoo,

Mweeee!

Kumbe pale kituoni ilikuwa cha mtoto, sasa mambo yapo humu ndani ya bus!
Nakwambia, si furaha hiyo, kila mtu anasema lake, jamani, jamani, na sisi watanzania Mungu katukumbuka! Tumeteseka kwa muda mrefu ila sasa itoshe!
Huyu baba si mbinafsi kabisaaa!

Nasema huyu ndiye kiongozi ambaye nchi yetu ilimsubiri kwa muda mrefu. Mzee mmoja wa makamo anasikika akimaka!

Huku akina mama kadhaa wakadhaa wakiyasindikiza maneno yake kwa vigeregere vinavyoyasisimua masikio ya wengi ndani ya bus.

Sasa tuko tazara! ghafla, tunashtushwa mwangwi mkubwa wa makelele yanayoashiria makutano ya watu.

Mara, nje ya bus, tunaona watu wengi mno!
Kinachonishangaza zaidi; ni pale ninapogundua kuwa katika uma ule zinaonekana bendera za vyama vyenye itikadi tofauti-tofauti lakini sasa wote wanaungana kwa pamoja katika hili!
Vijana kwa wazee! Tazama kule, wakinamama waliojifunga kisawasawa wakiandamana huku polisi wakiwasindikiza pembeni mwao kwa amani.

Mmmh!
Sasa magari ndiyo hayaendi kabisa!
Hee! Nikirudisha macho ndani ya daladala nagundua kuwa tumebaki wachache mno mle
Kumbe wenzetu wengi wameshashuka kitambo.
Ngoja na mimi nishuke chini.

Loh!
Kamwe maishani mwangu sijawahi kuona hamasa, shauku, na hisia za umoja kama ninazoziona sasa!
Hii yote ni katika kumuunga mkono mheshimiwa rais.

Kiongozi huyu atakumbukwa vizazi na vizazi katika historia ya nchi yetu.
Kijana mmoja anaelezea huku watu wakimsikiliza kwa makini.
Hebu ngoja nami nijisogeze hapa illi nisikie, maana kwa kweli mimi katika mambo ya siasa huwa ni mzito kuyaelewa. Halafu tena anajibu yule yule kijana baada ya kuulizwa swali chokonozi na mmojawapo wa mtu katika hadhira ile, eti, kwa nini watanzania wamkumbuke rais wetu huyu kwa miaka mingi ijayo?

Akisha kukohoa kidogo, anaendelea.

Uongozi ni kipaji, anasema, ndio maana mnaona hiki kinachotokea leo.
Huko nyuma tuzoea kuuona mwendo mduara mbaya!

Ndiyo, kama siyo sisi ni wenzetu.

Kwa mikono yetu wenyewe tuliufinyanga mfumo unaaozaa wenyewe na kuuwa wenyewe!
Yaani ninachozungumzia hapa ni mazingira yanakuchagua na mazingira yanakutumbua!
Daima ukiwa kwenye mfumo huu haijarishi wewe ni mwema au ni muovu kwa asili, ni lazima tu uende na maji.
Ajabu ni kwamba; wakati huo sisi wananchi wa kawaida kwa kutojua tulimshangiria sana kiongozi aliyekuwa anaondoa uuzo serikalini.

Ingawa hata hivyo viongozi wa aina hiyo hawakufaulu kamwe kuondoa madhara yaliyosababishwa na uozo huo!
Eti hilo nalo tuliridhika nalo!
Kweli, kweli! Ile hadhira inajibu.

Sasa mambo yamebadirika! Anaendelea yule Kijana.

Mara baada ya kuipitisha katiba mpya tena ile iliyopendekezwa na tume ya jaji Warioba, kifungu kwa kifungu. Yaani kama ilivyopendekezwa na wananchi. Kwa sasa mheshimiwa rais ameunda mifumo imara inayozuia wizi na ubadhirifu wa mali ya uma.
Ninyi wenyewe ni mashahidi jinsi yeye mwenyewe alipotutangazia wazi kuwa; iwapo hatatimiza wajibu wake kwa mujibu wa katiba hii mpya, na kulingana na viapo alivyoapa, basi, yuko tayari tumuwajibishe hata leo hii.
Si mnakumbuka msisitizo wake siku ile alipokuwa akilihutubia taifa kupitia bunge?

