Uzalendo unanajisiwa

justin mwanshinga

Senior Member
May 22, 2014
179
621
Uzalendo unaharibiwa kwa Uhamasishaji wa kiitikadi , kejeli , mipasho, matusi, uonevu , kutoyatenda yaliyo ya haki kwa tabaka la chini, kuwagawa, wananchi kwa misingi ya ukabila, ukanda , udini na itikadi .

UZALENDO haurejeshwi kwa kauli mbiu ,
UZALENDO unarejeshwa kwa kutenda HAKI tu maana tunu ya amani ni haki.

Huwezi ukamtukana mtu wa hadhi ya chini (mtawaliwa) ukategemea aambatane na wewe katika suala zima la kimaendeleo hasa ustawi wa jamii .

Watu wameharibu muda wao leo unawaambia hakuna ajira afu utegemee uzalendo !!
Hapo ni kujilisha upepo .

Kamwe huwezi kumuonea mtu halafu akupende , kamwe huwezi kumdhulumu mtu ( ulaji wa rambirambi ) afu akuhusudu .

Uzalendo wa taifa hili hasa kwa sisi vijana ni pale tutakapokubali kuyasimamia ya haki kwa ustawi wa watu wote .

Leo hii kwenye whatsapp groups, Jamii forum, Instagram , Twitter, fb watu hudiscuss watu badala ya masuala .
Hushambulia mtu (personal attack) badala ya kujibu hoja , wamekua wa vihoja badala ya issues .

Ajabu kuu waalimu wanafundisha nidhamu ya woga na kuwa wazumari badala ya kufundisha watu kuwa na fikra mtambuka zenye kuimarisha kuhoji na kuwa wanamapinduzi .
Mwaka 1967 wakati wa azimio la Arusha (Arusha Declaration) mwalimu Nyerere aliwaisema "The role of Teachers is to teach revolution" yaani kazi kuu ya mwalimu ni kufundisha mapinduzi .
Yaani kuwajenga wanafunzi katika suala zima la kuwaza masuala kuliko kuduscuss watu , kuwafunza watoto kuwa na weledi wa kuhoji mustakabali wa taifa na watu wake , kuwajengea uwezo wa kuwa na upendo na uzalendo kwa taifa lao na sio kuwafundisha kuwa waoga .

Inakera pale ambapo hata hatujui dira ya taifa maana viongozi wa ngazi tofauti tofauti wako busy kusaka sifa badala ya kuwatumikia raia .

Leo hii nchi ina mdororo wa kiuchumi , lakini wataalam wa mambo ya fedha na kiuchumi wako busy kisiasa na kusaka sifa .
Biashara zimekua ngumu , mzunguko wa pesa umekua mgumu , mabenki yanafungwa lakini hakuna anaejali zaidi tunaambiwa nchi inanyooshwa .

Huko kwenye ajira watu hawana uhamisho , wenzangu na mimi tunasugua gaga mtaani hakuna ajira eti dhambi kuu kusoma masomo ya sanaa .
Nani anajali !!

Uzalendo si kumlazimisha mtu aipende serikali bali ni kumshawishi aipende serikali kutokana na matendo yake .
Uzalendo ,
Ni kulipenda Taifa .

Wakati ukuta na muda ni mwalimu mzuri sana .

Mwanshinga Jr
 
Inashangaza sana,saa zima linapita lakini Uzi kama huu hauna wachangiaji sijui ni nini kimeikumba hii nchi,any way,ni kabisa ulichoandika kwasasa kinachoendelea ni ubakakaji mkubwa wa haki,watu wanapotea na hawapatikani,wakipatikana wanamazito sana ya kueleza,wataalamu wanapuuzwa na washenzi wanapata nafasi za kuwaongoza wenye akili,mwisho sio mzuri kabisa na muda utajibu yote haya.
 
Inashangaza sana,saa zima linapita lakini Uzi kama huu hauna wachangiaji sijui ni nini kimeikumba hii nchi,any way,ni kabisa ulichoandika kwasasa kinachoendelea ni ubakakaji mkubwa wa haki,watu wanapotea na hawapatikani,wakipatikana wanamazito sana ya kueleza,wataalamu wanapuuzwa na washenzi wanapata nafasi za kuwaongoza wenye akili,mwisho sio mzuri kabisa na muda utajibu yote haya
Dogo safi sana...!!! Tatizo jamii forum pia watu wanapenda udaku sana kuliko hali halisi..!!! Hatutafika mbele. Na tz ni nchi ya matukio. La makonda liliisha, mnalisikia tena bungeni? Ile kamati iliyo mhoji bungeni mrejesho?
 
Inashangaza sana,saa zima linapita lakini Uzi kama huu hauna wachangiaji sijui ni nini kimeikumba hii nchi,any way,ni kabisa ulichoandika kwasasa kinachoendelea ni ubakakaji mkubwa wa haki,watu wanapotea na hawapatikani,wakipatikana wanamazito sana ya kueleza,wataalamu wanapuuzwa na washenzi wanapata nafasi za kuwaongoza wenye akili,mwisho sio mzuri kabisa na muda utajibu yote haya.
Mkuu kuna tatizo
tukichangia na kuposti inakuja Error.
Mods watueleze kwa nini??
 
Back
Top Bottom