Gutapaka
JF-Expert Member
- Nov 28, 2015
- 283
- 219
Historia inazungumza wazi kuwa baada ya Uhuru wa Tanzania nchi haikuwa na wasomi wengi hivyo serikali iliwajibika kuandaa nguvu kazi itakayoweza kulihudumia Taifa hili.
Hata hivyo, wasomi walipangiwa ratiba mahususi katika mtaala ambayo ilizungumza juu watu wanaoishia ngazi mbalimbali za elimu wataelekea wapi (walioshindwa wapi na waliofaulu wapi)
Baada ya kuhitimu masomo wasomi wote wa wakati huo waliingia ofisini Kama waajiliwa baada ya kutoka Jeshi la kujenga Taifa. Hii inamaana moja tu, wasomi waliandaliwa kazi za kufanya wakati wakiwa Darasani.
Mimi napata shauku Sana ya kujua mtaalamu aliyekuwa Afisa Rasilimali watu au Afisa utumishi wa wakati huo. Hakika mtu huyu alikuwa na uwezo wa kutumia utashi wake barabara. Alikuwa anatafiti, na kupendekeza uwepo wa mahitaji katika maeneo Kisha kuajili nguvu kazi yenye kuzalisha huduma yenye kuliongezea Taifa nguvu kiuchumi.
Sijui nini kimetokea hivi Sasa kwa maafisa Rasilimali watu huko wizarani mpaka kufikia hatua ambayo inasemekana Taifa hili halihitaji wataalamu zaidi kwa maana wapo wengi na wanakidhi mahitaji. Je hii inamaana nchi hii yenye watu wanaokadiriwa milioni 55 haiwezekani kupelelezwa na kuona fursa zitakazo wasaidia watanzania wenye ujuzi na wasio na ujuzi kujiajiri na kuajiriwa?
Ndio! Wizara ya fedha na uchumi lazima wakubali kufanya Tafiti ambazo zitasaidia kufichua fursa ambazo zingepelekea watanzania wakawaida kufaidika kupitia ajira binafsi zenye tija. Ikiwa Ni ukweli kwamba serikali imefikia kikomo Cha kutoa ajira za uhakika kwa wahitimu wake ili hali iliandaa kizazi za kutegemea kuajiliwa tu.
Wakati wa kuamua umefika Kama ilivyo kwa mataifa mengine yenye uchumi mkubwa. Kama tunaendelea kuwa na uchumi wa kijamaa wenye ukakasi wa kibepari basi tupitie upya mipango na mikakati yetu tukijiwekea Dira Kama taifa ili kuwa na namna Bora ya kufikia malengo yetu yanayohusisha nguvu kazi hasa vijana ambao ndio chachu ya maendeleo ya Kweli.
Tawala zetu zinadhihirishaje kushindwa kuandaa nafasi za ajira kwa ajili ya wasomi, ama kujiajiri au kuajiriwa na hatimaye wasomi wa nchi hii tumegeuka wapiga dili zisizo tarajiwa kabisa Kama vile Umbea, Unafiki, Kubet na uchafu mwingine.
Tusifarijiane kabisa kutokana na vijana wengi kukosa fursa za ajira Serikalini Kama yalivyo matarajio ya wengi wetu, imepelekea kuwepo kwa chuki dhidi ya serikali na kusababisha vijana wengi kukimbilia kwenye siasa ili kujitengenezea uwezekano wa kuajiriwa huko. Ni Kweli Maisha Ni siasa lakini yapo Mambo mengine mengi ambayo vijana tungefaidika nayo Mbali na siasa.
Kama serikali hii ipo tayari kuwatumia wasomi wa nchi hii basi isiache kuwekeza kwenye kilimo na viwanda vyake. Huko Kuna faida kubwa Sana kuliko hata kwenye ndege na Meli au hizo Tanzanite zenye ukuta.
Lakini kushindwa kwao kunasababisha wasomi wabet leo, watu wasahau taaluma zao na hatimaye kuwa na chuki na serikali yao.
Hakuna njia nzuri ya kuwafanya watu kuwa wazalendo tofauti na ile ya kuwatumia wao wenyewe Kama viungo muhimu kwa maendeleo ya Taifa lao hiyo huwapa watu taarifa namna wanavyothaminiwa moja kwa moja. Tofauti na hapo tutahubiri Sana uzalendo na kulaumiana kwa sababu lazima wasomi tukimbilie kwenye aina fulani ya umbea wenye mwamvuli wa kiharakati na kuandika proposal ili mkono uende kinywani.