Pale alipowaambia viongozi wenzake kuwa wananchi ndio mabosi wao katika nchi hii.
Na kwamba serikali anayoiongoza yeye kwa mujibu wa sheria haitafumbia macho yule asiyetaka kuwatumikia wananchi kwa moyo wa kujitoa muhanga!
Ndiyo sababu mnaona Takukuru wanafanya kazi yao bila kuingiliwa na chombo chochote!
Polisi wanatimiza majukumu yao ya kuwa usalama wa laia.

Na mahakama zinatenda haki kwa kuwa majaji na mahakimu kwa mujibu wa katiba hii mpya wako huru ilihali nao wakijua fika kwamba mifumo mingine ya kichungunzi nayo iko huru tena nayo imewakodolea macho.

Ninasema uzalendo wa kiongozi huyu umeigusa ncha ya kilele cha utu kwa sababu hii.

1) Ni viongozi wachache sana wenye hurka ya kutotaka kujirundikia madaraka wakati wakiwa na uwezo huo.
2) Kwa afrika ni viongozi wachache sana ambao wanaoheshimu na kudhamini mawazo ya raia wao kama huyu wetu!

3) Ni vingozi wachache sana duniani wanaokubali kwa hiyari yao kuyatengeneza mazingira mazuri ya kuwajibishwa pindi wakishindwa kuwajibika!
Wakati huyu kijana akiendelea kuongea kwa msisimko mkubwa mara nasikia Ko! Ko! Ko!
Nastuka kutoka usingizini !!

Eti kumbe ni ndoto!

Ndugu zangu naomba nisaidiwe kuhusu hii ndoto.

Hiki nikichoota kinahusiana na haya anayoyafanya mheshimiwa rais?
Na pengine ndiye atakayefanya hata lile la kuunda mifumo huru ya kiutawala itakayokomesha kabisa hali hii ya mduara wa uovu?

Au huyu ni rais mwingine atakayekuja baadaye?
Loh!
Nimeutamani wakati niliouota ufike upesi.
 
Kama haya yote yametokea kweli, naamini watu wa Dar hamnaga kazi za kufanya, Huwezi kuta haya mambo Arusha, ngumu sana!
 
Hizi sasa mbwata, mswahili akipata utazisikia lakini kamwe wengine lazima tufikiri tofauti. Maneno matamu ndio yamewafikisha hapa mpaka zaidi ya 50 Bado mko maskini. Wote wanaokuja kwenu wapimeni kwa outcomes, nyie Hali zenu Bado hoehae na mnajisifia ujinga mko kwenye daladala tena za goms.
Wanasiasa wanawatega kijinga sana amkeni, wakati huu ndio mbaya zaidi kwa maisha yenu jamaa anakaribu nusu ya awamu Bado teua fukuza lini atawaletea maendeleo.
Approach yake mbaya na atendi haki kwa kuchagua, jifunzeni kusikiliza pande zote ndio maana Mungu amewaumba na masikio mawili.
 
Yametokea muda gani na siku gani haya?
Kwa maana nimepita tazara saa moja unusu asubuhi kuelekea vingunguti na saa tatu nimepita hapo kurudi mjini...kwa macho yangu sijaona kitu kama hicho.
 
Arusha kunasehemu nasikia sukari imeshaanza kufichwa, imekuwa adimu kuliko hata cocaine.
Unga wa ugali sijui nao ushashuka bei, mimi sijui maana natumia mihogo na viazi vitamu.
SAMAHANINI KWA KWENDA NJE YA MADA Maana nimeshindwa kuanzisha mada nyingine kwamaana haka kamchina kameisha chaja, na huku kijijini hakuna umeme mpaka niende mjini mwendo wa nauli sh 5000 kwenda na kurudi na magari yenyewe na mandoline.
 
Uzalendo gani unaouongelea hapa?

