Katika mashindano ya kutafuta kushiriki kombe la AFCON 2019 Tanzania imepangwa group L ikiwa na Uganda, Cape Vede na Lesotho. Inabidi tuanze kuijenga tiu yetu ya taifa sasa. Mawazo yangu ni kwamba muonekano wa wachezaji wa michuano inayoendelea sasa wote wamepanda juu na wamejaza vifua kiasi kwamba vimo vya akina Kichuya na Mohamed Hussein havipo kabisa japo ni wazuri sana. Hawa waishie ligi za ndani tu!
Ushauri wangu kwa TFF, wakati wa kuandaa timu ya taifa, kigezo cha kwanza kabisa kiwe physical structure ya mchezaji. Weka kabisa minimum height na weight. Hakikisha mchezaji anauwezo wa kula kuku zima na chapati kadhaa. Awe na uwezo wa kusukuma na kuresist kusukumwa. Awe na uwezo wa kuruka na mbio. Awe na Umri usiozidi miaka 28. Baada ya hapo ndio mafunzo ya kimchezo yaanze, na wacheze kama timu sio kila mtu kivyake.
Kwa vigezo hivyo ngoja nianze kutaja kikosi naanza kama ifuatavyo, na nyie endeleeni:

- Kipa Deogratias Mnishi na Manura - Yanga/Simba
- Mbwana Samata - Greese
- Thomas Ulimwengu - Private
- John Bocco - Azam ( Sina hakika ya Umri) - (aongeze chakula na zoezi la kupanua misuri)
- Msuva - aongeze chakula
- Domayo aongeze chakula