fimboyamnyonge
Member
- Jan 17, 2016
- 13
- 0
BilLaahi taufiqi wala Hidaayah wa Salaamu 'alaykum wa RahmatulLaahi wa Barakaatuhu
UZALENDO NI NINI?
Nimekua nikiwasikia watu mbalimbali miaka michache iliyopita wakiongelea ama uzalendo(hali) au mzalendo (mtu). Lakini bado nashindwa kuelewa kama walio wengi wamekwenda kwenye kamusi kujifunza maana ya uzalendo au hata kuulizia wazalendo walikua watu wa namna gani? Nachelea kufikiri kwamba wengi wetu uzalendo umekua kama msimu tu mpya wa kileo ambao umepoteza maana yake halisi,tumeuchukulia kwa tafsiri ama neno na si kutenda kutoka moyoni.Patriotism is devoted love, support, and defense of one's country; national loyalty uzalendo ni ile hali ya mtu kuipenda na kuithamini nchi yake na kuweka maslahi ya taifa lake mbele. uzalendo ni neno dogo lakini maana inayobebwa na neno uzalendo ni kubwa.
Turudi kwenye hoja wasomi wachache wamekua wakiwapotosha wananchi kwa makusudi ama kwa kujifanya wazalendo au kusingizia uzalendo kwenye masuala muhimu ya nchi kama njia mojawapo ya kuikosoa Serikali hamna Serikali duniani ambayo inafanya kila kitu kwa kupatia asilimia 100 kuna sehemu inakosea lakini kukosea huko kunakua ni kudogo kuliko kupatia.
Tanzania sasa hivi ipo kwenye mabadiliko ya kimfumo ambayo yalishajijenga kama sehemu ya maisha ya kawaida ya mtanzania ambayo yalitufanya tudumae kiakili na kusababisha uchumi udumae ki uchumi Tanzania ipo kwenye Preconditons for take off stage na inatengeneza mazingira ya kuelekea kwenye take off stage of economy ambayo wachumi wote wanajua ndio hasa kipindi kigumu kabisa kwenye uchumi ambao sisi tunaita kuelekea uchumi wa kati kwa kujikumbushia tukasome Rostow's Stages of Economic Growth model zile five stages.
1.Traditional society
2.Preconditions for take-off
3.Take-off
4.Drive to maturity
5.Age of High mass consumption
Tunacho kitu kimoja muhimu sana ambacho tumefanikiwa kwa asilimia 100 kukilinda nacho ni amani kwenye kujenga uchumi ulio imara ni lazima kuwe na amani mahali hapo lakini pia umoja na mshikamono,vyote hivi tumefanikiwa kwa asilimia 100 hasa baada ya kuipeleka nchi kwenye ujamaa. Lakini leo hii kunazuka watu wa hovyo kabisa walio wasomi wazuri sana na wenye dhamana kubwa na kuanza kupinga maandalizi ya kuelekea kwenye third stage of economic development hivi tukiendelea na Business as usual kwa hali ilivyokua hapa nchini kwetu tutafanikiwa kweli kuvuka?
Kila kukicha madudu mapya yanaibuliwa na watu wanapinga tu watu ndani ya Serikali ikiwemo baadhi ya viongozi na wapinzani wamekua ni sehemu ya matatizo ya kukwamisha ukuaji wa uchumi badala ya kuona hawana tena hoja za kuwafanya maarufu sasa wanaanza kupinga tu kila kitu tena kwa upotoshaji mkubwa sana na kwa viongozi baadhi baada ya musuala ynayogusa maslahi yao binafsi yawe ya familia na kisiasa kujipanga kwa makusudi kukwamisha mabadiliko.
Jana nimeshitushwa na msomi moja aliyebobea na mtu mashuhuri Jenerali Ulimwengu kuongea kitu cha kupotosha kabisa nashukuru Mh Mkapa alijaribu kumwelewesha kidogo suala la mabadiliko ya katiba ni suala muhimu sana kwa mustakabali wa Taifa letu ni suala ambalo halina budi kulikamilisha ili tuweza kuendena na mabadiliko ya kidunia yapo mambo mazuri kwenye katiba iliyopendekezwa na kwenye rasimu ya katiba yote yanazungumzika na kutekelezeka lakini huwezi kusema Rais mstaafu ashitakiwe kwa kupoteza mabilioni that is nonsense kwa mtu msomi na mwenye kuaminiwa na zaidi ya watanzania mil 10 wanaomfuatilia na mada zake nzuri kabisa kwenye Jenerali on Monday haiingii akilini kusema kwamba Serikali ilipoteza fedha kipindi kile sababu Jaji Warioba alifanya kazi yake vizuri,bunge la katiba kama lilikua na mapungufu still lilifanya kazi yake na bado kazi haijaisha tukiwa na kumbukumbu nzuri Mh Jakaya alishasema awali huu mchakato wa kutafuta katiba mpya nauanzisha lakini atakaekuja kama itakua ni kipaumbele chake ataumaliza ila ni suala zuri rejea hotuba ile ili kuweza kumsikiliza vizuri JK suala la katiba mpya si suala la siku moja kila mtu anajua hilo kama halikufikia malengo yake hilo ni suala jingine lakini kusema kwamba mchakato ulikosewa kabisa ni upotoshaji wa wazi na usiokuwa na mantiki
yapo mambo mengi pamoja na mazuriyaliyofanyika na mabaya pia yalikuwepo kutokea Uhuru na mabaya yale yakawa sehemu ya maisha ya watanzania na kuyaona kama utaratibu wa kawaida.
Tumemsikia Mh Mkapa jana alivyokiri kukosea kwenye uwekezaji kwamba awamu yake haikuwa na chombo cha regulate sheria za uwekezaji pamoja na mengine mengi anaweza kuja Mzee Mwinyi,Mzee Kikwete wote wakasema vitu walivyokosea ila havitatusaidia tunachotakiwa ni kusonga mbele maana havitabadilisha maisha ya watanzania mimi nilidhani Ulimwengu kwenye forum ile ya Kigoda cha Mwalimu angetumia kuhubiri uzalendo kwenye kujenga nchi na kuachana na siasa ambazo tumezifanya tokea tupate Uhuru.
Focus sasa iende kwenye kushauri ni jinsi gani nchi itafikia malengo na si kusubiri Serikali ishindwe ama tu tutafute kujijenga kisiasa au kijamii kwa kuona kila kitu kinakosewa hamna aisIyejua Developemt ni graudual change,huwezi kuniambia eti ndani ya mwaka moja au miezi kadhaa ila kitu kitakua kimebadilika fly overs,lami nchi nzima,maji,umeme,gas,mafuta,mashirika ya umma yanayozalisha kuzalisha kwa asilimia 100,ajira kuongezeka kwa asilimia 100 huo ni upotoshaji wa hali ya juu na haijawahi kutokea kwenye nchi yoyote duniani iliyoendelea.
tuwe wazalendo kwa matendo yetu na sio kwa maneno yetu
Nawatakia mfungo mwema wa MWEZI MTUKUFU WA RADHAMANI