Wazalendo ni wale waliopinga hii mikataba na sheria za madini wakati zinapitishwa sio hawa wanaokuja kutibu majereha leo hii tena wengine wakituhumiwa kuwa ni wanufaika.

Mlistahili kuwa jela na sio kujikosha leo hii.
 
Kama haya yote yametokea kweli, naamini watu wa Dar hamnaga kazi za kufanya, Huwezi kuta haya mambo Arusha, ngumu sana!

Arusha ipi mkuu ile ya maandamano na migomo ambayo lema alikuwa akijisikia anawapelekesha misukule na kumtukana fisadi lowasa?
 
Angeshughulikia issue ya Bashite kwa ujasiri na moyo huo huo, angeishafika mbingu ya saba muda huu. Tukubali labda kwamba nobody is perfect!
 
kweli kabisa kwa mwenye akili anajua kuwa magufuri ni mzalendo sasa tunasubiria bunge liache uvyama livae joho la uzalendo tutasonga mbele mungu ibariki tanzania
 
Mleta mada, wewe binafsi maisha yako yamebadilika kiasi gani na hili sakata la madini? Ulipokuwa kwenye daladala hukuwaza labda siku moja uwe na usafiri wako mwenyewe badala ya kupanda dala dala na kuboresha maisha yako?
 
Ndiyo,
Ni leo hii; wakati nikielekea katika mihangaiko yangu, katika kujitafutia riziki; nilipofika pale banana ili nipate usafiri, nikashangaa kukuta watu wengi wakisemezana makundi kwa makundi kumhusu mheshimiwa rais.

Dah!
Ukweli ni kwamba; japo navutiwa sana na maongezi haya ila naona ni bora niondokea maana nitachelewa kwenda kazini.
Kwa shida najilazimisha kuchukuwa basi la kariakoo,

Mweeee!

Kumbe pale kituoni ilikuwa cha mtoto, sasa mambo yapo humu ndani ya bus!
Nakwambia, si furaha hiyo, kila mtu anasema lake, jamani, jamani, na sisi watanzania Mungu katukumbuka! Tumeteseka kwa muda mrefu ila sasa itoshe!
Huyu baba si mbinafsi kabisaaa!

Nasema huyu ndiye kiongozi ambaye nchi yetu ilimsubiri kwa muda mrefu. Mzee mmoja wa makamo anasikika akimaka!

Huku akina mama kadhaa wakadhaa wakiyasindikiza maneno yake kwa vigeregere vinavyoyasisimua masikio ya wengi ndani ya bus.

Sasa tuko tazara! ghafla, tunashtushwa mwangwi mkubwa wa makelele yanayoashiria makutano ya watu.

Mara, nje ya bus, tunaona watu wengi mno!
Kinachonishangaza zaidi; ni pale ninapogundua kuwa katika uma ule zinaonekana bendera za vyama vyenye itikadi tofauti-tofauti lakini sasa wote wanaungana kwa pamoja katika hili!
Vijana kwa wazee! Tazama kule, wakinamama waliojifunga kisawasawa wakiandamana huku polisi wakiwasindikiza pembeni mwao kwa amani.

Mmmh!
Sasa magari ndiyo hayaendi kabisa!
Hee! Nikirudisha macho ndani ya daladala nagundua kuwa tumebaki wachache mno mle
Kumbe wenzetu wengi wameshashuka kitambo.
Ngoja na mimi nishuke chini.

Loh!
Kamwe maishani mwangu sijawahi kuona hamasa, shauku, na hisia za umoja kama ninazoziona sasa!
Hii yote ni katika kumuunga mkono mheshimiwa rais.

Kiongozi huyu atakumbukwa vizazi na vizazi katika historia ya nchi yetu.
Kijana mmoja anaelezea huku watu wakimsikiliza kwa makini.
Hebu ngoja nami nijisogeze hapa illi nisikie, maana kwa kweli mimi katika mambo ya siasa huwa ni mzito kuyaelewa. Halafu tena anajibu yule yule kijana baada ya kuulizwa swali chokonozi na mmojawapo wa mtu katika hadhira ile, eti, kwa nini watanzania wamkumbuke rais wetu huyu kwa miaka mingi ijayo?

Akisha kukohoa kidogo, anaendelea.

Uongozi ni kipaji, anasema, ndio maana mnaona hiki kinachotokea leo.
Huko nyuma tuzoea kuuona mwendo mduara mbaya!

Ndiyo, kama siyo sisi ni wenzetu.

Kwa mikono yetu wenyewe tuliufinyanga mfumo unaaozaa wenyewe na kuuwa wenyewe!
Yaani ninachozungumzia hapa ni mazingira yanakuchagua na mazingira yanakutumbua!
Daima ukiwa kwenye mfumo huu haijarishi wewe ni mwema au ni muovu kwa asili, ni lazima tu uende na maji.
Ajabu ni kwamba; wakati huo sisi wananchi wa kawaida kwa kutojua tulimshangiria sana kiongozi aliyekuwa anaondoa uuzo serikalini.

Ingawa hata hivyo viongozi wa aina hiyo hawakufaulu kamwe kuondoa madhara yaliyosababishwa na uozo huo!
Eti hilo nalo tuliridhika nalo!
Kweli, kweli! Ile hadhira inajibu.

Sasa mambo yamebadirika! Anaendelea yule Kijana.

Mara baada ya kuipitisha katiba mpya tena ile iliyopendekezwa na tume ya jaji Warioba, kifungu kwa kifungu. Yaani kama ilivyopendekezwa na wananchi. Kwa sasa mheshimiwa rais ameunda mifumo imara inayozuia wizi na ubadhirifu wa mali ya uma.
Ninyi wenyewe ni mashahidi jinsi yeye mwenyewe alipotutangazia wazi kuwa; iwapo hatatimiza wajibu wake kwa mujibu wa katiba hii mpya, na kulingana na viapo alivyoapa, basi, yuko tayari tumuwajibishe hata leo hii.
Si mnakumbuka msisitizo wake siku ile alipokuwa akilihutubia taifa kupitia bunge?

Pale alipowaambia viongozi wenzake kuwa wananchi ndio mabosi wao katika nchi hii.
Na kwamba serikali anayoiongoza yeye kwa mujibu wa sheria haitafumbia macho yule asiyetaka kuwatumikia wananchi kwa moyo wa kujitoa muhanga!
Ndiyo sababu mnaona Takukuru wanafanya kazi yao bila kuingiliwa na chombo chochote!
Polisi wanatimiza majukumu yao ya kuwa usalama wa laia.

Na mahakama zinatenda haki kwa kuwa majaji na mahakimu kwa mujibu wa katiba hii mpya wako huru ilihali nao wakijua fika kwamba mifumo mingine ya kichungunzi nayo iko huru tena nayo imewakodolea macho.

Ninasema uzalendo wa kiongozi huyu umeigusa ncha ya kilele cha utu kwa sababu hii.

1) Ni viongozi wachache sana wenye hurka ya kutotaka kujirundikia madaraka wakati wakiwa na uwezo huo.
2) Kwa afrika ni viongozi wachache sana ambao wanaoheshimu na kudhamini mawazo ya raia wao kama huyu wetu!

3) Ni vingozi wachache sana duniani wanaokubali kwa hiyari yao kuyatengeneza mazingira mazuri ya kuwajibishwa pindi wakishindwa kuwajibika!
Wakati huyu kijana akiendelea kuongea kwa msisimko mkubwa mara nasikia Ko! Ko! Ko!
Nastuka kutoka usingizini !!

Eti kumbe ni ndoto!

Ndugu zangu naomba nisaidiwe kuhusu hii ndoto.

Hiki nikichoota kinahusiana na haya anayoyafanya mheshimiwa rais?
Na pengine ndiye atakayefanya hata lile la kuunda mifumo huru ya kiutawala itakayokomesha kabisa hali hii ya mduara wa uovu?

Au huyu ni rais mwingine atakayekuja baadaye?
Loh!
Nimeutamani wakati niliouota ufike upesi.
Ndoto hiyo na za aina yako ataifurahia, waweza kupewa hata airtime STAR TV. Ahsante kwa ubunifu.
 
Back
Top Bottom